The 100Megawatt Syndrome

Serikali inaweza kuomba bank guarantee on your behalf kutoka kwenye Development bank kama IFC, EADB, ADB. Billioni 400 ni ndogo sana (vijisenti) kwa serikali ya Tanzania. Serikali imewasaidia kwa kiwango gani kutukwamua katika hilo janga kwasababu wananchi ndio tumemwajiri Rais wa Tanzania na serikali yake na ndio tunaowalipa mishahara yao kwa kutumia kodi zetu?
Samahani mdondoaji hapa nilikuwa namjibu Zomba aliyesema CDM wanaweza pewa bank gurantee, serikali inatoa kwa shirika, hapa nilimjibu kwa vile alidhani CDM or anyone can invest without such capital
 
Samahani mdondoaji hapa nilikuwa namjibu Zomba aliyesema CDM wanaweza pewa bank gurantee, serikali inatoa kwa shirika, hapa nilimjibu kwa vile alidhani CDM or anyone can invest without such capital

Engineer Nsiande,

Baada ya majidiliano haya nasikitika sana kwanini Tanesco mnakubali kubeba lawama zisizo wahusu ni vema mkajivua hizo lawama kwasababu zinaweza kuwapelekea mkageuka kuwa kama ATCL baadae lawama zikawaangukia nyie. Ni vema muamke na moyo wa uzalendo kama mpo kuwaondoa wale walio na moyo wa kifisadi katika shirika.

Pia kwa majibu haya naona it is absolutely pointless kuchangia mada hii wacha makali ya umeme yatafune tu hadi uchumi uporomoke kabisa kwani ushauri unaoangaliwa navyoona ni ule kama nilivyosema mwanzo cash cow proposals. Kwasababu hiyo naona mijadala hii haina maana kuichangia bora niwe mtazamaji tu.
 
Wote tunazungushana tu, mtu pekee ambaye akitaka hata ndani ya siku thelathini kuondoa mgao ni Rais Kikwete. Tatizo ni kuwa hataki kutumia madaraka aliyonayo kuondoa hili tatizo.
kwasababu kuna wanaofaidika na hii power crisis, mgao ukiisha na wao mkwanja utakatika......kwa bahati mbaya ama nzuri JK ni mmojawapo wa wanaofaidika
 
Ndio maana hilo igizo lao wabunge kumpigia kelele Ngeleja ni mojawapo ya upotezaji muda na sauti mkubwa uliowahi kufanyika Bungeni. Hakuna hata mmoja anayeuliza Rais afanye nini? Kuna watu wanasema ati tatizo la umeme ni "janga la taifa" hakuna mtu anawauliza nani kasema kuwa ni "janga la taifa". Kiongozi kusema kuwa ni "janga la taifa" haina maana ni janga la taifa hadi kiongozi mwenye uwezo wa kusema hivyo atakaposema kisheria. So far, nishati siyo janga la kitaifa.
 
Ni kawaida ya binadamu wote kuwa huwa tunafikiri kulingana na uwezo wa akili zetu. Huwezi kumchukua watu wa kawaida kama mimi na wewe ukataka tufikiri kama Albert Einstein.

Miradi inayobuniwa na viongozi walioko madarakani leo ni matokeo ya uwezo wa akili zao. Katika kipindi cha miaka 15 tu baada ya uhuru, kulijengwa miradi ya mikubwa ya umeme huko Pangani, Nyumba ya Mungu, na Kidatu. Miaka mingine mitano iliyofuata pamoja na ugumu wa uchumi wakati huo, bado tulijenga mradi mwingine wa Mtera. Nadhani wakati huo kulikuwa na decision makers waliokuwa na uwezo mkubwa kiakili kulingana na waliopo sasa hivi.
 
Ndio maana hilo igizo lao wabunge kumpigia kelele Ngeleja ni mojawapo ya upotezaji muda na sauti mkubwa uliowahi kufanyika Bungeni. Hakuna hata mmoja anayeuliza Rais afanye nini? Kuna watu wanasema ati tatizo la umeme ni "janga la taifa" hakuna mtu anawauliza nani kasema kuwa ni "janga la taifa". Kiongozi kusema kuwa ni "janga la taifa" haina maana ni janga la taifa hadi kiongozi mwenye uwezo wa kusema hivyo atakaposema kisheria. So far, nishati siyo janga la kitaifa.
Mzee Mwana K, JK anafaidika na ule mgawo wa hela wa kila mwezi wa 15 billion TZSH IPTL inaowakatia government officals.
15 BILLION TZSH per month!! That's serious money, man! Power crisis ikiisha huo mshiko watautoa wapi?
 
vigogo serikalini wanavutiwa na IPTL mshiko wa 15 billion Tshz per month!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Halafu mgao wa umeme ukiisha kabisa akina JK, Kigoda, na vigogo wa magamba watakula wapi?
Magamba haya sijui yataisha lini.
Wajinga ndio tuliwao hadi tunalia na kuzirai...............kama kule Igunga
 
Ndio maana hilo igizo lao wabunge kumpigia kelele Ngeleja ni mojawapo ya upotezaji muda na sauti mkubwa uliowahi kufanyika Bungeni. Hakuna hata mmoja anayeuliza Rais afanye nini? Kuna watu wanasema ati tatizo la umeme ni "janga la taifa" hakuna mtu anawauliza nani kasema kuwa ni "janga la taifa". Kiongozi kusema kuwa ni "janga la taifa" haina maana ni janga la taifa hadi kiongozi mwenye uwezo wa kusema hivyo atakaposema kisheria. So far, nishati siyo janga la kitaifa.
hata JK alisema kumlaumu Ngeleja sio haki (sabasaba)

... but, what next?
 
hata JK alisema kumlaumu Ngeleja sio haki (sabasaba)

... but, what next?

Kuwalaumu Tanesco ama Ngeleja ni kujichumia dhambi za bure. Mwenye final say ya kumaliza mgawo in a matter of minutes ama kuuendeleza ni mtu mmoja tu. JK.
 
situtain ya Tanesco hivi sasa iko hivi.
  • Tanesco Inapata faida au hasara ndogo through mgao. Na ikizalisha at its full capacity kupitia vyanzo vyote Tanesco financially iko hoi. tafakari
Sasa shirika lapofikia linapofikia hali ya kwamba mgao ni best option ya existance yake na faida kiuedeshaji...............

Tuandae jeneza maana huu umeme wa mafungu mafungu hautasaidia............

Kuna mtaalam alisema zile gererator ziko twin tower pale BOT zinaweza kusupply umeme mkoa wa singida na dodoma kwa pamoja. kwa maneno haya unapata ujumbe gani.? think twice ...........

Gharama ya generator zote zilizoko ofisi a wizaa naidara na bunge zingeweza kuwapatia genreator safi kabisa mkoa wa Kigoma..... think thrice

Inaonekana viongozi wengi wao Kwao Tanzania ni Dar. Thanks wana dar wanapatwa na tatizo la mgao wa umeme matatizo ya watanzania yanajulikana.

Hope Pale ikulu kuna generator . Nadhani pia kuna visima vya maji ya chumvi. teh teh teh yes hiyo ni ilala.......

Tanzania 2020 where will we be.
 
Yaani we acha tu Mkuu!!! Huu ni ufisadi wa hali ya juu!! Kwanini tusiwe na power projects yenye uwezo wa kuzalisha hata 1000m au zaidi badala ya hizi projects zenye uwezo mdogo ambazo hazitoshelezi kabisa mahitaji ya nchi yetu. Huu ni usanii na ufisadi wa hali ya juu unaofanywa na Kikwete na Serikali yake.

Unanikumbusha pale ambapo East China juzi tu wamejenga THREE GEORGES project wakidhani ndio mwisho wa mgao wa umeme lakini leo hii wanakosa umeme wakati West China wana umeme hawajui waufanyie nini. Mimi naona Projects za 100MW ni bei nafuu na zinatufaa, cha maana zinapojengwa basi zifanye kazi kweli. Jinsi uchumi utovyokua ni kweli vema project kubwa zaidi zikafikiriwa.

