Teknology na Maisha ya Nchi yetu

Nimekataa

JF-Expert Member
Dec 2, 2018
285
585
Habari zenu wakuu wangu?

Natumaini ni wazima na mnaendelea na majukumu yetu ya kila siku.

Mada kuu ni kama unavyo isoma hapo

Teknology kwa maisha ya sasa imekuwa sana, kiasi kwamba hakuna Taifa linaweza endelea ikiwa litaipa mgongo maendeleo ya Tech.
Kwa nchi kama ya kwetu hapa Tz kuna maendeleo madogo sana katika kukua kwa tasnia hii ya Science.

Kwani hata mipango na malengo makubwa ya maendeleo sioni swala la viwanda vya kitaaluma vyenye kuunda Mfano.Simu, Magari, Machine kubwa za kuchimba na ku lift mizigo, Uundaji wa mashine tiba,Undaji wa viwanda vya nishati mbali mbali.

Ukweli halisi ili tuinuke ki uchumi lazima tuwe na vyanzo vya mapato kutoka kwenye fedha za kigeni.

Mfano rahisi nchi kama Russia anatamba mbele ya nchi za NATO nikutokana na uzalishaji mkubwa wa Gass na Mafuta.
Ila sio mzalishaji mkubwa wa mafuta ya Alizeti na Maindi.

Wazo langu...
Dunia sasa imebadilika kwa kiasi kikubwa, kila taifa lina fanya biashara katika kupigania uchumi wake.
Hivyo basi ungefanyika utaratibu kupitia vyuo vyetu hapa Tanzania kuwaalika wataalam mbali mbali kutoka nchi mbali kama China na kwingineko bila kujali gharama ili tuwape mafunzo ya kisasa yanayo endana na maisha ya sasa.Na kuacha kusafirisha wanafunzi wachache nje na mwishoni huamua kubaki huko huko.

Na mataifa ya wenzetu wana wataalam wengi tuu na huko kwao hawana maisha na wala hawathaminiki kama China. Tuwachukue waje watupe madini mapya na sio haya madesa tulio nayo ambayo badala ya kuzalisha wasomi yana zalisha machawa.

Maana elimu yetu imeshindwa kabisa kukua kwa Science yaan tuna wasomi ambao wameshindwa hata kuunda tuu Bulb ilio gundulika zaidi ya miaka miatatu nyuma.

Nchi nzima macho yapo kwenye reli bwawa la umeme na pesa za mkopo. Mkumbo huu unazoa kuanzia wanavyuoni mpaka bodaboda na mimi kilaza wa mwisho yaani hakuna tofauti ya alie enda shule na yule alie enda banda la video kuangalia ma picha picha.

Mwisho kila mtu pale alipo atatue changamoto zake kwa kutumia ubongo wake.Na sio kila kitu Mama...ooh serikali.Yaani hata kuvunja kokoto na nyundo unataka usaidiwe.

Asanteni. Taifa niletu sote
 
Ndipo ninapo muelewa JPM kuwa tuzalishe umeme wetu wakutosha na tuuze nje ya nchi.
 
kweli mkuu tunaweza tukawaokota wataalam wanaoachwa hovyo huko Duniani tukawaleta hapa kwetu wakatusaidia kutuboost kwenye issue za tech
 
kweli mkuu tunaweza tukawaokota wataalam wanaoachwa hovyo huko Duniani tukawaleta hapa kwetu wakatusaidia kutuboost kwenye issue za tech
Kabisaa...
China kuna mpaka vijana wana uwezo wakuunda vifaa mbali mbali vya umeme na taaluma kubwa kubwa lakini hawana maisha...
Ila wale tukiwapata na kuwajengea Camp na kuwafanya jamaa zetu hakika tutatoka kupitia wasomi wetu.
 
Mkuu nimekuelewa sana, tukitumia teknolojia vyema tutapiga hatua sana.
Bila tech hatuendi kokoteee broo...
Watu niwengi maitajio ni makubwa.
So lazima tuwe na machine ziweze kutukidhi katika maisha yetu.

Na hii ni nadra sana wakubwa zetu kujua
 
Back
Top Bottom