Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
- Thread starter
- #61
Unanikumbusha pale ambapo East China juzi tu wamejenga THREE GEORGES project wakidhani ndio mwisho wa mgao wa umeme lakini leo hii wanakosa umeme wakati West China wana umeme hawajui waufanyie nini. Mimi naona Projects za 100MW ni bei nafuu na zinatufaa, cha maana zinapojengwa basi zifanye kazi kweli. Jinsi uchumi utovyokua ni kweli vema project kubwa zaidi zikafikiriwa.
Ili tatizo la umeme liishe, TZ itahitaji vichwa safi na sio CHAMA CHA MAGAMBA - wanaojivua gamba kama si wao kila wapatapo msukosuko.
Tom,
Kama hizi 100mw zingekuwa ni miradi ya Tanesco na kwa kumilikiwa na Tanesco, I will second your points kuwa tujenge 100mw station kila mkoa, lakini hizi 100mw ninazozungumzi ani hizi short term goals za kuwalipa wengine.
Ukiangalia what was the cost ya mitambo ya Richmond kuzalisha hizo 100mw, utatapika na utajiuliza kwa nini tulikimbilia ku-subcontract na si kununua hiyo mitambo sisi wenyewe iwe mali yetu?