Tendwa: Jakaya Kikwete ameteleza kutoa msimamo wa CCM bungeni

Alexandry Nemesi

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,494
568
Dar es Salaam. Aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa amesema Rais Jakaya Kikwete aliteleza kueleza msimamo wake na ambao baadaye ulibainika kuwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati akizindua Bunge Maalumu la Katiba, Machi 21.

Tendwa, ambaye alistaafu Agosti mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na Jaji Francis Mutungi, alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Tendwa, ambaye alikuwa Msajili kwa miaka 13, alisema akiwa kiongozi mkuu, Rais Kikwete alipaswa kutoa mwongozo wa uendeshaji wa Bunge Maalum la Katiba.

"Sikuwapo nchini, lakini kwa kadri ninavyoelezwa, kama hiyo ni kauli yake, basi alijisahau kusemea msimamo wa chama chake, (CCM) na sera yake ya serikali mbili katika bunge hilo," alisema.

"Rais ni mtendaji, alipaswa kutoa guidelines (miongozo) ya jinsi ambavyo Bunge Maalum la Katiba linatakiwa kufanya. Alichokisema, aliteleza.

"Alijisahau na kurudi kwenye chama kwa sababu hiyo ndiyo sera ya chama chake, " alisema Tendwa.

"Na siyo yeye tu (Kikwete) kwani nimemsikia hata Dk Shein (Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi), akisema kuwa msimamo wa CCM ni serikali mbili," aliongeza Tendwa.

"Nimemsikia Makamu wa Pili wa Rais (Balozi Seif Ali Iddi) akisema hivyo na Rais wangu (Kikwete) katika mikutano mbalimbali ya hadhara, naye amelisema hilo."

Madai ya kuibeba CCM

Tendwa ambaye katika uongozi wake wa miaka 13 alikuwa akituhumiwa mara kwa mara na vyama vya upinzani kuwa anakibeba chama tawala, alisema: "Nadhani na yeye (Rais Kikwete) kasema. Nadhani alijisahau kuwa ni kiongozi wa taifa."

"Rais ni mtendaji na mimi nasema aliteleza. Turudi katika hoja kwa kujadili rasimu iliyoko mezani."

Kauli hiyo imekuja kipindi ambacho baadhi ya viongozi wakiwamo wa vyama vya siasa nchini, Dk Wilbroad Slaa (Chadema), Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad na pia aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, pia kumkosoa Rais Kikwete.

Kwa nyakati tofauti, wameeleza kuwa Kikwete ndiye mtu pekee anayeweza kutuliza mvutano ulioibuka katika mchakato huo unaoendelea kwenye Bunge la Katiba.

Ulikoanzia mzozo

Machi 21, wakati akifungua Bunge Maalum la Katiba, Rais Kikwete aliipinga Rasimu ya Pili ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba, akigusia mambo saba ya msingi yaliyomo katika rasimu hiyo na kutaka yatazamwe kwa kina, kubainisha kuwa mengine hayawezi kutekelezeka.

Miongoni mwa mambo hayo ni muundo wa Muungano kuwa wa serikali tatu uliopendekezwa katika rasimu hiyo.

Kikwete, ambaye alisema anatoa maoni yake binafsi, alipinga waziwazi pendekezo la serikali tatu na kuegemea katika muundo wa serikali mbili unaoungwa mkono na CCM, huku akifafanua kuwa idadi ya watu waliopendekeza muundo wa serikali tatu ilikuwa ndogo.

Walilosema wengine

Julai 7, wakati akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na televisheni ya ITV, Maalim Seif alimtupia lawama Rais Kikwete kuwa amechangia kuukoroga mchakato wa katiba kwa kufuata msimamo wa chama chake, badala ya maoni ya wananchi yaliyomo katika rasimu ya pili ya katiba.

Maalim Seif, ambaye alilenga kauli iliyotolewa na kiongozi huyo wa nchi wakati akifungua Bunge la Katiba, alisema kauli ya Rais Kikwete imeondoa imani ya wananchi kuhusu kupatikana kwa katiba inayotokana na maoni yao.

