Timotheo Mnzava Ashiriki Maombi ya Kuombea Nchi ya Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,960
954

MHE. TIMOTHEO MNZAVA ASHIRIKI MAOMBI YA KUOMBEA NCHI NA VONGOZI WAKE & KUMUOMBEA RAIS SAMIA

Mbunge Jimbo la Korogwe Vijijini Mhe. Timotheo Mnzava ameshiriki Wiki ya Sikukuu ya Pasaka kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Dini, Chama na Serikali huku akiungana na viongozi mbalimbali kuombea Nchi ya Tanzania na viongozi.

Mhe. Mnzava Jumapili ya Pasaka Tarehe 09/04/2023 amewafuturisha Viongozi wa Dini, Viongozi wa Chama na Serikali wa Tarafa za Bungu na Mombo. Katika Tarafa ya Bungu hafla ya kushiriki Iftar imefanyika Wilayani Korogwe katika Bwalo la Shule ya Sekondari ya Bungu.

Aidha, Jumapili ya Pasaka, Mhe. Mnzava alifika Magamba Kwalukonge Kushiriki Uhitimishwaji wa mashindano ya Mpira wa Miguu yaliyopewa jina la "PANDA MITI CUP" yaliyoshirikisha timu kutoka Kata Tatu za Mombo, Mkalamo na Magamba kwalukonge.

Kabla ya kuhitimisha Mashindano hayo Mhe. Mnzava alipata nafasi ya kushiriki zoezi la Upandaji Miti na kuendelee kusisitiza suala la kutunza Mazingira, kuhifadhi na kulinda vyanzo vya Maji.

Vilevile, Jumapili ya Pasaka Tarehe 09/04/2023 Mhe. Mnzava alizindua Album ya Kwaya ya Ufunuo ya Kanisa Anglican la Mt. Cyprian Vugiri, Korogwe.

Mhe. Mnzava aliwapongeza vijana na kuwatia Moyo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kumtumikia Mungu kwa njia ya Uimbaji. Pia amewashauri kuvifanya Vikundi vya Kwaya kuwa vikundi vya Uzalishaji.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-11 at 17.51.19(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-11 at 17.51.19(1).jpeg
    96 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-04-11 at 17.51.18(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-11 at 17.51.18(1).jpeg
    104 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-04-11 at 18.58.31.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-11 at 18.58.31.jpeg
    46.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-04-11 at 18.58.31(3).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-11 at 18.58.31(3).jpeg
    62.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-04-11 at 18.58.32.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-11 at 18.58.32.jpeg
    44.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-04-11 at 18.58.33.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-11 at 18.58.33.jpeg
    70.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom