Rungu
JF-Expert Member
- Feb 23, 2007
- 3,932
- 1,726
Si rahisi kwa sababu karibuni wote walimsoma Marcus!...hebu nionyeshe kiongozi mpigania UHURU mwafrika ambaye hakusukumwa na changamoto za Hayati Garvey!
Si rahisi kwa sababu karibuni wote walimsoma Marcus!...hebu nionyeshe kiongozi mpigania UHURU mwafrika ambaye hakusukumwa na changamoto za Hayati Garvey!
Samahani, sidhani ya kwamba unajua unachojadili.mi naomba hitler azaliwe tena kwenye nchi yetu tu basi sio kwa dunia nzima
Sidhani ni vile. Vita Kuu ya Pili iliharakisha kushuka jwa nguvu ya Uingereza na iliharakisha 1) kutokea kwa Marekani iliyoona ukoloni kama mchezo bila faida 2) ilifanya Urusi ya Kikomunisti kuwa nguvu ya kimataifa na kuongeza wasiwasi juu ya ukoloni shauri ya tishio la ukomunisti.Kuna mkondo wa mawazo kwamba ingawa Adolf Hitler alisababisha maafa makubwa kwa kuanzisha vita kwa sisi waAfrica hiyo ilikuwa kama baraka kwa sababu baada ya vita nchi za wakoloni zilielemewa kiasi cha kwamba ilikuwa rahisi kwa waAfrica kupigania uhuru. Je hii imekaaje?
Hapo sijakupata vizuri Mkuu...Marekani iliyoona ukoloni kama mchezo bila faida
Mbona bado kuna ukoloni mamboleo?Hakika ukoloni usingedumu hadi leo
Hapo sijakupata vizuri Mkuu
Mbona bado kuna ukoloni mamboleo?
kwa ufupi nataka nchi itawaliwe na dikteta hata kwa miaka mitano tu kwa sababu wakubwa wamejisahau au unabisha?Samahani, sidhani ya kwamba unajua unachojadili.
a) Ukitaka nchi yako awe na "Hitler" tazama huyu alifanyia nchi yake alichotawala: mamilioni ya watu walikufa, mamilioni wajeruhiwa kwa maisha, robo ya nchi imechukuliwa na majirani, wakazi (milioni 10 Wajerumani kutoka majimbo ya mashariki yaliyotwaliwa na Poland/Urusi) kufukuzwa kama wakimbizi, nchi yote kugawiwa kwa miaka 40. Halafu wanasayansi bora kufukuzwa, kuuawa au kufanywa wakimbizi (tangu Hitler Kijerumani si tena lugha ya sayansi no.1 duniani) Je, una chuki kubwa dhidi ya nchi yako kuitakia "Hitler mpya"??
b) Je unajichukia kama Mwafrika?Hitler kwa Afrika inamaanisha fundisho katika shule eti watu weusi ni nusu-wanyama, wanafaa kwa kazi ya mkononi ngazi ya chini pekee na ukoloni wa kudumu (ila tu si ukoloni tamu kama Waingereza!).
Si nchi karibu zote za Afrika zilitawaliwa na madikteta tangu uhuru - imesaidia nini? Kinyume chake!kwa ufupi nataka nchi itawaliwe na dikteta hata kwa miaka mitano tu kwa sababu wakubwa wamejisahau au unabisha?
Sidhani kama ni sahihi kukubaliana na hawa watu katika kuchambua swala zima la ukoloni manaake wao ndio walikuwa wenyewee!Soma hii taarifa ya majadiliano kati ya raisi Roosevelt (Marekani) na Churchill mwaka 1941 walipokutana kabla ya Marekani kuingia vitani.
Kwangu hatua kubwa ni kuendeleza Kiswahili. Fikra zinafuata lugha na maneno tunayotumia.Sidhani kama ni sahihi kukubaliana na hawa watu katika kuchambua swala zima la ukoloni manaake wao ndio walikuwa wenyewee!
