TIGO yazidi kufulia kanda ya ziwa/mwanza.

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Kampuni ya simu za mikononi ya tigo imezidi kuporomoka kibiashara katika maeneo ya kanda ya ziwa hasa mkoani mwanza kutokana na kutokuwepo hewani kwa muda mrefu. Ni takribani wiki moja na zaid mtandao wa tigo unapatikana kwa kusuasua hapa mwanza. Wakazi wengi wa kanda ya ziwa wanatumia mtandao wa vodacom na airtel (zain). Kutokana na kulitambua hilo kampuni ya tiGO imekuwa ikitoa promoshen mbalimbali kwa wakazi wa kanda ya ziwa ili kuwavuta kibiashara. Pamoja na promoshen hizo tigo wameshindwa kuboresha upatikanaji wa mtandao wao hata maeneo ya mjini. Takriban miezi minane au zaid iliyopita kampuni hiyo ya tigo ilianzisha kitu kinachoitwa extreme kanda ya ziwa ambapo mteja anakatwa sh. 200 na kupewa dakika 20 za bure ambazo wangezitumia hadi sa 12 jioni. Baada ya kuona promoshen hiyo imeshindwa kuwateka watu wa kanda ya ziwa tigo waliamua kuongeza dakika ambapo kwa takriban mwezi mmoja sasa extreme kanda ya ziwa inampa mteja dakika 33 kwa sh. 200. Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mwanza hivi sasa wanailalamikia kampuni hiyo kwani mara nyingi baada ya wao kujiunga na extreme hiyo mawasiliano ya simu tigo kwenda tigo au kwenda mitandao mingine yanakatika. Mpaka muda huu napoandika habari hii tigo haiko hewani tangu asubuhi, nadhani wakazi wa mwanza ni mashahidi. Kwa wale wenye ndugu, jamaa, marafiki, wake, wachumba au wapenzi walioko mwanza msishangae mtakapoona watu wenu hawapatikani kwenye namba zao za tigo ni tatizo kubwa la kimtandao ambalo limewasibu na wengine wengi wameapa kuachana na tigo na kujiunga na vodacom au airtel kwa kuhofia kupoteza fursa mbalimbali zikiwemo nafasi za kuitwa kwenye interview. Wakazi wawili niliozungumza nao walisema wametuma maombi ya kazi na wanategemea muda wowote kuitwa kwenye interview kwa njia ya simu na bahati mbaya kwenye barua zao za maombi walijaza namba zao za tigo ambazo kwa muda wa wiki moja sasa zimekua zikipatikana kwa masaa machache.
 
Acha kabsaa mara nyngne cm zinaingliana kuna cku nlimpgia baby wngu nkackia sauti ya kidume ilikuwa ugomvi mkubwa cku nyngne alipokea mama ndo nikajua tigo wenge
 
Mimi niko musoma hapa matatizo tupu especially linapokuja swala la mahusiano mtu wako yuko kwa mfano dar ankutafuta sdiku nzima hupatikani linakuwa balaa,tigo lile tangazo lenu mko nchi nzima plse toeni lingine linaloonyesha mnapatikana dar tu kwa uzuri coz kuna kipindi nilikuwa singida kwa miezi miwili ukitoka nje kidogo tu ya pale town hupatikani kwenye simu
 
Tena singida ndo usiseme mimi nina jamaa zangu wawili wakishaingia singida tu wanahamia airtel, wakirudi dar unawapata kwenye tigo.
 
Hamieni Vodacom jamani mbona mnapata shida mtume pesa M-PESA kwa wapenzi wenu!
 
Back
Top Bottom