SI KWELI Tilisho wametangaza nafasi za wahudumu wa Mabasi yao pamoja na Wakatisha tiketi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari Wadau,

Nimekutana na tangazo la kazi likionesha kuwa Kampuni ya usafirishaji ya Tilisho inahitaji Wafanyakazi kwa nafasi ya Wakatisha Tiketi na wahudumu wa ndani ya Mabasi.

Nimepata mashaka baada ya kuona ukilifuata tangazo hili ndani yake linahitaji usambaze link kwenye magroup ya WhatsApp na Facebook ili kuendelea hatua inayofuata.

Je, kuna ukweli juu ya Tangazo hili?

Screenshot_20240304-123924.jpg
 
Tunachokijua
Tilisho Safaris ni kampuni ya usafirishaji yenye asili ya Rombo, Tanzania. Kampuni hii hutoa huduma za usafiri wa Mabasi katika mikoa ya Dar es Salaam, Rombo, Arusha, na Moshi.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Februari 2024 kupitia mitandao ya kijamii kumeibuka tangazo la nafasi za kazi likidai kuwa kampuni ya Tilisho inatafuta Wafanyakzi katika nafasi za Wakatisha tiketi, Wahudumu wa ndani ya Mabasi, Makondakta, wafanya usafi ndani ya gari na waosha magari. Jamiicheck imefuatilia tangazo hilo na kubaini kuwa ukifungua kiunganishi chake (link) na kujaza jinsi na umri wako tangazo hili linakutaka usambaze link hiyo kwenye magroup ya WhatsApp na Facebook na mitandao mingine ili kuendelea hatua inayofuata. Tazama kwenye picha hapa chini:

1709554830199-png.2924312

Upi ukweli kuhusu uvumi huu?
JamiiCheck imefuatilia ukurasa rasmi wa Instagram wa kampuni ya Tilisho na kubaini kuwa hakuna tangazo lolote la kazi lililotolewa na kampuni hiyo kwa mwaka huu 2024 kama inavyodaiwa na tangazo hilo linalosambaa.

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imebaini kuwa mnamo Februari 8, 2024 Kampuni ya Tilisho kupitia ukurasa wake wa Instagram iliweka taarifa kukanusha kuhusika na tangazo hilo la kazi. Kupitia taariffa hiyo kampuni ilitumia picha ya tangazo hilo na kuiwekea alama ya 'Fake' kama inavyoonekana hapa chini:

1709555941544-png.2924317
Zaidi ya hayo, JamiiCheck imebaini kuwa Machi 2, 2024 kampuni ya Tilisho kupitia ukurasa wake wa Instagram ilitoa taarifa ya pili kukanusha kuhusika na tangazo hilo. Sehemu ya ujumbe wao katika kanusho hilo ulieleza:

"Hatuhusiki na chochote kinachoendelea na hizi taarifa lakini tunaendelea kulifanyia kazi hili jambo kwasababu sio salama na halileti sura nzuri na njema kwenye biashara na jina la Kampuni yetu"

1709556212577-png.2924320

Picha ya taarifa ya Tilisho ya Machi 2, 2024
Aidha, JamiiCheck imebaini kuwa mnamo June 2, 2023 kampuni hiyo iliwahi kutoa taarifa nyingine ya kukanusha taarifa ya mtu aliyedaiwa kutangaza ajira kupitia kampuni yao.

1709557206947-png.2924341

Taarifa iliyokanuswa June 2, 2023

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo hapo juu JamiiCheck imejiridhisha kuwa tangazo hilo linalosambaa halina ukweli na linapaswa kuepukwa.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom