Timu ya Brazil yamtumia Yesu kuifunga Marekani

Jamani Yesu ni wa watu wote si wa walokole peke yao wala dini ya walokole. Mimi namwamini Yesu na amenitendea makuu katika maisha yangu lakini sijiiti mlokole wala si sali kwenye hayo makanisa yanayojiita ya walokole. Uzuri hata waislamu wanayoijua dini yao vizuri wanajua kwamba Yesu bin Mariam ndiye atakayerudi kuhukumu ulimwengu wala sio Mohamed.

Tumtangulize Mungu mbele kwa kila tufanyalo tutafanikiwa.Sishangai kilichotokea kwa Wabrazili.

Tiba

Sisi footballers wetu (Taifa Stars) nasikia wanatanguliza bangi - na bado waliifunga New Zealand!
 
Jamani hawa walokole wametoka wapi? Hapa bwana ni uwanja wa soccer hiyo kuhusu imani kila mtu anajua, sasa siasa za kuanza kutumobilize hapa si sehemu yake. Maneno yanaweza kua mazuri lakini ukayatoa sehemu isiyo staili yakawa hayana maana. So hapa tunataka uchambunzi wa soka tu, wenyekujua soccer wanatuelimisha tusio jua tunauliza then inakua burudani murua. Ukitata kuhubiri injili nenda www.dullnet.com.
Nawaunga mkono wote wanaosema hii si thread ya kuhubiri dini.
 
mechi ya jana ilikuwa balaa tupu sikuamini macho yangu ktk kipindi cha pili dk za majeruhi pale ambapo tulipachikwa mabao mawili mpaka timu yetu ya kimarekani ikaanza kuchanganyikiwa.
Kwakweli sikuamini !! Kilichotokea.
Wakati nashangaa kapteni wa brazil akatoboa siri kuwa ushindi wao umetoka kwa jesus,
sikuwahi kuwaza kama yesu unaweza kusaidia mpaka mpirani.

Hakika jina la yesu linauweza mkubwa sana.
Sasa timu yetu ya kimarekani ijipange upya kurudisha heshima.

naona umesahau kama marekani ni wakristo na wanamtumia huyohuyo unaemwita jesus sasa sijui imekaaje hio bora ingekuwa wamecheza na iran tungekuelewa duhhhhhh....pumba

kiboko yenu ni kibwetere na yupo njiani...
 
Baada ya mechi kwa mara ya kwanza maishani niliona Wachezaji wa timu ya 'Taifa' wakipiga magoti na kusali bila kujali madhehebu kama siyo dini,Wamisri pia walikuwa wakimkumbuka Mungu kila walipopata goli.Tanzania haiwezekani kwa vile kuna walioenda kwa babu kutambikia tayari hivyo kusali kutavuruga mambo.IESUS NAZARENUS REX IUDAEORUM.
 
inamaana hii come back ya brazil kwa usa ndio imetumika kuhubiri kiasi hiki? au inamaana hii ndio come back kubwa sana katika soccer mpaka watu wakaitumia kutolea mifano yote ya dini au? what about come back ya liverpool against ac milan ilikuwa nguvu ya nani? au kwa vile wa brazil walikuwa wana t shirt za "thank you jesus" ? sasa zile mechi zingine ambazo brazil huwa wanapoteza inamaana yesu anakuwa kawanyima ushindi au wanakuwa hawajaomba? in short the best team won thats all coz both teams prayed n after praying then u perform, u dont just sit back and wait for jesus to perform for u.team effort played a big part here.

ni mimi au mimi nimeandika alichosema Captain wao,
siko hapa kuhubiri bali nasema kweli hiyo kweli inaweza kukuweka huru ata wewe.
Nisipo hubiri mimi ata mawe yatahubiri maana huyo Mungu wa kweli (Yesu) anao uweza wakufanya chochote hana kikomo kamwe maana ni Mungu.
naona mpaka mnaanza kuniamisha kwenye jukwaa la dini.
 
