TCRA inavumilia matusi na uvunjaji wa maadili kwenye Vyombo vya habari!

Ni kweli mkuu lakin BASATA wanahusika pia,kifupi ni kwamba hawa wameishiwa wanatukana mpaka aibu! KUIGIZA WANAWAKE NI UPUUZI AMBAO HAUVUMILIKI,WASHENZI KABISA!.

Leo tutatawatazama tena tutathmini kama mwendo mdundo au wamepunguza hii kadhia inayokera haswa
 
ze comedi wamefulia zamaani, nshaacha kuangalia huu sijui mwaka wa ngapi
 
Kwani nani anahusika? Wizara ya Nchimbi? Au TCRA? Ninavyojua hawa kina kayombo(wa TCRA) wanahusika na Mawasiliano...Ilitakiwa kipindi cha uchaguzi watuambie nani alikuwa anatuma message za kumkashifu dkt. Slaa. Hata hivyo all in all wote wako Polluted!
 
Waswahili wanasema Muungwana ni Vitendo:

Nachukua fursa hii kwa moyo wa Dhati kuwapongeza wasanii wa ZE COMEDY baada ya kusikia kilio chetu na kufanyia marekebisho kale kasegment ka kauzu kuliko Dagaa.

Nilikuwa nimeamua kutotazama hasa napokuwa na familia katika eneo hili la kauzu kuliko Dagaa. Kwa wiki mbili mfululizo nimeona wanatumia maeneno fulani hivi ya kulalamika laiki hayasikiki vizuri ambao mie nauona kama ubunifu mzuri na bado lengo linalokusudiwa kuonyesha mzazi analalamika linafika bila kutukana kama ilivyokuwa awali.
 
TCRA wamekaa kimya kabisa mpaka alipuke mbunge mjengoni ndio utasikia wanaamka, lakini hata TBC hivi chombo cha taifa hakina kweli bodi ya maudhui au ndio wakurugenzi wote hawajui hata miiko ya weledi wa habari, bora liende
Mtajijibu wenyewe magamba maana tukiwaletea maada mnasema wapinzani hatuna point..Jiulize na Ujijibu kwanini Tido Mhando alikatizwa mkataba wake TBC? Mtasema siasa tena?
 
Back
Top Bottom