Tff, fa mikoa na nmb mnatupeleka wapi?

Aug 19, 2011
8
0
TFF,FA MIKOA NA NMB MNATUPELEKA WAPI?
Habari zenu ndugu wasomaji. Leo ninamaswali machache na hoja kadhaa ambazo nahitaji majibu toka kwa TFF, FA MIKOA naBenki ya NMB kama wadau wakubwa wa Soka hapanchini.

Naamini kila mtu anakumbuka kozi za Walimuwa Soka zilizokuwa zinafanyika hapa nchini takiribani mikoa yote ya Tanzania nabaadhi ya mikoa ilijirudia mara kadhaa, Na nyingi ziliendeshwa kwa Walimu waSekondari na Shule za msingi ili kuinua vipaji toka mashuleni, hii inatokana naTFF kuangahika kwa muda mrefu kutafuta Wadhamini na hatimaye Benki ya NMBkujitokeza na kudhamini kozi hizi kitu ambacho ni kizuri kinachohitajika katikakukuza Soka letu Tanzania.

Kilichonishtua ni mwaka 2009/2010ilitakiwa kuendeshwa kozi hiyo kwa mikoa 26 ya Tanzania Bara na Benki ya NMBilitoa fedha za kuendesha kozi hiyo pamoja na mipira 30 kila mkoa,koni 18 kilamkoa, jezi jozi moja kwa ajili ya mkufunzi na fedha walipewa TFF ili watume kwakila FA mkoa kwa mikoa yote 26.Lakini cha kushangaza hawa TFF walitumapesa hizi na vifaa hivyo kwa mikoa kama kumi tu ikiwamo Shinyanga, Mwanza,Singida, mikoa ya Kisoka Ilala,Temeke na Kinondoni na pia fedha Tshs 710,000 kwaajili ya posho ya mkufunzi, chakula, malazi na mawasiliano sasa swali je fedhanyingine za mikoa 16 zimekwenda wapi mimi na wewe msomaji wangu hatujui.

FA za mikoa teule ambayo ilipewa fedhahizo pia nao walichakachua kwa mtindo wao na kutoa fedha hizo kwa ufinyo Mfanoni Mkoa wa Shinyanga ambao kozi iliendeshwa januari 26, 2010-Februari 7,210 namkufunzi alikuwa Marehemu Suleiman Gwaje ambaye pia alilalamikia hili, piaulitokea ugomvi na kurushiana maneno kati ya viongozi wa FA mkoa na WajumbeWatendaji kutokana na fedha hizo mpaka baadhi ya wajumbe kutaka kupinduauongozi huliopo madarakani.

Utaratibu ulitakiwa kuwa hivi mkufunziakabidhiwe fedha zake katika mchanganuo ufuatao: - Posho ya siku 16 @ Tshs30,000 jumla 480, 000, Nauli Tshs 230,000 yaani kwenda na kurudi pamoja namawasiliano akiwa katika kituo chake cha kazi. Matokeo yake haya hayakufanyikana mkufunzi alipelekwa katika migahawa ya ajabu yenye bei nafuu na huduma hisiolidhishaili kupiga panga fedha hizo.Wanafunzi waliotakiwa kushiliki kozi hiziwalikuwa ni Walimu na idadi ni 45 kwa kila mkoa yaani katika ile mikoa 10 teuleya TFF.

Kwa mjibu wa TFF wenyewe walisema gharama ya Cheti kimoja ni Tshs10,000 na fedha hizi ulipwa na NMB na tayari zilishakabidhiwa kwa TFF lakinicha kushangaza hakuna hata mkoa moja kati ya mikoa hii 10 walioendesha kozi hiimwaka 2009/2010 wamepata Vyeti hivyo. Sasa piga hesebu mikoa 26, kila mkoaWalimu 45 na kila mmoja gharama ya cheti ndio hiyo je ni Shilingi ngapizimechakachuliwa na hawa jamaa?