Alisema mchakato huo hivi sasa unamtegemea Rais pekee, huku akisisitiza kuwa hakuna binadamu aliyekamilika na kumshauri kutafuta uwezekano wa kuweka mambo sawa, ili kujenga tena imani kwa wadau wote.

Julai 4, Dk Slaa, wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jijini Dar es Salaam, alimtaka Rais Kikwete kujitokeza hadharani kutafuta suluhu ya kupata mwafaka wa mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa hakuna mamlaka nyingine zaidi inayoweza kuunusuru.

Naye Jaji Warioba kwa nyakati tofauti amemshauri Rais Kikwete kuchukua hatua zitakazoondoa matatizo katika Bunge la Katiba ili kuwezesha mchakato huo kukamilika.

Alisema ni muhimu kiongozi huyo mkuu wa nchi kuweka kando tofauti za mawazo na mitazamo ili kupata Katiba Mpya kwa masilahi ya Taifa.

Mwanzoni mwa wiki, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na naibu waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi alifichua kuwa msimamo wa serikali mbili unaoonyeshwa na wabunge wa chama hicho ni maagizo ya Kikwete.

Awashauri Ukawa

Kuhusu Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Tendwa aliwashauri wajumbe wote wanaounda umoja huo kurejea bungeni ili kujadili vipengele vinavyogusa maslahi ya wananchi na kuweka kando sura ya kwanza na sita zinazohusu muundo wa Serikali.

Aliwataka wajumbe wanaounda Ukawa kuacha kususia vikao na kutoka kwenye Bunge la Katiba kama walivyofanya tangu Aprili 16 na kusema kuwa busara zaidi ndizo zinazotakiwa kutumika kupitia majadiliano kwa lengo la kumaliza mgogoro uliopo na kuwezesha mchakato kuendelea.

Alisema rasimu siyo katiba bali ni andiko linaloweza kubadilishwa na kuvunjwa vunjwa, hivyo wajumbe wa Ukawa warudi bungeni na kuandaa rasimu ya katiba itakayokwenda kupigiwa kura na wananchi.

"Unatoka nje na unasema hurudi, wewe ni nani? Kunahitajika hapa uvumilifu wa kisiasa. Watu hawa (Ukawa) na wengine wanatakiwa kuaminiana katika mchakato huu. Warudi bungeni wajadili vifungu vya katiba vinavyowagusa wananchi.

"Wasijadili pekee muundo wa Muungano, wajadili vifungu vinavyohusu wananchi, kisha iandikwe rasimu itolewe kwa wananchi kwa muda mwafaka na wao waende huko wawaelimishe ili wafanye uamuzi sahihi.

"Hoja ya msingi iwe upigaji kura uwe wa serikali mbili au tatu kwa kuwa vifungu vingine vimekwishaafikiwa," alisema Tendwa.

Aliongeza kuwa inashangaza kuona tangu wajumbe hao watoke bungeni ofisi ya msajili wa vyama vya siasa haikutakiwa kuendelea kukaa kimya kuhusu Ukawa wanaojitangaza kinyume cha kanuni na sheria.

"Ofisi hiyo (ya msajili) imekuwa kimya, haisemi lolote kuhusu Ukawa. Hawana uhalali wa kisheria na mamlaka. Kwa hiyo msiwakuze bure bila sababu ya msingi kwani hatujui wameanzia wapi, mizizi yao ipo wapi," alisema.

Kuhusu lugha inayotumiwa na wajumbe kwenye Bunge la Katiba, Tendwa alisema ni ya mitaaani na wakati mwingine watoto hutumia lugha nzuri kuliko ya wabunge hao.

"Lugha ya matusi kuingizwa bungeni ni aibu. Hata watoto hawafanyi hivyo, lakini wabunge tunaowategemea kabisa ndio wamekuwa wakitumia maneno ya kibabe na kejeli. Wanatakiwa kujifunza kuwa wanapoingia bungeni lazima lugha za mitaani waziache nje," alisema.

