Tfda wanafanya kazi gani?

kilumbi

Member
Oct 9, 2012
24
4
Leo mchana niliwapigia simu watu wa TFDA na kuwaeleza kuwa kuna maji ya RWENZORI hapa MUSOMA ambayo yamesambaa mjini wakati muda wake wa kutumika umekwisha. Cha ajabu wamenijibu kwamba wao wako mbali hivyo hawawezi kushughulikia suala hilo badala yake nimtafute Bwana Afya wa Manispaa.

Hivi masuala ya Chakula na Dawa si yanapaswa kushughulikiwa na TFDA? Kwa hiyo sisi tulio mbali na Makao makuu ya TFDA tuendelee kula/kutumia vitu vilivyoisha muda wake?

Nadhani sasa kuna haja ya kuweka OFISI za TFDA kwenye kila Makao Makuu ya Mkoa.

View attachment 68326
 
Back
Top Bottom