Team Magufuli vs Team Mafisadi

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Utafiti makini na wa kina uliofanywa na team ya wadadisi makini wa mambo ni kwamba mafisadi, majizi, majitu yenye husuda na chuki dhidi ya nchi yetu ndani na nje ya Nchi yameungana pamoja dhidi ya Magufuli kuhakikisha kwamba hafanikiwi katika dhamira yake ya kuileta Tanzania tuitakayo. Ishara kuu ya majitu haya ni kupinga kila zuri analofanya JPM.

Kumkatisha tamaa na kum frustrate ndio mana kila anapofanya zuri mfano kuzindua barabara ya njia nane yenyewe yanapinga, akizindua daraja la kupita majini yenyewe yanapinga, akijenga madaraja ya juu yenyewe yanapinga, akinunua ndege mpya yenyewe yanapinga....Magu yeye asiyumbe.

Ashikilie hapo hapo.
 
Unamzungumzia Magufuli yule ambae majuzi alikuwa na Fisadi Nyangumi pale Ikulu au Magufuli yupi hasa?

Unamzungumzia Magufuli ambae kaenda kujenga international airport kijijini kwao huku tenda ya ujenzi akimpa mshikaji wake Matiko; au Magufuli gani hasa?

Unamzungumzia Magufuli huyu huyu ambae wizara yake ilinunua kivuko substandard kwa mabilion ya pesa na kwa kuchelea watu wasihoji akaamua kwenda kukificha JWTZ, au Magufuli yupi unayemzungumzia?

Ni Magufuli huyu huyu ambae pamoja na kufahamu Tanzania imetafunwa sana na Wanasiasa Teule na top government executives lakini anaogopa kuwataja hata majina; au ni Magufuli mwingine?!

Ni Magufuli huyu huyu ambae hivi karibuni serikali yake imecheza tiktaka na kudai LUGUMI ipo clean kabisa na waliosema ni fisadi ni wazandiki au unazungumzia akina Magufuli ambao bado wapo Chato?!

Hebu twende taratibu! Ni Magufuli yupi?! Ni yule ambae wiki kadhaa zilizopita aliutangaziwa umma kwamba RC wa Dar ni Mkwepaji wa Kodi au kuna Magufuli mwingine huko serikalini?!

Au unamzungumzia Mussa Magufuli ambae aliuziwa nyumba ya serikali na kakake pasipo kufuata utaratibu?!
 
Wanapinga huku wakipita kwenye hayo mabarabara na madaraja? Pia na ndege wanapanda? Mashenzi hayo. Yapotezee!!!!!
 
Huu kama kweli ndo utafiti, basi vyuoni wanatufundisha ujinga sana..... Na mm nadhan ipo haja sasa ya kufanya marekebisho ya mtaala wa elimu. Maana kwa namna hii sidhani kama Taifa tunaelekea wapi!!!!!
Hoja hupingwa kwa hoja sio kwa vioja. Kamalizie kupika baba anataka kula ana njaa
 
Huu kama kweli ndo utafiti, basi vyuoni wanatufundisha ujinga sana..... Na mm nadhan ipo haja sasa ya kufanya marekebisho ya mtaala wa elimu. Maana kwa namna hii sidhani kama Taifa tunaelekea wapi!!!!!
Hivi ilikuwaje mtaa unakopikwa upuuzi kama huu ulipewa jina la la mwanamapinduzi mashuhuri kabisa Afrika!!??
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Heri kuwa fisadi, mwizi na n.k kuliko hata wewe mjinga unayefikiri naendeleo ya nchi ni dhamira ya mtu 1!
 
Wanapinga huku wakipita kwenye hayo mabarabara na madaraja? Pia na ndege wanapanda? Mashenzi hayo. Yapotezee!!!!!1
Hivi hao mafisadi ni akina nani haswa?Maana kwa mujibu wa jiwe anahoji,"kwani huko nyuma mlikuwa hamlipi kodi?msiniulize zilikwenda wapi maana siyo kazi yangu kujibu"
Sasa tujiulize,wakusanyaji wa kodi walikuwa akina nani na walizipeleka wapi?????
Baadaye unamsikia jiwe akiendelea,"waacheni wastaafu wapumzike,wamelifanyia mambo makubwa taifa hili"
Yaani hapo mpaka kichwa kinauma kutafakari!
 
Unamzungumzia Magufuli yule ambae majuzi alikuwa na Fisadi Nyangumi pale Ikulu au Magufuli yupi hasa?

Unamzungumzia Magufuli ambae kaenda kujenga international airport kijijini kwao huku tenda ya ujenzi akimpa mshikaji wake Matiko; au Magufuli gani hasa?
Anamzungumzia yule aliyempa kimada nyumba ya serikali!Anamzungumzia yule aliyegawa kivuko kibovu kwa jeshi ili watu waache kuhoji ununuzi wake!Anamzungumzia yule aliyejipa tenda ya kutengeneza vitambulisho vya wajasiliamali na kuchukua 20,000 kwa kila mjasiliamali!
 
Uchambuzi wako si wa kina, ni wa unazi zaidi kuliko uhalisia.

Ukija na msimamo kuwa wafanyabiashara ni mafisadi au wapiga dili, basi hata uchumi lazima utakupa shida
 
Anamzungumzia yule aliyempa kimada nyumba ya serikali!Anamzungumzia yule aliyegawa kivuko kibovu kwa jeshi ili watu waache kuhoji ununuzi wake!Anamzungumzia yule aliyejipa tenda ya kutengeneza vitambulisho vya wajasiliamali na kuchukua 20,000 kwa kila mjasiliamali!
WHAAAAAAAAT😈😈😈!!!
 
Back
Top Bottom