Ligi yetu inakua ila baadhi ya wachezaji na mashabiki bado Wana fikra za kipuuzi na za kizamani. Ni upuuzi kwenye ligi kuu ya nchi kuwa na wachezaji wanaoamini goli halipatikani sababu ya taulo la kipa au kuna vitu vimefukiwa.Hayo mambo ni ya timu za mtaani. Ajabu zaidi hata zinazojiita timu kubwa za Simba na yanga bado zina wachezaji wanaoamini ushindi unaweza kuzuiwa na taulo la kipa au vitu kufukiwa.
Toeni adhabu Kali sio hivyo vimilioni . Pia toeni adhabu Kwa klabu ambayo shabiki au mchezaji atafanya huo upuuzi.
Kuwa na wachezaji aina hii taifa haliwezi kusonga mbele maana hawawezi kujituma wakiamini ulozi ndio unawakosesha ushindi. Pia mashabiki wanaofanya huo upuuzi ni wale ambao ujinga bado haujawatoka yaani elimu ndogo sasa hao dawa yao ni kuwapeleka tu hata polisi tu walale hata wiki kwa kosa la kuingilia mchezo.