TFF wanatatizo gani jamani kwanini Simba haichezi katikati ya wiki kisa maandalizi?

bulabo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
620
759
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusu ligi yetu. Ukiangalia Chelsea kacheza Jumamosi na Jana iumanne kacheza why Simba tunawekwa ubwete sana.

Niwaambie viongozi wa Simba kama wanaona kukaa tu bila kucheza mechi kisa mashindano ya kimataifa tunashusha viwango vya wachezaji. Mimi ni mwanasimba lakini kwenye hili linafikirisha mno kama akili yako inafanya kazi vizuri. Yanga wamecheza Jumamosi na Jumatano wamecheza why Simba tu.

Wanasimba tusione kama TFF wanatufanyie roho nzuri lakini wanatuuuaaa bila sisi kujijua. Simba inawachezaji wengi wazuri lakini kwa sbb hawapati mechi fitness ndio maana wachezaji siku ya kaizer walikuwa kama wameleweshwa kitu.

Tuna AME hachezi, Athumani hachezi, kennedy hachez, morrison hachez, ndemla hachezi n.k
 
Bro ukiangalia simba ilicheza mechi ya azam federation tarehe 27 April 2021 mpaka inacheza na kaizer zilikuwa siku 18 kavu. Huoni kama ni Tatizo kwa simba yetu
Mimi ni muumini wa tafiti. Ukinithibitishia kwa utafiti kwamba hiyo sababu ndiyo iliyopelekea Simba kufanya vibaya, nitakuunga mkono au taninyamazisha. Mimi naona timu zinacheza mfululizo lakini zinatoa sare tuu, sijui nalo hilo linakaaje
 
Bro ukiangalia simba ilicheza mechi ya azam federation tarehe 27 April 2021 mpaka inacheza na kaizer zilikuwa siku 18 kavu. Huoni kama ni Tatizo kwa simba yetu
Siku 18 kavu na mlikimbia....
Mlipokuwa yanga mnashiriki kimataifa uliwahi hoji hili?
Japo sisapoti team kukaa bila kucheza ila mnahoji kana kwamba kuna mazingira ya upendeleo wakati ni kawaida hapa bongo.
 
Simba wiki iliyopita . Alienda south na kukaa wiki nzima bila sababu..

Dar jo burg ni masaa matatu tu kwa ndege.. ila simba alipangiwa acheze mechi jumamosi , yeye simba akaenda south toka jumatatu asubuh.. na kukaa south wiki nzima kama mtalii vile.. huku mwenzake kaizer anacheza mechi zake za ligi hadi jumatano..

Tazama marudiano tena simba karudi dar na mechi imepangwa jumamosi.. leo jumatano ila bado kaizer hajaja bado .. ila angekuwa simba angeshafika tangu jumatatu ili akae tu hotelini
 
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusu ligi yetu. Ukiangalia Chelsea kacheza Jumamosi na Jana iumanne kacheza why Simba tunawekwa ubwete sana. Niwaambie viongozi wa Simba kama wanaona kukaa tu bila kucheza mechi kisa mashindano ya kimataifa tunashusha viwango vya wachezaji. Mimi ni mwanasimba lakini kwenye hili linafikirisha mno kama akili yako inafanya kazi vizuri. Yanga wamecheza Jumamosi na Jumatano wamecheza why Simba tu...
Vibwengo wa Utopolo mnaacha kushughulikia timu lenu lipate japo nafasi ya pili mnahangaika na Simba, shauri yenu.
 
Utopolo mlikimbia mechi, japo TFF na bodi ya ligi nao ni michosho tu.
 
Viongozi wa Simba ndio wanao omba Tff wakiamini itawasaidia. Hii inaonyesha viongozi pale Simba hawajui lolote kuhusu mpira haiwezekani mchezaji akae mda mrefu bila kucheza alafu acheze mechi ngumu. Ndio maana Mexime alisema hatuna viongozi wa mpira.
 
Ninachokiona,utopolo wanataka Simba icheze kabla ya mechi za champions league ili wapoteze kwani wanajua wachezaji watajilnda dhidi ya kuumizwa kama ulivyo mpango wa utopolo kuhonga timu pinzani na Simba ili waumize wachezaji muhimu wao wapate furaha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom