The role of collective ministerial responsibility and accountability of our leaders

EmeraldEme

Senior Member
Mar 8, 2012
116
20
Ndugu zangu, mimi nimekuwa mkereketwa sana wa siasa za hapa kwetu na jinsi mifumo ya utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wetu na wizara zao zinavyoweza kufanya nchi ika prosper au kushindwa kuprosper.tumeona baadhi ya wizara zikivurunda, na mawaziri wao badala yake wakahamishwa kutoka wizara moja kwenda nyingine. Nakumbuka Mheshimiwa Raisi ameshabadilisha baraza la Mawaziri kama mara 2 hivi.Swali langu ni kuwa, itafika lini viongozi wetu kuwa collectively responsible for the actions za wenzao au za subordinates wao? Hivi kuna kipindi kweli tutapata viongozi wa ku feel kuwa wanahitajika waadhibiwe kwa niaba ya wenzao au hata wang'atuke kwa sababu ya wenzao? Nimeshuhudia Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi aliwahi kung'atuka kipindi flani akiwa Waziri. Pia Mheshimiwa Lowassa alijiuzulu either kwa shinikizo au kwa kuamua mwenyewe kwa ajili ya maslahi ya Nchi.Leo hii wapo wengi tu viongozi wameshindwa kufanya hayo, tuna mfano mzuri bado tuna msiba na makovu juu ya vifo vya wenzetu karibia 300 ambao walifariki kutokana na mgomo wa madaktari ambao chanzo chao amongst the many ni kutokutimiziwa maslahi yao. Nilidhani kiongozi mzuri angekiri kuwa Wizara yake imemshinda hivyo ang'atuke kupisha wenye uwezo waongoze, ila sivyo ilivyokua badala yake pakawa na vuta nikuvute za hapa na pale na hatimaye issue imekuwa overtaken by events, na sasa ni kama imeanza kusahaulika. Nalileta kwenu wanajamii ili tuweze kulidiscuss kwa kina hili suala.NB: I stand to be corrected where necessary.
 
Back
Top Bottom