Elections 2010 TEMCO 'yapigwa chini' kuangalia uchaguzi 2010

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
302
Viongozi wa vyama vya siasa wamepinga vikali Kamati ya Kuangalia Uchaguzi Tanzania (Temco) kuruhusiwa kuwa mwangalizi wa ndani wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 31 na kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuiondoa kwenye orodha, kwa kile walichodai hawana imani na chombo hicho.

Wamesema hawana imani na watendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya Temco, kwa madai kuwa wanaonekana kuwa mashabiki wa chama tawala.

“Mratibu wa Temco, Dk. Benson Banna, yumo ndani ya Redet sasa kweli hapa haki itatendeka, hata kama wataona matokeo halisi hawawezi kusema ukweli wa mambo … tunajua ndani ya Temco kuna mashabiki wa CCM,” walisema

Wakurugenzi wa Temco ndio wamo pia kwenye Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) na kwamba walishatoa utafiti kuonesha wagombea urais, ubunge na udiwani wa CCM ndio wanaoongoza na hivyo inawapa shaka kama Temco inaweza kusema uhalisia wa hali ya uchaguzi ulivyokwenda.
 
Viongozi wa vyama vya siasa wamepinga vikali Kamati ya Kuangalia Uchaguzi Tanzania (Temco) kuruhusiwa kuwa mwangalizi wa ndani wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 31 na kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuiondoa kwenye orodha, kwa kile walichodai hawana imani na chombo hicho.

Wamesema hawana imani na watendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya Temco, kwa madai kuwa wanaonekana kuwa mashabiki wa chama tawala.

"Mratibu wa Temco, Dk. Benson Banna, yumo ndani ya Redet sasa kweli hapa haki itatendeka, hata kama wataona matokeo halisi hawawezi kusema ukweli wa mambo … tunajua ndani ya Temco kuna mashabiki wa CCM," walisema

Wakurugenzi wa Temco ndio wamo pia kwenye Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) na kwamba walishatoa utafiti kuonesha wagombea urais, ubunge na udiwani wa CCM ndio wanaoongoza na hivyo inawapa shaka kama Temco inaweza kusema uhalisia wa hali ya uchaguzi ulivyokwenda.

Toka lini ukamkabidhi nyani akulindie shamba la mahindi!? Kama hutavuna mabua!!
Tunasema mwaka huu ni wetu na Dr. Slaa ndie Rais wetu
 
Aaaah kumbe TEMCO ndio hao eeeh!
Nimewaona ktk picha nyingi za mikutano ya JK wakiwa mbele wamevalia kapelo (baseball cap) nyeupe zenye maandishi hayo..sasa napata kuelewa zaidi kinachoendelea.
 
Aaaahhh Benson Bana... ananikumbusha Yusuph Bana wa Yanga, kwa kurusha mipira ya magoli

Tatizo la Bana ni kuongopa sana asije akafeli tena kiasi kwamba anakua kibaraka kwa kila mwenye nafasi kama ya JK... Tusubiri jinsi TEMKO?REDET/CCM watakavyorespond
 
"Mratibu wa Temco, Dk. Benson Banna, yumo ndani ya Redet sasa kweli hapa haki itatendeka, hata kama wataona matokeo halisi hawawezi kusema ukweli wa mambo … tunajua ndani ya Temco kuna mashabiki wa CCM," walisema

Hivi REDET bado wanataka kuchakachua hata kura zetu jamani hata aibu hawana?
 
Back
Top Bottom