Ili tatizo la umeme liishe, TZ itahitaji vichwa safi na sio CHAMA CHA MAGAMBA - wanaojivua gamba kama si wao kila wapatapo msukosuko.
 
situtain ya Tanesco hivi sasa iko hivi.
  • Tanesco Inapata faida au hasara ndogo through mgao. Na ikizalisha at its full capacity kupitia vyanzo vyote Tanesco financially iko hoi. tafakari
Sasa shirika lapofikia linapofikia hali ya kwamba mgao ni best option ya existance yake na faida kiuedeshaji...............

Tuandae jeneza maana huu umeme wa mafungu mafungu hautasaidia............

Kuna mtaalam alisema zile gererator ziko twin tower pale BOT zinaweza kusupply umeme mkoa wa singida na dodoma kwa pamoja. kwa maneno haya unapata ujumbe gani.? think twice ...........

Gharama ya generator zote zilizoko ofisi a wizaa naidara na bunge zingeweza kuwapatia genreator safi kabisa mkoa wa Kigoma..... think thrice

Inaonekana viongozi wengi wao Kwao Tanzania ni Dar. Thanks wana dar wanapatwa na tatizo la mgao wa umeme matatizo ya watanzania yanajulikana.

Hope Pale ikulu kuna generator . Nadhani pia kuna visima vya maji ya chumvi. teh teh teh yes hiyo ni ilala.......

Tanzania 2020 where will we be.

Ujumbe niupatao kwa mimi ambaye siijui vizuri Singida/Dodoma ni kua: Nikifikiria tu load ya umeme inayohitajika kulisha viyoyozi vya ghorofa zote Twin Towers nzima, naamini kabisa inazidi ile load ya Singida na Dodoma nzima. Hivyo kama SIASA ZETU TULIZOJENGEWA NA CCM zinasema ni lazima VIYOYOZI viwepo TWIN TOWERS basi zile GENERATOR ni halali.
 
The Citizen Correspondents
Mbeya. Cabinet minister Samuel Sitta said yesterday that people who have plunged the country into the current power crisis must bear full responsibility for their actions."It's not enough to apologise to Tanzanians for the suffering they are going through… it must be said that all those who caused this misery must be held responsible," he told a forum organised by CCM members from universities in Mbeya Region.

Mr Sitta, who is also East African Cooperation minister and former National Assembly Speaker, said Tanzania was blessed with abundant resources that could be used to generate power for domestic consumption and export. "It is due to sheer greed that the nation is now in darkness," he said without mentioning names.

huyu mzee ni mpuuzi anafanya mgao wa umeme siasa, kila siku serikali inasema ni matatizo ya kiufundi na kina cha maji mtera ndio maana tuko gizani kumbe yeye anajua ni GREED za jk lakini amekaa kimya anakwenda kuropoka kwenye majukwaa.

kwa kauri kama hivi ni wazi mzao wa umeme ni biashara
 
Dah! hii picha imenishika maana inaelezea reality ya huyu jamaa na fani mnayompigia kelele ni zigo alilomtwisha mwenyekigoda kwa maana kati ya magamba wote ni yeye ndio alionekana mwenye akili kupita wenzake
 
Kujenga mitambo ya kufua umeme zaidi ya matumizi iendane na ukarabati wa miundo mbinu ya kusafirisha umeme,kwani kiasi kikubwa kinapotea njiani, kutokana na uchakavu wa miundo mbinu au ikiwezekana tuanze kujenga smart grid.
Gasi nayozalishwa kwa sasa ni ndogo kutoka kwenye gas processing plant,haitoshi kukidhi mahitaji ya mitambo itayoongezwa na matumizi ya viwanda,hivyo basi inatakiwa kujenga gas processing plant kubwa ili tuweze kufunga mabomba makubwa ya kusafirisha gesi hadi kwenye vinu vya kufua gesi
Geothermal energy is abundant katika Bonde la ufa .Kenya wanatumia nishati hiyo haichafui mazingira na ipo ya kutosha,tulivalie miwani.