Kinachoendelea sasa kuna kampeni ya TFF yachini kwa chini kuhamasisha makatibu wa TAFCA wa ile mikoa ambayo ilibahatika kufanyakozi hii kuwaomba Walimu walioshiriki kozi hii wachange elfu kumi (Tshs 10,000)ili watengenezewe Vyeti hivyo kwa kupitia kwa Katibu wa TAFCA Taifa ili kufichahili lilofanyika ambalo pia limekwama kutokana na kutokuwa na imani tena na TFF,sasa mimi najiuliza Soka letu litakua kwa mtindo huu? TFF, FA MIKOA na Benki yaNMB wanatupeleka wapi?

Pia baadhi ya mikoa kozi hii ilifanyikamwezi Oktoba 2009 kama Singida, Mwanza na mingineyo lakini Shinyanga ilifanyikatarehe 26 Januari, 2010 pia badala ya kuwa na Walimu 45 wa sekondari na shuleza msingi waliotakiwa kushiriki walishiriki 26 tu tena katika mazingira magumukwani hapakuwa na hata maji ya kunywa na washiriki walio wengi walifanya kuwakamatatu barabarani na kuwataka washiriki kozi hii na hili lilifanywa makusudi kwanifedha ya kuendesha kozi hii kwa mkoa huu ilikuwa ishaliwa na viongozi wa FAmkoa.

Na maelezo kutoka TFF, washiriki walitakiwakujigharamia chakula na malazi kitu ambacho walikifanya Walimu hawa tena bilakinyongo. Je ni kweli ndio mkataba unavyosema maana mkataba huu ni siri kati yaTFF na Benki ya NMB hakuna mdau wala TAFCA anayeufahamu mkataba huo sasatujiulize watu wakikataa kujitokeza kushiriki kozi hizi tutamlaumu nani kwaubabahishaji huu?Na kwa nini fedha hizi zisikabidhiwe kwachama cha makocha Taifa na kuwambia waendeshe kozi hizi badala ya FA za kilamkoa kwani wao ndo wanajua watu gani ambao wanapenda na wanataka kuwa walimu wasoka.

Mimi kama mimi siamini kama Benki ya NMBhailifahamu hili kwani kama hawafahamu inaamanahawafanyi ukaguzi wa fedha zao wanazotoa kwa TFF? Na kamawanafahamu wamechukua hatua gani? Na kamawamechukua mbona taarifa hatujaiona wala kuisikia? Kamahawajachukua hatua inamaana na wao pia wanahusika katika hili?Mimi kama mdau wa Soka hili la Bongoinaniuma sanana kubakia na maswali TFF, FA MIKOA na Benki ya NMB wanatupeleka wapi? Na wapokwa ajili ya kuendeleza Soka au maslahi yaobinafsi? TFF Na Benki ya NMB naomba mchunguze au mtoe maelezo kuhusu hili maanalinatia kinyaa na aibu katika Soka letu na kamahamna taarifa basi Habari ndiyo hiyo.


Na MagesaJaphari
E– Mail:japharimagesa@yahoo.com, japharimagesa@gmail.com


NB:Kwaharaka haraka tu, Fedha inayosadikika kutafunwa na TFF na FA MIKOAWatu 45@ mkoa × 10,000 gharama ya cheti × 26 mikoa iliyotakiwa kushiriki jumla 11,700,000.FEDHAya Wakufunzi mikoa 26,ilitolewa kwamikoa 10, je mikoa 16@Tshs 710,000× 16 mikoa ambayo haikutumiwa jumla 11,360,000GRAND TOTAL Tshs 23,060,000Hizindizo tulizojua kwa mjibu wa hesebu iliyopo je tusizozifahamu ni ngapi? AKILIKUMKICHWA!
 
Naomba mtoe maoni yenu na wahusika wapate huu ujumbe kama wataweza wawasiliane na mimi kwa barua pepe hizo katika makala hii.
 
Back
Top Bottom