SoC04 Teknolojia ya vitambuzi mwendo kutatua changamoto za uvamizi wa Wanyamapori katika makazi pembezoni mwa Hifadhi za Taifa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jerry Farms

Member
Jul 18, 2022
63
43
Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na hifadhi nyingi za taifa, hifadhi hizi zikiwa chini ya mgawanyiko wa: Hifadhi za taifa, hifadhi teule,hifadhi za mawindo na mapori ya akiba.

Ramani ya hifadhi za Taifa Tanzania

IMG_20240503_143256.jpg

Picha toka mtandaoni Wikipedia

Mfano wa hifadhi hizi ni Serengeti, Mikumi, Saadani, Ngorongoro nakadharika.

Ili kuleta uwiano wa ki ikolojia pembezoni mwa hifadhi hizi kuna jamii ziishizo na kuendesha maisha yao ya kila siku mfano wa jamii hizi ni Wamasai na Wahadzabe.

Hifadhi za taifa zina manufaa mengi kupitia utalii na uhifadhi wa mazingira.

Kufuatia mabadiliko ya tabia nchi na shughuli za binadamu kando ya hifadhi hizi, kumeibuka changamoto ya muingiliano wa wanyama na binadamu. Kufuatia muingiliano huu kumejitokeza changamoto kuu mbili:
•Uharibifu wa mazingira na ikolojia.
•Uvamizi wa wanyamapori kwa jamii za wakazi pembezoni mwa hifadhi. Andiko hili litajikita kuangazia changamoto ya pili na njia za utatuzi.

Changamoto ya uvamizi wa wanyamapori katika makazi ya watu pembezoni mwa hifadhi ni suala sugu na mtambuka. Visa mbalimbali vimekua vikiripotiwa vya uvamizi wa wanyamapori, uharibifu wa mali za wakazi kando ya hifadhi,vifo na hata ulemavu.Mfano mnamo mwaka 2018-2020 katika maeneo ya wilaya ya Mwanga na Same ekari 5873 za mashamba ziliharibiwa na tembo huku kukiripotiwa vifo 98 vya mifugo.

Kwa mkoa wa Ruvuma maeneo ya Tunduru na Namtumbo yaliripoti uvamizi wa tembo toka Hifadhi ya Mwalimu Nyerere katika vijiji sita,( Gazeti la mwananchi 21 May,2021). Katika mikoa ya Kanda ya ziwa watu 63 waliuwawa huku 53 wakijeruhiwa kwa kipindi cha mwezi Julai 2021 hadi Juni 2023.

Kwa mujibu wa tafiti toka mamlaka za kusimamia hifadhi, matukio ya uvamizi wa wanyapori katika jamii ziishizo pembezoni mwa hifadhi yamechagizwa na; uwepo wa wanyama wengi kuliko malisho(sio sana), binadamu kuvamia maeneo hifadhi, uharibifu wa ekolojia(vyanzo vya maji na chakula) na shughuli za binadamu kando ya hifadhi kuvutia wanyama mfano kilimo cha mazao pembezoni mwa hifadhi.

Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (Tanapa), Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori(Tawiri) na Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania(Tanapa) imekua ikichukua hatua mbali mbali kukabiliana na changamoto hii. Baadhi ya hatua hizo ni; utoaji mafunzo ya kukabiliana na wanyama, kutoa vifaa vya kutolea taarifa juu ya uvamizi wa wanyama na utoaji wa fidia.

Pamoja na juhudi hizi changamoto ya uvamizi wa wanyamapori bado ipo hivyo matumizi ya Teknolojia( vitambuzi mwendo) hayana budi kuingia ili kusaidia katika utatuzi wa changamoto hii. Ili kufanikisha hili yafuatayo hayana budi kufanyika ili kupunguza na kuepuka athari ziletazwo na uvamizi wa wanyamapori.