Incourage small power generation kwenye sehemu kama vijiji,ili wananchi watokane na hadha ya kukosa umeme.
Power generation kutoka nuklia haitajiki kwa sasa kwanza matumizi yetu hayajafika hata 5000MW,pili safety standard ziko juu sana,kwa nchi yetu ambayo hata kuhifadhi mabomu kwenye ghala ni big issue tuachane nayo.

Mwenyezi Mungu katupa jua linawaka masaa 12 kila siku,mpango makusudi wa kuwezesha kuwavutia wekezaji wa solar power iimarishwe
 
Tanesco is a state owned company, not an independent or private company, which means it can easily secure financial guarantees from Serikali. Tatizo ni kuwa bado viongozi wetu wanaodai hawajui kwa nini Tanzania ni masikini hawajaweza kuoanisha umeme na uzalishaji mali ambao ndio msingi wa mapato.

Chukulia mfano kama umeme ukisambazwa nchi nzima na si mijini pekee, kutaleta msukumo mpya wa uzalishaji mali na huku mashambani, ubora wa mazao na hata uhifadhi utafanyika. Mashambani watu wataweza kufungua viwanda vidogovidogo vya kusindika na kuhifadhi vyakula, nalo litasaidia vipato vyao na kuondokana na mazoea ya kulima mazao ili yauzwe kwa Ushirika an sehemu nyingine. Basically we will be pushing processing industry into rural areas for food and cash crops. Sasa kwa hawa mabingwa wa Kilimo Kwanza, hawaoni kuwa tutajiongezea faida kubwa na ku-retain true value ya mazao badala ya sisi kupewa compensation through pricing or merely 25% of the true value of zao?

Expansion hii ya rural areas, itasababisha nako mijini kuwe na Domino effect, tutalazimika kuwa na ubunifu na kuanza kujituma zaidi ili kuzalisha zaidi.

Lakini nikirudi nyuma kwanza, kuna sekta kadhaa au huduma za jamii ambazo zitanufaika sana kwa umeme kupatikana kila sehemu. Sekta ya elimu, ambapo wanafunzi watakuwa na uwezo wa kupanua uwezo wao kielimu kupitia mitandao (si tunasambaza fibreoptics za SEACOM nchi nzima? je zitatumia kuni?) na vitendea kazi vingine. KUkua na kupanuka kwa wigo wa elimu ni msingi mkuu wa kuleta ushindani na ubunifu katika kila sekta.

Huko majumbani, nako umeme utasaidia kila mtu kwa mengi. Nadharia kuwa umeme ni kitu cha anasa na si cha ulazima ni lazima kifutwe kwa nguvu zote.

Nikirudi kwenye expansion ya umeme nchi nzima, uzalishaji utaongezeka maradufu na kutoa ajira maradufu na kuongeza pato la Taifa maradufu, it is as simple as that.

Now, why is CCM and its government not taking this opportunity to take Tanzania to a next level of development? jibu sina zaidi ya kuwa ni ubinafsi na upeo mfupi.

Hizi 100mw ni short terms projects ambazo miaka hii 25 ambayo tumekuwa tukizitumia, tungekkwisha maliza ujenzi wa project kubwa ya long term na yenye uwezo mkubwa kama Steigler Gorge Ruhidji au wind and solar farms kule Dodoma na Singida.

Time is money and time is not on our side. Serikali na Wananchi ni lazima wang'amue hili na tatizo hili la Umeme si la kisiasa pekee, au chama kimoja bali ni la nchi nzima.

Kamwe hatutaweza kuwa Taifa huru linalojitegemea kama dhana hii potofu hatutaondokana nayo. Na hata tukiweka hizo station nyingine, makosa tuliyoyafanya miaka 25 iliyopita ya kuzembea kufanya maintenance Mtera, Kidatu na power plants nyingine yasirudiwe.

Kama Serikali ina ni a ya kweli kutatua tatizo la umeme, jambo hilo si gumu, kama waliweza kununua VX kwa kila Mbunge na Waziri, kwa nini washindwe kuhakikisha umeme ni wa uhakika?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom