Tendwa: Tubadili mfumo wa uchaguzi kutetea wabunge wanaofukuzwa uanachama

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
tendwa1(2).jpg

John Tendwa, msajili wa vyama vya siasa nchini

MSAJILI wa Vyama Vya Siasa, John Tendwa amesema kwamba ofisi yake inafikiria kuwezakubadilisha mifumo ya uchaguzi kwa kufikiria nafasi na haki za msingi za mpigakura dhidi ya chama kinapomfukuza uanachama mbunge. Kauli hiyo ilitolewa leo na Tendwa wakati akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dares Salaam mara baada ya kuapishwa kwa viongozi wapya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ambapo alisema suala la kufukunzwa uanachama mbunge si geni lilishatokea hata katika mfumo wa chama kimoja.

Tendwa alitoa kauli hiyo mara baada ya kuulizwa swali la waandishi wa habari kuhusiana na kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid kufukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) hali ilimfanya kupoteza nyadhifa zake. Ambapo Tendwa aliongeza kuwa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi inapotokea hali ya namna hiyo , alihoji kuwa mpigakura anafikiriwaje na chama juu ya sifa na haki za msingi dhidi ya chama.
 
Alijisemea Mtikila MGOMBEA BINAFSI nyie mkakataa, au kwanini tusiwe kama Malawi Mutharika aliukwaa uraisi then akatibuana na Muluzi akaanzisha Chama kingine akiwa Ikulu na hakupoteza his presidency
 
Kosa si la vyama, ila kwa sasa vyama vya siasa ndivyo vinavyoshambuliwa. Ni kitendo kisichoeleweka Hamad kufanya kampeni nje ya utaratibu wa chama hadharani kumpinga kiongozi aliye madarakani. Kwa nini asisubiri wakati unapowadia agombee nafasi hiyo badala ya kufanya kama alivyo fanya?

Kwa vyo vyote maana ya chama ni jumuiya ya watu walijiwekea taratibu za kufuatwa, na anayefanya kinyume cha taratibu hizo ni haki kuwekwa nje ya uringo. Vinginevyo zitungwe sheria za kuwabakiza wabunge hao kutokana na kuchaguliwa na wananchi wengi ingwa bado ukwasi pale wanapogombea kwa kupitia chama cha siasa. Bora kama mtu anajijona hakubaliani na mambo ya chama basi aamue kuwa mgombea binafsi sheria hiyo ikipitishwa.
 
Ataendelea kufikiri hadi atakapo staafu kwani naamini chama cha magamba hakitakubali hiyo sheria, ikipita tu wabunge wengi wa magamba wataunga hoja za CDM bila kuwa na wasiwasi wa kuogopa kutishiwa kufukuzwa chamani.
 
Katiba mpya ndio jawabu

Ukiwaambia hivyo watahakikisha kifungu hicho hakiwepo kwenye katiba mpya kwa vile hiyo ni njia ambayo CCM na sirikali yake wanafikiria ni mahsusi kwa ajili ya kusambaratisha mshikamano wa vyama vya upinzania unaozidi kushika kazi ya ajabu kuimarika na hivyo kuwa tishio lisiloepukika.
 
Back
Top Bottom