Jamani mnaijua soccer kweli???? Ina maana Kakobe, mama Lwakatale (na waumini wao)wakicheza na Brazil nani ataibuka mshindi?? Naomba tusichanganye mada, tuongelee soccer na jinsi gani Brazil waliweza kucontain pressure ya wamarekani na kuweza kurudisha zile goli mbili na kushinda la tatu. Binafsi naipenda Brazil si kwa soccer zuri tu, bali pamoja na nidhamu ya ndani na nje ya uwanja. Hebu fikiria lile goli lililokataliwa na refa, ingekuwa ni Taifa Stars au Simba ingekuaje? Nafikiri pangetokea na mauaji ya kimbari!!

We need an entertaining and disciplined players like Kaka kule kwetu tz, kama tunataka kufika mbali. Na si bla bla za Simba, Yanga na TFF!
 
Mechi ya jana ilikuwa balaa tupu sikuamini macho yangu ktk kipindi cha pili dk za majeruhi pale ambapo tulipachikwa mabao mawili mpaka timu yetu ya kimarekani ikaanza kuchanganyikiwa.
Kwakweli sikuamini !! Kilichotokea.
Wakati nashangaa kapteni wa brazil akatoboa siri kuwa ushindi wao umetoka kwa Jesus,
Sikuwahi kuwaza kama Yesu unaweza kusaidia mpaka mpirani.

Hakika jina la Yesu linauweza mkubwa sana.

brazil.jpg

Sasa timu yetu ya kimarekani ijipange upya kurudisha heshima.

[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif][SIZE=-1]...te he he! hatari kubwa sana haya mambo ya imani, nyie wamarekani mngemtumia 'Liberty' mngeshinda.[/SIZE][/FONT]
 
mbona sion mnachobishania hapa?
wote waliomba kwa mungu mmoja, ila aina ya sala ilitofautina kwani wale wa usa walomba sala ndefu sana tena ndani yake kukawa na kulazimisha flani,
wale wengine waliomba sala fupi.
na ikumbukwe kuwa Mungu huwa anatoa kwa mda wake, si pale unapopiga magoti na kuomba utapata, wengi wenu hamjui jinsi ya kuomba, sala za kulalamika siku zote huwa matokeo yake hayaji haraka maana unalazimisha, Na mungu wa ibrahim,yakobo na isaka hayuko hiv, hawezi kukujibu.
kwa hiyo pale timu zote mbili ziliomba ila sala ikatofautiana kabisa, moja ilikuwa tulivu na nyingine ya kelele na kulazimisha.
 
.
Kwani hawa yesu wako wangapi?
.
Kila moja anadai yesu wake ndio wa kufuata!

Kuna yesu kweli au wajinga ndio waliwao!


Wanatuchanganya tu, sasa wanataka tumfuate Yesu yupi?

Nadhani tunalotakiwakufanya ni kutenda mema ambayo unadhani ukifanyiwa wewe litakufurahisha. Nadhani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetenda ya Yesu wa kweli bila kuwa na sababu ya kwenda Kanisani au Msikitini.
 
Hebu fikiria lile goli lililokataliwa na refa, ingekuwa ni Taifa Stars au Simba ingekuaje? Nafikiri pangetokea na mauaji ya kimbari!!

We need an entertaining and disciplined players like Kaka kule kwetu tz, kama tunataka kufika mbali. Na si bla bla za Simba, Yanga na TFF!


Umezidisha chumvi hapo Mzee! Hapa kwetu pia kuna wachezaji wana nidhamu sana kuliko ata Brazil.
 
Yesu ni yeye yule jene na leo na hata milele.....yesu afwatwi mpaka utakapo pata neema yake....ndipo utamuona yesu vinginevyo vigumu sana kumuelewa ni nani........

Zab 60:12

kwa neema yake tutafanya mambo ya ajabu.ajabu ikiwa ni pamoja na mambo yasiofikiriwa kutokea...amen???
Ukimfwata yeye hutoona njaa.kiu za dunian.....wish ningewaona wana jf wote wakiingia mbinguni siku ya mwisho akiwemo mwandishi

mungu akubariki ndugu
 
Back
Top Bottom