Tatizo nilionalo ni kwamba zile vuguvugu za kuhamasisa kujitambua na kujikomboa kifikra zilizokuwepo mara baada ya uhuru hivi sasa zimeyeyuka na badala yake akili mgando inatawala barani Africa! Nawasilisha tu.
Hapo umenena!Kwangu hatua kubwa ni kuendeleza Kiswahili
Sujui kama umesoma. Sijawahi kusikia ya kwamba kusoma na kuelewa ni kukubaliana.Sidhani kama ni sahihi kukubaliana na hawa watu katika kuchambua swala zima la ukoloni manaake wao ndio walikuwa wenyewee!.
Hayo majadiliano ya Roosevelt & Churchill sijayasoma. Nadhani ni vyema kukubaliana kutokukubaliana katika swala hili. Hii itasaidia kutokupotezeana muda.Sijawahi kusikia ya kwamba kusoma na kuelewa ni kukubaliana.
Hitler alikuwa mnyama sana na wajerumani wenyewe hawataki hata kumsikia manake kawachafulia historia dunia nzima. Cha kushukuru ni kwamba alishindwa vita zote mbili na kupelekea ujerumani kugawanywa kwa mataifa manne. Kama ageshinda vita nadhani wafrika tungeuwawa wote kama wayahudi halafu Africa ageuze mashamba au holiday camps. Kwa hitler binadamu ni mzungu mwenye mwonekano wa Arier peke yake, kama huna muonekano wa ki arier wewe kwake ni trash. Japo yeye mwenyewe hakuwa Arier... lol
Habari zako kuhusu Hitler ni haba sana.mzee hitler hakushindwa vita kwa uwezo, its just by number of allied soldiers, sometime germans were running out of bullets then they get killed, they had the best weapons and best generals, there tactic are used even by today by major powers! yes hitler was bad on one side only of killing jews apart from that he was just a good leader who believe in super-race theory. its not bad kila kitu kina level yake, mbona hata hapa tz wahaya na wachaga wanajiona ni watu wa superior race kuliko labda watu wa pwani etc
hitler never thought of colonising africa even a bit! he never wanted some cheap labor like other European countries he wanted pure german breed ( aryan race-considered to be superior race of people)
Kwa ninavyofahamu mimi kwanza Hitler akuwa hana niya ya kutawala Africa yote.
kama sikosei aliipenda sehemu ya north africa [Tunusia,moroco na Egypti kidogo.
Huko alimweka kibarakawake fulani aliyeitwa Romel na kuliongoza jeshi la kinazi
kuwaondoa wakoloni wengine ili yeye awe kwenye pawa kwa faida ya Hitler.
Pili pamoja na ukatili wake wote aliyowafanyia wayahudi milioni 6,Hitler aliipenda sana nchi yake
na raia wake. Watu kama HIMLER,GORGO,ROMEL na Hitler mwenyewe walihakikisha kwanza Ger
many na watu wake wanakuwa safe na mengine baadae. Na alikuwa na future ya kuona nchi yake
oneday inakuwa super power. Sema uchokozi wake kwa poland,rusia,france,italy na marekani ndiko
kulikomponza. Stallin,Mousalin,Chuchirl na Nicksoni waliamua kuungana na kumtoa kwenye uso wa
dunia!. Tafauti na viongozi wetu wa kiafrica wanaochukia raia wao na kuzitafuna mali zote ndani ya nchi
kwa faida yao! enzi ya Hitler hawa wote wangenyongwa tu pummmmbffffu
Hitler alikuwa na ndoto za "Third Reich" unaelewa hili? Alitaka kutawala dunia nzima.
Hitler alikuwa na ndoto za kutengeneza a "master race" na kuondoa watu asiowataka, alianza na Wayahudi, alichukia weusi, kwa nini unafikiri asingetaka kuua weusi na wengine kuwafungia katika utumwa wakiwafanyia kazi hawa wa "master race" ?