Bunge la Katiba linatarajiwa kuendelea tena Agosti 5, huku kukiwa na wasiwasi kama wajumbe wa Ukawa watarejea au la baada ya kususia vikao hivyo.

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta tayari ameitisha kikao cha Kamati ya Mashauriano chenye wajumbe 27 kitakachofanyika jijini Dara es Salaam Julai 24 kwa lengo la kuinusuru katiba hiyo na kuwashawishi Ukawa kurejea bungeni.

Wakati akistaafu, Tendwa alisema anajivunia kuifanya ofisi ya Msajili iwe ya kisasa, akisema aliteuliwa bila ya kupewa adidu za rejea na alitegemea kuwa ofisi hiyo ingekuwa na wanasheria, lakini alijikuta mtu pekee mwenye taaluma hiyo.

Chanzo: Mwananchi

My take-Kauli ya Tendwa ni dhihirisho na mtazamo wa tuliowengi ambao kwa namna moja ama nyingine tulishangazwa na hatua ya Amiri Jeshi mkuu badala ya kutimiza wajibu wa kuzindua BMLK alijikita katika kuelezea msimamo wake na wa chama chake huku akitambua yeye ni mkuu wa Nchi haya Nchi.Matokeo ya kauli zake ndio chanzo cha uchakachuaji wa msingi wa Rasimu ndani ya BMLK.
 
Kuteleza si jambo la ajabu kwa mwanadamu yeyote yule kwani tumeumbwa na Mwenyezi Mungu na mapungufu mengi - hoja je anajua kwamba aliteleza?

Way Forward: Aombe radhi kwa wajumbe wote wa Bunge hilo hasa UKAWA, atoe msimamo wake kwamba tunajadili Rasimu iliyowakilishwa na Tume ya Jaji Warioba si vinginevyo. Baada ya haya nafikiri UKAWA watakuwa wa kwanza kuingia Bungeni tarehe ya vikao ikishafika.
 
Huo ndio ukweli, kumbe mtu akiwa nje ya system akili huwa inarejea kichwani ee! Sikutegemea kama Tendwa angeweza kutoa hoja yenye mashiko kama hii. Alipokuwa kwenye kile kiti chake asinge thubutu kupayuka haya anayo yasema sasa. Funguka mzee wangu ili hata ukifa uende na amani ya bwana.
 
Ukiwa kwenye system akili unakabidhi system.
 
Aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa nchini,John Tendwa amesema Rais Jakaya Kikwete aliteleza kueleza msimamo wake na ambao baadaye ulibainika kuwa wa chama cha mapinduzi (CCM) Wakati akizindua Bunge maalum la katiba,March 21.

My take-Kauli ya Tendwa ni dhihirisho na mtazamo wa tuliowengi ambao kwa namna moja ama nyingine tulishangazwa na hatua ya Amiri Jeshi mkuu badala ya kutimiza wajibu wa kuzindua BMLK alijikita katika kuelezea msimamo wake na wa chama chake huku akitambua yeye ni mkuu wa Nchi haya Nchi.Matokeo ya kauli zake ndio chanzo cha uchakachuaji wa msingi wa Rasimu ndani ya BMLK.

Source-Mwananchi toleo la leo.
Poleni kama wengi wenu bado mnaamini Kikwete ni rais kweli,Yule yupo ikulu kama mfano wa rais tu wala hana madaraka yoyote kule,Wenye madaraka ya kweli wamejificha wanaiendesha nchi kwa rimoti kontro.
 
Tendwa katoa yaliyo moyoni mwake lakini mkuu wa nchi alilishwa maneno hayakutoka moyoni mwake na matokeo yake ndio tanayoyaona sasa. Hii nchi ni yetu sote na lengo la Rasimu ya Katiba ni kwa manufaa ya wote sio CCM!
 
(Tendwa) alisema " ... akiwa kiongozi Mkuu, Rais Kikwete alipaswa kutoa mwongozo wa uendeshaji wa Bunge Maalum la Katiba .... Sikuwapo nchini lakini kwa kadiri ninavyoelezwa, kama hii ni kauli yake, basi alijisahau kusemea msimamo wa chama chake (CCM) na sera yake ya serikali mbili katika Bunge hilo", alisema.
 
