The Commander In Chief Test: Membe, Sitta and Lowassa

nafikiri C-I-C hashughuliki na migogoro midogo ambayo kwanza Diplomasia inahitajika,ndipo Mh. Membe anapoingia.Bunge lina kazi ya kuisimamia Serikali,na Mheshimiwa Lowassa alichofanya Bungeni ni kutimiza wajibu wa Bunge kuishauri Serikali.Sitta alikuwa anakaimu nafasi ya Pinda,na aliyosema ni maneno ya kidiplomasia pia maana Malawi hawajasogeza Jeshi ziwani na kwa kweli kama wazamiaji wa kuokoa waathirika wa ajali majini hatuna, hakika Malawi wakiweka Manowari hapo Nyasa,utaona watu wakikimbia hadi Dar kwa miguu.
Hapo hakuna mmoja wao anayefanania na Amiri Jeshi Mkuu,maana tishio bado ni kama na hakuna.Lakini kwa mwanasiasa kila fursa unayompa atafanya siasa!Iwe bungeni,msibani kanisani,msikitini hata kwenye baa!
 
Membe alianza vizuri alipokuwa anaotoa msimamo wa serikali kuhusu suala hilo lakini alimalizia vibaya kwa kuchekacheka wakati anahitimisha. Vinginevyo msimamo huo aliosoma kama alishiriki ulikuwa mzuri.

Sitta alionyesha kitu ninachokipenda kuonyesha uthabiti unapojadili au kutoa msimamo katika masuala ya msingi.

Ipo haja ya hii staili ya kucheka wakati wa kuzungumzia masuala nyeti ya nchi tukianzia na mkuu wa kayu, Membe, waziri wa fedha, na wengineo ya hao wanaohusika kufanya hivyo kuitolea maelezo taili yao hii.

Lowassa sijamfuatilia kuhusu suala hili.

Vinginevyo kati ya Membe na Sitta bado na M"bookmark" kama anayefaa.
 
Back
Top Bottom