Nida na watu wa mitandao acheni ubabaishaji katika suala la kufuta usajili wa namba

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,219
2,825
Mbona kusajili mnatuma mawakala mpaka maporini huko wanafika na usajili unafanyika bila mlolongo wowote iweje kufuta namba mpaka mtu afike kwenye duka la mtandao husika?

Yaani mnaendekeza faida tu kwa upande wenu bila kujali madhara kwa mteja na jamii yake au taifa kwa ujumla! Kumbukeni baadhi ya mawakala wenu siyo waaminifu na mteja kuwajua ni kazi sana au asiwajue kabisa!

Mtu anataka kusajili laini moja wakala anafanya uhuni anasajili laini hata tatu bila mteja kujua. Baadae anaenda kuziuza laini hizo nyingine halafu kesho mteja akigundua hawezi kuifuta namba eti mpaka afike dukani kwenu! Huu kama siyo ubabaishaji ni nini sasa?

Laini hizo nyingine zinaenda kutapelia watu, nyingine zinaenda kucheat ndoa za watu, nyingine kufanyia ujambazi na kadhalika. Pia laini hizo zinazuia mmiliki wa namba ya nida baadhi ya huduma muhimu kwa mfano akitaka kusajili namba ataonekana ana mamba nyingi kumbe nyingine siyo zake (sijawahi kushuhudia lakini nasikia kuna ukomo wa idadi ya laini katika kusajili)

Lengo la serikali ni kila mtu (Mtanzania mtu mzima) awe na namba yake ya nida hivyo kila mtu ana wajibu wa kushughulikia swala la kupata namba hiyo. Kwa mantiki ni kwamba nyinyi watu mnasababisha watu waendelee kubweteka tu kwa kuona kumbe namba ya nida haina umuhimu wowote

Tuachane na maelezo mengi, ruhusuni mtu aweze kufuta namba kwa kwa hiari yake kama ilivyo kusajili kwa hiari yake
 
Back
Top Bottom