Kuteleza si jambo la ajabu kwa mwanadamu yeyote yule kwani tumeumbwa na Mwenyezi Mungu na mapungufu mengi - hoja je anajua kwamba aliteleza?

Way Forward: Aombe radhi kwa wajumbe wote wa Bunge hilo hasa UKAWA, atoe msimamo wake kwamba tunajadili Rasimu iliyowakilishwa na Tume ya Jaji Warioba si vinginevyo. Baada ya haya nafikiri UKAWA watakuwa wa kwanza kuingia Bungeni tarehe ya vikao ikishafika.
Hapo nyekundu ni ngumu kama vile ilivyo ngumu kufunga injini ya Toyo kwenye FUSO
 
Tendwa katoa yaliyo moyoni mwake lakini mkuu wa nchi alilishwa maneno hayakutoka moyoni mwake na matokeo yake ndio tanayoyaona sasa. Hii nchi ni yetu sote na lengo la Rasimu ya Katiba ni kwa manufaa ya wote sio CCM!
Alilishawa na Mwalimu au division zero form Six? akili za kuambiwa inamaana hachanganyi na za kwake? Acheni utani na mheshimiwa nyie vijana!!!!! Atawa----------- soon hapa.
 
Huo ndio ukweli, kumbe mtu akiwa nje ya system akili huwa inarejea kichwani ee! Sikutegemea kama Tendwa angeweza kutoa hoja yenye mashiko kama hii. Alipokuwa kwenye kile kiti chake asinge thubutu kupayuka haya anayo yasema sasa. Funguka mzee wangu ili hata ukifa uende na amani ya bwana.
Tatizo la hiko chama ni ukosefu wa uhuru. Akiwa pale analindwa kwa kila kauli atayoitoa na ole wake iwe tofaut na bos wake. We huoni kina nyoka wa chuma wanavyoandamwa?
 
Tendwa katoa yaliyo moyoni mwake lakini mkuu wa nchi alilishwa maneno hayakutoka moyoni mwake na matokeo yake ndio tanayoyaona sasa. Hii nchi ni yetu sote na lengo la Rasimu ya Katiba ni kwa manufaa ya wote sio CCM!

Mkuu inawezekana Tendwa ndiye aliyeteleza. Na inawezekana kuwa baada ya kuondoka labda amesahau game inavyochezwa. Tatizo ambalo linatusumbua wengi ni kuwa hatutaki kukubali ukweli au hali halisi kwamba CCM hawataki katiba ambayo itatandika njia ya kufa kwake. Kikwete pamoja na kuwa ni rais wa nchi tunasahau kuwa yeye ni mwenyekiti wa CCM. Tunatakiwa pia tutambue kuwa, kwa sasa maslahi ya CCM yako juu ya maslahi ya wananchi, Tanzania, Tanganyika au hata Zanzibar. Kwa hiyo kama katiba italinda kwanza maslahi ya CCM, vipengele vinavyohusu maslahi ya Tanzania vinaweza kupitishwa kwa ulaini sana.

Kwa mwana CCM yoyote mwenye akili timamu anajua kabisa kuwa muundo wa serikali tatu ni msingi wa kifo cha CCM.

Hadi maslahi ya Tanzania yatakapokuwa mbele, all what is happening now in regard to katiba ni mradi wa CCM, ukawa ni wasindikizaji tu.
 
Kuteleza si jambo la ajabu kwa mwanadamu yeyote yule kwani tumeumbwa na Mwenyezi Mungu na mapungufu mengi - hoja je anajua kwamba aliteleza?

Way Forward: Aombe radhi kwa wajumbe wote wa Bunge hilo hasa UKAWA, atoe msimamo wake kwamba tunajadili Rasimu iliyowakilishwa na Tume ya Jaji Warioba si vinginevyo. Baada ya haya nafikiri UKAWA watakuwa wa kwanza kuingia Bungeni tarehe ya vikao ikishafika.