•Kutenganisha maeneo ya hifadhi na makazi. Japokua mipaka ipo kati ya hifadhi na makazi, mamlaka za usimamizi zinatakiwa kuja na mpaka ndani ya mpaka wa hifadhi, mpaka huu tuuite mpaka wa "kidigitali". Huu ni mpaka ambao utafungwa vifaa maalumu vya utambuzi wa mienendo ya wanyama pembezoni mwa hifadhi.​
Mpaka wa "kidigitali".
Hili ni eneo tegwa ndani ya hifadhi ya wanyama, eneo hili litakua na upana wa mita 30 likiambaa usawa wa mpaka mkuu wa hifadhi. Ni mpaka ndani ya mpaka wa hifadhi.
Eneo lote la mpaka huu litafungwa vitambuzi mwendo ambavyo vitakua na kazi ya kuangalia mwenendo wa shughuli zote za wanyama ndani ya hifadhi. Punde wanyama watakapo ingia ndani ya mpaka huu, taarifa zitatumwa kwenda katika kituo cha ufatiliaji cha wahifadhi.
Picha ya mchoro wa mpaka wa kidigitali.
IMG_20240509_080949.jpg

Mchoro binafsi

Vitambuzi mwendo na ufanyaji wake wa kazi
Hivi ni vifaa vya kielektroniki ambavyo vina teknolojia ya kisasa ya utambuzi wa mijongea ya viumbe. Kupitia miale ya lenzi maalumu zitolewazo na vifaa hivi punde wanyama watakapo ingia ndani ya eneo lililofungwa vifaa taarifa inakusanywa, inachakatwa na kutumwa. Wahifadhi watafunga mfumo maalumu ambao utaviwezesha vifaa hivi kutambua uwepo wa makundi ya wanyama, mfumo wa utambuzi unaweza kuwa wa kuanzia mnyama mmoja ama kundi la wanyama 5 nakuendelea. Vifaa hivi ndani ya mpaka wa kidigitali, vitakua na kazi ya kutambua uwepo wa wanyama ndani ya mita 30 za mpaka. Punde vitakapo daka taarifa hizi zitatumwa moja kwa moja kwenda katika kituo kikuu cha ukusanyaji wa taarifa cha wahifadhi na hatua kuchukulia haraka.
Zingatio
Maboresho ya mfumo yafanywe mara kwa mara kulingana na mahitaji ya wakati.
Picha ufanyaji kazi wa vitambuzi mwendo
IMG_20240503_151404.jpg
Picha toka mtandaoni, Google.
"Sensor"-Kitambuzi mwendo.
"Fresnel lens"-Lenzi tambuzi za mijongeo ya wanyama.
"Detecting area"-eneo la utambuzi( mpaka wa kidigitali)

Kituo cha kupokea taarifa ya mienendo ya wanyama mpakani mwa hifadhi.
Kituo hiki kupitia vifaa vilivyo fungwa katika mpaka wetu wa "kidigitali" kitapokea taarifa moja kwa moja juu ya uingiaji wa wanyama katika mpaka tengwa hivyo kabla ya wanyama hawajamaliza kuuvuka mpaka mkubwa wa hifadhi na kuenda katika makazi, timu ya wahifadhi itafika eneo husika kwa haraka na kuchukua hatua za kuwadhibiti wanyama hawa.

Kupitia mfumo huu wa taarifa kupelekwa kwa haraka serikali itaepuka utoaji wa fidia na jamii itaepushwa na mathara ambayo yangetokea baada ya wanyama kuingia katika makazi yao.

Faida za mpaka wa "kidigitali"
•Utambuzi wa haraka wa wanyamapori pindi watakapoingia katika mpaka tengwa la mpaka hivyo kudhibitiwa kwa urahisi.
•Mfumo utarahisisha utambuzi uvamizi wa binadamu kuingia ndani ya hifadhi.
•Kupunguza gharama ambazo zingeingiwa na mamlaka za usimamizi wa hifadhi kwa kuzungukia hifadhi kufanya doria. Doria sasa itafanywa na teknolojia kutambua vyote! Yaani uingiaji wa binadamu hifadhini na uvukaji wa wanyama kwenda kwenye makazi pembezoni mwa hifadhi.
•Kuepuka athari za uvamizi wa wanyama pori na hivyo kuipunguzia gharama serikali katika utoaji wa fidia. Gharama ya vifo, uharibifu wa mali na nyinginezo zitaepukwa katika jamii.
•Mfumo wa huu wa ulinzi ni rafiki wa mazingira, vifaa ndani ya mpaka wa hifadhi hauna madhara kwa wanyama na ekolojia.
Changamoto zinazoweza kujitokeza katika matumizi ya teknolojia hii.
• Udukuzi wa mfumo na uharibifu wa miundombinu toka kwa watu wenye hila za kufanya shughuli haramu hifadhini.
•Gharama katika ununuzi na ufungaji wa vifaa vya kielectroniki.
•Uharibifu wa vifaa.

