Kama taifa tufanyeje kudhibiti hii vita ya kimyakimya inayoendelea kwenye hifadhi za taifa kati ya wananchi, majangili na askari wanyamapori?

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
709
1,773
Sijui ni bahati mbaya au nzuri ni kuwa kuna habari nyingi za kutisha sana zinatokea huko kwenye hifadhi za taifa kati ya wananchi na askari ila hazifiki kwenye vyombo vya habari. Tukiachilia mbali mauaji pia wanaokamatwa hifadhini hupewa kipigo kitakatifu kabla ya kufikishwa mahakamani. Yaani ukikamatwa hifadhini utakutana na kichapo cha haja kabla ya kufikishwa popote. Lakini wananchi tujiulize imekuwaje hali ikawa hivi? Je, Askari wanakosea sana au wako sahihi? Vipi wananchi nao hutimiza wajibu wao wa kufuata sheria bila shuruti?

Nikianza na Askari wanyamapori ni kweli kisheria hawako sahihi kupiga mtuhumiwa wala kuua. Kila mtu hana hatia hadi itakapothibitishwa na mahakama. Tukijikumbusha hali ya ujangili kwenye hifadhi za TANAPA na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro tunaweza kuona kwa kiasi fulani askari nao hawana jinsi zaidi ya kutumia mkono wa chuma ili sheria zifuatwe. Miaka ya 90 hado mwanzoni mwa 2000 kuna askari kibao waliuwawa na majangili huko Ngorongoro. Mwaka 2000 OCD wa Ngorongoro aliuwawa kwa kupigwa risasi na jangili la kisomali wakati akiwa kwenye operesheni. Bahati mbaya habari ya askari kuuwawa hazipewi uzito. Kwa wale msiojua ni kuwa ukiwa porini bora ukutane na wanyama kuliko jangili. Wao huwa hawana lingine zaidi ya kukuua. Nadhani pia mnamkumbuka mzungu wa harakati za kulinda tembo aliyeuwawa miaka michache iliyopita. Je, askari wafanyeje wakiwa katika hali hiyo?

Miaka ya nyuma kidogo enzi za JKIKWETE nilikuwa nikiongea na mwongoza watalii maarufu sana Arusha akawa anasikitika sana ujangili wa meno ya tembo unaoendelea hifadhi ya Tarangire. Akadai tembo wa Tarangire huwa ni wakali sana sababu ikiwa kujihami na majangili. Hayo majangili ya meno ya tembo ndo huwa wakikutana na askari hifadhini yanaua tu. Kwahiyo askari nao ili kujihami ni kuamua kufanya matumizi mazuri ya bunduki tulizowapa kulinda hifadhi. Majangili ukiyapeleka kwenye sheria huyashindi kwasababu ya utajiri walio nao. Au atahukumiwa kwenda jela miaka 2 au kulipa faini ya 500k. Mchezo umeisha.

Wananchi na sisi pia wengi wetu bila nguvu kutumika huwa hatuelewi kabisa. Kama ni kuni si ukatafute kwenye maeneo ya nje ya hifadhi? Kuna ulazima gani wa kuingia eneo la hatari ambapo Askari wako vitani na majangili? Huko hata ukikutana na jangili utapata shida tu. Mimi ninaunga mkono 100% nguvu kutumika kuondoa wananchi wanaoingia hifadhini bila utaratibu. Wananchi tufuate sheria.

Wewe una maoni gani?
 
Back
Top Bottom