Perfectly! Na ndicho nilitegemea wanaojiita viongozi wa dini na wadau wengine wangefanya. Wangewashauri pia wajumbe wa CCM kuacha kujadili "rasimu yao" na badala yake wajikite kwenye rasimu halali kama ilivyowasilishwa na Tume ya Warioba. Pia Mwenyekiti wa BMK na wasaidizi wake wakemewe kwa upendeleo wa waziwazi.

Kuna mdau mmoja alinivunja mbavu humu jamvini jana kwamba Wajumbe wa UKAWA wametoka nje ya Bunge ilhali wale wa CCM wametoka nje ya mjadala; yupi nafuu?
 
Hawa CCM wakiwa ndani ya Serikali hawaoni ubovu wa serikali yao ila wakitoka wanajifanya ndio wakosoaji wakubwa.

Huyu Tendwa ile ofisi ya Msajili alikua anaitumia kama tawi la ccm, leo anapata wapi ujasiri wa kukosoa sehemu ya uozo wake.
 
Aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa nchini,John Tendwa amesema Rais Jakaya Kikwete aliteleza kueleza msimamo wake na ambao baadaye ulibainika kuwa wa chama cha mapinduzi (CCM) Wakati akizindua Bunge maalum la katiba,March 21.

My take-Kauli ya Tendwa ni dhihirisho na mtazamo wa tuliowengi ambao kwa namna moja ama nyingine tulishangazwa na hatua ya Amiri Jeshi mkuu badala ya kutimiza wajibu wa kuzindua BMLK alijikita katika kuelezea msimamo wake na wa chama chake huku akitambua yeye ni mkuu wa Nchi haya Nchi.Matokeo ya kauli zake ndio chanzo cha uchakachuaji wa msingi wa Rasimu ndani ya BMLK.

Source-Mwananchi toleo la leo.

JK siyo tu ameteleza bali ameanguka kabisa hivyo kupoteza sifa ya kuwa Rais na amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama!

Kwa wenzetu ambao demokrasia imekomaa alitakiwa KUJIUZULU AU KULAZIMISHWA KUJIUZULU NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UCHOCHEZI!
 
Aliyekuwa msajili wa vyama vya siasa nchini,John Tendwa amesema Rais Jakaya Kikwete aliteleza kueleza msimamo wake na ambao baadaye ulibainika kuwa wa chama cha mapinduzi (CCM) Wakati akizindua Bunge maalum la katiba,March 21.

My take-Kauli ya Tendwa ni dhihirisho na mtazamo wa tuliowengi ambao kwa namna moja ama nyingine tulishangazwa na hatua ya Amiri Jeshi mkuu badala ya kutimiza wajibu wa kuzindua BMLK alijikita katika kuelezea msimamo wake na wa chama chake huku akitambua yeye ni mkuu wa Nchi haya Nchi.Matokeo ya kauli zake ndio chanzo cha uchakachuaji wa msingi wa Rasimu ndani ya BMLK.

Source-Mwananchi toleo la leo.
Hakuteleza! Alikusudia baada ya kuchanganyikiwa na mapendekezo ya rasimu ya katiba kinyume na matarajio yake. Yeye alidhani kwakuwa wengi wa wajumbe ni CCM na walikuwa viongozi, wangeleta maoni ya kiCCM badala ya maoni ya wananchi. Kwakuwa yalishakuwa hadharani akawa hana namna ila kutumia hila ile ya kuiponda rasimu ile wakati wa bunge la katiba na ndio maana wakamtanguliza warioba kwani ange anza yeye kama utaratibu ualivyotakiwa Warioba angepangua hoja zake na kumwaibisha. Hakuna cha kuteleza pale!
 
hivi mtu na akili zako timamu unamsikiliza tendwa? zile pesa alizolipwa zimeshaisha inawezekana sasa anataka apewe teuzi ya tume na kamisheni mbalimbali.

mkuu nasoma sana mabandiko yako na naikubali ila hapa umechemka jadili alichosema sio yeye
 
Back
Top Bottom