Asante sana kwa hilo. Hata mimi kwa kusikiliza mafundisho yake redioni nimeona hilo kwamba anaona kuwa uchawi hauna uhalisia yaani haupo na yanayotendeka ni ujanja ujanja tu au mazingaombwe. Mazingaombwe ni tofauti sana na uchawi, japo yapo mazingaombwe yanayofanywa kwa msaada wa nguvu za giza.Dhana ya kupinga kinachoitwa Uchawi au Ushirikina, amekiandika kwenye kitabu chake kinaitwa 'Jinsi ya kuushinda Ulimwengu'. Nlikisoma miaka 13 iliyopita. Ishakuwa kitambo ila nakumbuka vizuri allivyoandika kwenye kitabu chake. wakati huo pia nilisoma kitabu chake kingine kinaitwa ' Maswali wanayobandikwa wakatoliki' Mle kachambua hoja moja baada ya nyingine kuhusu Ukatoliki. Huyu Padre huwa haamini kama kuna uchawi Duniani.
Nilikuwa mkoa flani padre mmoja kijana sana akiwa na miezi michache ya upadre akahubiri na kukemea sana wote wanaoamini katika uwepo wa uchawi. Alikuwa akisema; watu wanalala kwenye hizi nyumba zetu zilizojaa panya halafu wanaamka asubuhi wametafunwa miguu au wana chale mwilini zinazotokana na kuumwa na panya halafu wanasema ni wanga wamewachanja chale. Akiongea mengi na watu niliokaa nao benchi la nyuma walikuwa wakicheka na kusema huyu padre hajui kitu, hayajamkuta, amekulia wapi?
Mapadre wengi pia hawaamini uwepo halisi wa shetani na kazi zake. Wanafikiri shetani ni kielelezo tu kinachotumika kuelezea uovu. Na wengi wa mapadre hufikiri kuwa Mungu ni nadharia tu. Niishie hapo kwa sasa.