bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,355
- 6,802
Hhm Nakubaliana na wewe kuhusu uchafu wa jiji hili la Dar ambao ni wa kuaibisha. Nadhani wengi wetu ijapokuwa tunajifanya tumestaarabika lakini kwa kweli bado tunao ushamba ndani ya mioyo yetu.
Hata na mimi huchukia sana kuona mtu anafungua kioo cha gari na kutupa chupa au takataka nyengine barabarani bila ya aibu. Mimi nikiwa nyuma ya gari aina hilo humuwashia taa kama ishara ya kutopendezewa na lile alilolifanya, ijapokuwa inawezekana sana yeye mwenyewe asielewe kusudio langu.
Mfano mwengine unamwona mtu mtanashati anaishi kwenye jumba la fahari huko Mbezi beach lakini ndani ya compound yake bado kuna ng'ombe na mbuzi na kuku ambao anafuga. Jamani sisi majirani huwa munatukera sana lakini hatuna la kufanya maana hayo mapumba munayolishia wanyama ndiyo yanayoongeza idadi ya mapanya kwenye nyumba ya mfugaji pamoja na jirani. Unajitahidi kununua sumu ya panya na kufanikiwa kucontrol
Na ng'ombe hao utakuta ameajiri kijana anawatembeza barabarani eti kutafuta majani na mwishowe kusumbua madereva na hata wapita njia.
Musijitetee kwamba eti unapunguza makali ya maisha, kweli ungeweza kujenga nyumba nzuri kama huna fedha za kumwaga?