Tibaijuka akataa kupokea shilingi 200 millioni

Tuzo hii ni sawa na ya Nobel ambapo pesa hupokea anayeshinda mchujo. Tuzo hii si ya UN na kimaadili UN haitoi zawadi ya pesa kwa mtu!!

Alichofanya ni blackmailing. Mtoa tuzo ni Prince wa Kuwait na Waziri Mkuu. Prof. Tibaijuka kaona nafasi ya kupata pesa nyingi zaidi kwa ajili ya maafa na anaweza kuwa ameelekeza pesa hizo zipelekwe huko ili kusaidia jambo linaloweza kufanya mtoaji kuongeza.
 
Kugeuza geuza maneno - kwani fedha alizo pewa Rugemalila zilikuwa ni haramu si zililipiwa kodi stahiki? Taifa hili lina mamlaka gani ya kuhamulia wenye fedha halali wampe nani wamwache nani - Tibaijuka alifanya kosa gani la jinai zaidi ya watu kutokana wivu na roho mbaya kumzulia mama wa watu mambo chungu mzima na fitina tu, mbona mzee Mengi aliwahi kumpatia fedha Prof. Tiba kwa madhumuni kama ya Rugemalila mbona Serikali ya awamu ya nne ilikaa kimya kuhusu fedha za Mzee Mengi - ya Rugemalila ndiyo yakakuzwa out of proportion na wengi walio pewa fedha na Rugemalila walitiwa msukosuko kweli kweli - hata Rugemalila angehamua kugawa fedha zake sokoni kama njungu kwani tatizo ni nini- zi zake?

Mama wa watu katiwa msukusuko na kuhojiwa maswali yasiyo na mantiki eti "fedha za shule yako kwa nini hukushirikisha Bodi" - Serikali ilitaka imwigilie mpaka jisi ya ku-run shule ambayo ni ya kwake binafsi (Private). Ukosefu wa msimamo ya Serikali ya nne kuhusu suala hili ukawaondoa Prof. Tiba na Prof.Muhongo watu ambao walikuwa na umuhimu wa pekee Serikalini wakatemwa kwa shinikizo lisilo na mantiki hata kidogo zaidi ya fitina tu na kugeuza geuza maneno ili wapate kisingizio cha kuwahengua.

Sina shaka after shock ya Tsunami iliyo mpata imemfanya a decline tuzo lililo halali kwake - si kama tuzo la Nobel tu, sasa tatizo ni nini kwani - au alijua watu watanza tena kumzulia mambo.
Naona unatokwa povu jingi huku ukiandika huu utumbo; sina shaka na hela aliyotoa mzee mengi sababu anajulikana wazi kwa kutoa misaada kila mara tofauti na rugemalila ambaye hata sumni hajatoa kuchangia maafa ya bukoba, umegusia kuwa mama tibaijuka alipewa hela na rugemalila; kwa taarifa yako na baki na kumbu2 kichwani mwako " hela aliyopokea mama tibaijuka kutoka kwa rugemalila ni rushwa".
 
By Raymond Kaminyoge, Mwananchi

Dar es Salaam. Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anne Tibaijuka amesema amepata tuzo nchini Marekani ikiwa ni kuthamini mchango wake akiwa Umoja wa Mataifa lakini akakataa kuchukua fedha dola 100,000( zaidi ya Sh 200 milioni) ambazo huambatana na tuzo hiyo.

Alisema alikataa kupokea fedha hizo kwa sababu maadili ya nchi yetu hayaruhusu kupokea zawadi kama hiyo.

Alisema lakini aliwaeleza kwamba katika mkoa anakotoka kumetokea tetemeko la ardhi na kuna maafa.

Alisema wao wataamua cha kufanya lakini yeye binafsi amekataa kupokea fedha hizo.

Its too late.......kama ni kuchafuka alishachafuka siku mingi.......angekataa zile za mboga
 
Hee Mama Tiba: Kwani si KILA KIINGIACHO SI HARAMU BALI KITOKACHO? Pokea Mkwanja huo. maandiko yanakulinda.
 
Mwenyekiti hana Mamlaka ya kumvua uanachama, msifananishe CCM na magenge yenu ya Kisiasa!

Acha ulofa we kenge maji, mzee wa hapahapa aliposema kwenye mkutano wa ccm kama ingekuwa ni yeye wanachama wanaimba wana imani na mtu fulani angewafukuza wote, alimaanisha nini?
 
Anayesema hakupokea ni mwongo kwa sababu Tibaijuka ameagiza fedha hizo zielekezwe kwenye maafa Kagera. Kitendo cha kutoa maagizo zielekwe wapi ni kupokea. Angeweza kuelekeza vinginevyo.
 
Mambo mrngine yanashangaza .Huyu. mama sehemu ya wapiga kura wake wamekumbwa na tetemeko na sijasikia popote pale kama ameshatoa msaada wowote kwa watu hawa.Si angechukua hiyo hela na akatuingizia kwenye acc ambayo mkuu wake wa mkoa anaonekana anaitangaza kila sku kwenye luninga? Maana najua hana haja na hela ya mboga.
 
Habar za jioni magwiji,
Mkichunguza kwa jicho la ndani ya utosi mtaona kwa ukaribu kabisa mbio na heka heka za mama huyu profesa katika Media za Ndani na Nje ya Tz akijieleza,kujitetea...
kwa lengo la kujisafisha....
Alianza na voice of America, akaja BBC, Mara kaibukia kwa Muhcn Mambo TV 1 ndani ya mawazo pevu...
Stori anayoinadi ni ile ile kana kwamba anawapa waandishi maswali ya kumuulza,...Kisa eti kwa sabb alipata tunzo huko ughaibuni ilio ambatana na FEDHWAAAA sasa yy madai yake etiiij ameuchunia mpunga na kujinyakulia tuzo peke yake...Hoja yke ni kuwa kama anauwezo wa kukataa mamilioni hayo kwann tumuone alikuwa na NIA MBAYA /KAIBA fedha za escroooo...Kwan anashida gan mpaka afanye hvyo...Lkn anasahau kuwa kilichotangulia ni ukwapuaji huo wa jasho La wa Tz ndipo akaja kukataa hzo fedha,ambaz kisingi CC tunamuona ni mtu alietosheka na alicho tupokonya ndo mana hzo nyengine haztakiii,[HASHTAG]#HATUKUELEWI[/HASHTAG] NA WALA HAWATOKUELEWA#
Eti amefanya kaz na WAZUNGUA na wanamjua sio Mwizi xx inakuaje wazungu wanaskia eti KAIBA FEDHWAAAA,Lkn amesahau kuwa wazungu hawashangai kuiba kwake bali wanamshangaa njia aliotumia kuikwapua hio Ngawira....
Sipendi kuwachosha ila nawaomba mumshauri kuwa hata atumie MEDIA za dunian kote,Dhambi ameshaifanya na hawez kuifuta ,kilichobak akiri tu ndo atapata PEACE OF MIND...
[HASHTAG]#MAMA[/HASHTAG] PROFESA PUMZIKA XX HAWATAKUELEWA#
 
Aziungamaye dhambi zake atasamehewa
Tena heri mtu yule ambaye Yesu hamuhesabii kuwa na dhambi yaani kamsamehe dhambi
 
Back
Top Bottom