The Worlds Dirtiest Cities!

Ethiopia wamefulia kuliko Bongo, we nenda Addis, Kampala, Bujumbura, Kigali hivyo vimiji vyote viko kama vile uko mkoa yaani kumechoka siyomchezo. Barabara zao zimejaa mashimo, traffic lights kwao ni dili yani wapowapo, huwezi ukafananisha na bongo hata kidogo. :eyeroll2:

Mr. Me nadhani hujawahi kufika Kigali, kule hata mfuko wa plastiki huwezi kushuka nao. Yaani ni pasafi sana.

Bujumbura nimewahi kufika na sijaona kama ni pachafu kuliko Dar.

Dar ni kiboko ya uchafu bwana, utaona watu na magari ya kifahari wanafungua vioo na kutupa vitu barabarani bila ya aibu yo yote. Au jaribu kusafiri nyuma ya daladala au magari ya abiria ya mikoani, watu wanajitupia ovyo taka bila ya kujali. Mitaro yote imejaa maplastiki.

Ni Keenja tu ndiye aliwahi angalau kuweza kuweka mji huu katika hali ya usafi.
 
Kigali inaweza kabisa kuingia katika miji safi Afrika na kuchukua namba na katika miji misafi duniani basi inaweza kabisa kuwemo katika top 20. Nilikuwa huko mwaka jana nilishangaa sana jinsi mji ulivyo msafi kupita kiasi. Kagame kafanya kazi nzuri sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom