Malinzi na jamaa zake wamesubiri mkono udondoke washibe tenga anaendelea kutembea hadi wamehamaki. Wababaishaji na makanjanja waliokua likizo sasa wanajiandaa kushughulikia soka la TZ. Shukrani kwa Amos Makala.Endelea na upuuzi wako. Tunasubiri TFF iongozwe na nyinyi vichwa vya panzi baada ya kutengwa na kujitenga na jamii ya soka ulimwenguni. Inawezekanaje Tenga afanye yote hayo huku mnamtazama hadi hali inakuwa hivi?
Wenye akili tunajua kilichonyuma ya pazia. Tenga amefanya vizuri kiasi, sasa angeachia kila kitu ili serikali hii dhaifu iinie mkenge inaoutafuta
Tenga, Tenga mbona karidhia kama unavyotaka sasa endeleeni bila Tenga. Na yeye hagombei po pote povu la nini?Swala la muhimu hapa je TENGA alifuata utaratibu wa kisheria? Kama la kwa nini na kwa manufaa ya nani? Je mbona anaogopa Wajumbe walimchagua hapo awali??
Ndinani issue hapa si Malinzi kwenda TFF kuiba ama vinginevyo, kama ni mwizi mbona hajawahi kushtakiwa mahali popote achilia mbali kutiwa hatiani na kufungwa. Chuki zenu kwa Malinzi zisiwafanye kuwa vipofu hata kwa mambo yaliyo wazi kiasi hiki.
Hapa tunazungumzia TFF kuifuata kikamilifu katiba yao iko wazi sana juu ya utaratibu wa kuifanyia mabadiliko hata mhitimu wa darasa la saba bajua utaratibu huo wa kikatiba wa namna ya kuifanyia marekebisho katiba ya TFF.
Hakuna kifungu kinachoelekeza kurekebisha katiba kwa waraka na hakuna mtu huru anayeweza kuthibitisha kwamba wajumbe waliokubali mabadiliko kwa njia ya waraka wanakidhi idadi(akidi)??
Mtu yeyote anayetetea huu uharamia unaofanywa na TFF ni dhahiri kwamba yeye ndiye anataka kutuibia watanzania kwa kutaka Nyamlani apate mteremko wa kuwa raisi.
Hivi nikiwauliza mnaogopa nini Nyamlani kushindanishwa na watu wengine mtanijibu nini???
Mwita, hakuna kifungu kinachoelekeza wala hakuna kifungu kinachokataza kuwa maamuzi hayawezi kufanywa kwa njia ya RESOLUTION; utaratibu wa namna hiyo hata FIFA wanauafiki ama sivyo TFF wasingeutumia. Kuhusu idadi ya wajumbe walioafiki kubadilishwa kwa katiba kwa mtindo huu, the majority waliafiki na ndio maana ikabadilishwa kama ilivyopendekezwa ama sivyo kama wasingekuwa na majority ya wajumbe walioafiki TFF wasingetekeleza mabadiliko yaliyopendekezwa!
Wakina Malinzi mara nyingi wanatumia pesa kupata uongozi mahala popote wanapousaka; iwe GYMKHANA club hata kule YANGA , kwahivyo kwa wao kutumia pesa kupata uongozi wa aina yeyote ile ni investment ambayo lazima iwe na return na return anayoitaka Jamal kule TFF sio kuendeleza soka bali kwenda kukomba fedha[ $$$$$$] na hilo yeye mwenyewe katika nafsi yake anajua ndicho kinachomsukuma!
Tusifikiri kwa kutumia makamasi JE ANACHOFANYA TENGA NI SAHIHI???
Malinzi hana vigezo kwa mujibu wa katiba ya sasa ya tff ambayo inamtaka kiongozi wa Tff awe amewahi kuwa kiongozi kwenye mambo ya mpira wa miguu kwa angalau miaka 5, malinzi ameshindwa kuthibisha kama amewahi kuongoza kwa kipindi hicho.
Anachofanya makala ni kutetea tumbo lake tu
Toka FIFA ianzishwe tarehe 21/May/1904 hata siku moja haijawahi kubadili katiba yake kwa njia yoyote ile zaidi ya kutumia congress ( kwenye katiba ya TFF inaitwa General Assembly/mkutano mkuu).Mwita, hakuna kifungu kinachoelekeza wala hakuna kifungu kinachokataza kuwa maamuzi hayawezi kufanywa kwa njia ya RESOLUTION; utaratibu wa namna hiyo hata FIFA wanauafiki ama sivyo TFF wasingeutumia. Kuhusu idadi ya wajumbe walioafiki kubadilishwa kwa katiba kwa mtindo huu, the majority waliafiki na ndio maana ikabadilishwa kama ilivyopendekezwa ama sivyo kama wasingekuwa na majority ya wajumbe walioafiki TFF wasingetekeleza mabadiliko yaliyopendekezwa!
Wakina Malinzi mara nyingi wanatumia pesa kupata uongozi mahala popote wanapousaka; iwe GYMKHANA club hata kule YANGA , kwahivyo kwa wao kutumia pesa kupata uongozi wa aina yeyote ile ni investment ambayo lazima iwe na return na return anayoitaka Jamal kule TFF sio kuendeleza soka bali kwenda kukomba fedha[ $$$$$$] na hilo yeye mwenyewe katika nafsi yake anajua ndicho kinachomsukuma!
Alikwenda Ghana kufungua kituo cha michezo ambacho nasi tulipewa pesa sawa za kujenga kituo kama hicho, cha ajabu cha kwetu hakionekani ila anajenga ghorofa kariakoo, kuulizwa anasema sio lake bali la mke wake, tehe tehe tehe tehe dhihaka hizi kaka.Kessy Francis ebu jikumbushe matatizo ya uongozi yaliyokuwapo kabla ya Tenga, kisha umshambulie Tenga Kama ulivyofanya! Kweli watu ni rahisi kusahau!