Haya makampuni ya Simu ya Tigo na Airtel yanafanya zoezi la usajili wa laini kuwa gumu kutokana na utaratibu wao wa kipekee waliojiwekea.
Ukienda kusajili laini Vodacom unatakiwa uoneshe kitambulisho chako cha NIDA pekee alafu unawatajia namba zako za Vodacom unazotaka kusajili (hata kama ni tano zote unawatajia palepale moja baada ya nyingine).
Lakini kwa upande wa Tigo na Airtel wao wanataka namba zote unazowatajia laini zake ziwe kwenye simu wakati huohuo. Sasa unakuta mteja ana laini nyingi za mtandao huohuo na moja tu ndio inakua active kwenye simu kwa mudahuo. jibu wanalokupa ni kwamba hawawezi kuzisajili hizo laini.
Nimewauliza kwanini utaratibu wao ni tofauti na Vodacom wakati mchakato wa kusajili laini ni zoezi la pamoja la kitaifa hawakunipa jibu linaloeleweka.
Walichoniambia ni kuwa ukimaliza kusajili laini yako iliyopo kwenye simu ujumbe unakuja wenye namba ambazo huyo wakala wa usajili anatakiwa ajaze.
Lakini kwa Voda ukishamaliza kuwatajia namba zako inakuja confirmation message/ meseji ya uthibitisho wa kukamilika kwa usajili basi na sio kingine.
Kwa maoni yangu naona Tigo na Airtel mnaleta usumbufu kwa wateja na kufanya zoezi la usajili hasa kwa mitandao yenu kusuasua huku wenzenu Voda wakiendelea kufanya vizuri kwa sababu wanafanya mambo kuwa rahisi yaani unaenda na kitambulisho chako cha utaifa au namba ya NiDA,unawatajia namba zako zote za mtandao husika kazi inakua imeisha.
Leo pia nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi kuwa hadi sasa laini zaidi ya milioni 30 nyingi kutokea makampuni haya hazijasajiliwa huku zikibakia wiki 13 pekee kabla zoezi halijaisha.
Karibuni tujadili