Jinsi ya kukabiliana na changamoto hizi.
•Doria za mara moja moja za wahifadhi kukagua vifaa na usalama wa mpaka wa kidigitali uliowekwa.
•Ushirikishwaji wa wanajamii katika kutoa taarifa juu ya hujuma zozote zinazopangwa/ zilizotekelezwa kwenye mfumo wa ulinzi.
•Serikali kupitia wizara ya Maliasili kupanga bajeti wezeshi kugharamia vifaa, elimu ya matumizi ya vifaa na ukarabati wa vifaa katika hifadhi. Kupitia fungu tengwa changamoto ya uhaba wa fedha na gharama zinginezo zitatatuliwa.
•Elimu ya uhifadhi na uzalendo kwa wanajamii.
Uhifadhi na mahusiano mema na jamii jirani na hifadhi ndio msingi wa mafanikio wa uhifadhi. Jitihada mbalimbali hazina budi kuchukuliwa ili kujenga mahusiano mema baina ya wanyamapori, wahifadhi na jamii ziishizo pembezoni mwa hifadhi.

Angalizo: Shughuli za kibinadamu haziruhusiwi ndani ya hifadhi ila nnje ya hifadhi hivyo hakuna budi jitihada kufanyika kutengeneza mahusiano mema. Mipaka ya hifadhi iheshimiwe na mahitaji ya jamii kuzunguka hifadhi yazingatiwe.
 
•Kituo cha kupokea taarifa ya mienendo ya wanyama mpakani mwa hifadhi.
Kituo hiki kupitia vifaa vilivyo fungwa katika mpaka wetu wa "kidigitali" kitapokea taarifa moja kwa moja juu ya uingiaji wa wanyama katika mpaka tengwa hivyo kabla ya wanyama hawajamaliza kuuvuka mpaka mkubwa wa hifadhi na kuenda katika makazi, timu ya wahifadhi itafika eneo husika kwa haraka na kuchukua hatua za kuwadhibiti wanyama hawa
Tahadhari kabla ya hatari.

Una maana wanakuwa wameanza kwenda nje, ila kabla hawajatoka ile nje nje yenyewee wameshajulikana🤔. Kama mtoto katoka kibarazani ila bado hajavuka geti👏.

Hii teknolojia nilianza kuisikia kwenye ranchi za mifugo kwa ng'ombe. Je inawezekana kwa wanyamapori?. Na kuna hawa watu wa australia wao wameweka hadi kama vispika mnyama akisogea eneo halitakiwi kinatoa sauti asiyoipenda basi anarudi ranchi (Geofencing) Ikiwa adapted na kwa teknolojia ya sasa ya AI basi mapori yataendeshwa kisasa zaidi bila muingiliano usio wa lazima wa watu.

Mipaka ya hifadhi iheshimiwe na mahitaji ya jamii kuzunguka hifadhi yazingatiwe.
Both teams to score, win win✔
 
Tahadhari kabla ya hatari.

Una maana wanakuwa wameanza kwenda nje, ila kabla hawajatoka ile nje nje yenyewee wameshajulikana🤔. Kama mtoto katoka kibarazani ila bado hajavuka geti👏.

Hii teknolojia nilianza kuisikia kwenye ranchi za mifugo kwa ng'ombe. Je inawezekana kwa wanyamapori?. Na kuna hawa watu wa australia wao wameweka hadi kama vispika mnyama akisogea eneo halitakiwi kinatoa sauti asiyoipenda basi anarudi ranchi (Geofencing) Ikiwa adapted na kwa teknolojia ya sasa ya AI basi mapori yataendeshwa kisasa zaidi bila muingiliano usio wa lazima wa watu.


Both teams to score, win win✔
Naam! Tahadhari kabla ya hatari, nimeipenda hio both team to score....👊👊
 
Back
Top Bottom