The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
DIGITALI NA UWAZI SERIKALINI B.jpg


Uwazi wa serikali ni dhana kwamba watu wana haki ya kujua serikali yao inafanya nini na serikali ina wajibu wa kutoa taarifa kwa umma. Hata hivyo, kuna njia nyingi za kutafsiri uwazi wa serikali na siku hizi unaweza kupatikana kwa urahisi kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii.

Kadiri teknolojia inavyokuwa sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku, wananchi sasa wangependa kuona serikali zao zikitumia njia mpya na za kibunifu ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya uwazi wa utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa wananchi.

Uwazi wa serikali hauwezi kupatikana bila ushiriki wa wananchi. Kuwezesha ushiriki wa wananchi katika michakato ya kisiasa na kidemokrasia huanza kwa kuhakikisha kwamba serikali iko wazi na umma unaweza kufikia taarifa muhimu bila vikwazo.

Ikiwa serikali imejitolea kweli kuwa na uwazi, inapaswa kuwa tayari kuwekeza katika teknolojia inayoiruhusu kwenda zaidi ya kutoa habari tu. Uwazi katika karne ya 21 pia inamaanisha kuwapa umma, kwa mfano, utiririshaji (live-streaming) wa maudhui ya sauti na video za mikutano ya serikali na kuwezesha ufikiaji wa moja kwa moja wa maudhui hayo kwa wananchi.

Teknolojia ya digitali inaweza kufungua njia mpya kwa serikali kupata maoni kutoka kwa wananchi, hasa wale ambao wanakosa muda wa kuhudhuria mikutano ya hadhara au kukaa nyumbani ili kutazama au kusikiliza tena video au rekodi za mikutano hiyo.

Teknolojia ya digitali pia naweza kuhakikisha kuwa maudhui yanapatikana kwa watu wenye ulemavu wa kuona au kusikia, na inaweza kuwa mchakato wa gharama nafuu na usiotumia muda mwingi. Kutumia teknolojia ya digitali kunatoa fursa kwa wananchi kushirikishwa kikamilifu na kujihusisha na masuala wanayojali.

Matumizi ya teknolojia hii yanaweza kukuza uwazi kwa kuwaarifu washiriki kila hatua ya michakato ya serikali inapokamilika. Katika kupiga vita ufisadi, kuwawajibisha viongozi wa umma, na kujenga imani kwa raia, serikali zinaweza kupiga hatua ikiwa zitatekeleza sera za uwazi.

Mapinduzi ya teknolojia ya digitali yanasaidia kuongeza uwazi, ushiriki na ushirikiano. Katika miaka hii, matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa muhimu sana; yameongeza uelewa wa wapiga kura na kuwapatia uwanja mpana wa kutoa maoni yao ya kisiasa, na pia inawawezesha wanasiasa kulenga kundi maalum la watu.
 
Kweli, hii ndio uzuri wa serikali inayoongozwa na Mama mpenda Amani, Haki mwenye kujali na kuthamini watu wake.

Dkt Samia Suluhu Hassan OOOOOYEEEEEEE
 
Ndio! Teknolojia ya digitali inaongeza uwazi katika utendaji lakini SIO katika sekta zote, kwa sababu kuna baadhi ya sekta ambazo taarifa zake unaweza kuzipata MTANDAONI na kuna baadhi ya sekta ambazo taarifa zake hazipatikani MTANDAONI na kunakuwa na TAARIFA ZA NDANI.
 
Back
Top Bottom