TCRA yataka makampuni ya simu kusitisha matangazo yanayowekwa kabla ya miito ya simu

watakuwa wametusaidia sana kama watatekeleza kweli maana ilishakuwa ni kero sana ....unasikiliza tangazo dakika 15 ndo simu inaanza kuita au unaambiwa haipatikani na muda mwingine unahamua kukata tu ata kabla haijaita.
 
watakuwa wametusaidia sana kama watatekeleza kweli maana ilishakuwa ni kero sana ....unasikiliza tangazo dakika 15 ndo simu inaanza kuita au unaambiwa haipatikani na muda mwingine unahamua kukata tu ata kabla haijaita.
Safi sana!
 
Wamechelewa sana hawa jamaa!
Mtu unapiga simu dakika moja nzima unasikiliza matangazo halafu baadaye unaambiwa "namba ya mteja unayempigia hapatikani". Jinga kabisa!!!

Wasiishie hapo tu waangalie na vifurushi vya data, ni aibu kwa Ulimwengu huu Internet kuwa bado ni anasa. Na pia mtu akitaka kujiunga basi apewe chaguo kama anajiunga bando la internet ajiunge la internet, Kama anajiunga la sms ajiunge la SMS vivyo hivyo kama anajiunga la dakika basi ajiunge la dakika.

Na sio kupewa Dakika, SMS na Mb 3 (ujinga mtupu)
Mkuu kwenye bando sio siri wanatuibia sana
 
huwa nahangaika kutafuta nchi yenye mobile data za bei rahisi kushinda Tanzania, nimetafuta almost dunia nzima nchi maarufu zote nimekosa, sisi tuna raha sana vifurushi bei rahisi na speed pia sasa kwenye 4G zipo vizuri.
Mkuu habari kuna uzi nilianzisha kutaka msaada wako hukutokea anyway nina simu ya tecno c8 haisomi 3g nilipo ingawa simu zingine kama samsung etc zinasoma ila nikitoka hapa kwenda sehemu nyingine yaani mji mwingine inasoma shida ni nn natumia tgo
 
Naona hili Tangazo limemgusa kila mmoja,

Hapa ndo watawala wajue sasa kumbe watu wanafurahia mambo mazuri yakitendeka,

Na sio habari za kulazimishana kumkubali mtukufu.
 
Mimi Tigo ndio huwa wananishangaza......yaani hata simu yangu iwe na salio la 10,000/= lakini kila dakika simu yangu inaingia sms inayoniambia salio lako halitoshi......yaani kwa siku moja naweza kufuata zaidi ya meseji hamsini za aina mpaka imekuwa kero kwangu.....
Pole sana. Hii kuna mteja wetu pia ilikuwa inamtokea hasa hasa kama unatumia iphone. Solution, chukua iyo namba uiBLOCK hautapata tena izo sms.
 
Back
Top Bottom