TBS na TFDA okoeni maisha yetu kwa kupima ubora wa unga wa mahindi na muhogo unaosagwa mitaani

Katika mambo yote kuhusu vyakula vya nafaka, mimi nagopa sana hicho kitu kinachoitwa "fortification" kinachofanyika katika unga wa sembe.

Kwa fikra zangu hizo fortifications ni "slow killing poisons" za kuua watu weusi kwa siri, ni mpango wa wazungu, tunanunua sumu kujiua sisi wenyewe. Unless TBS etc, watuambie hizo fortifications zinaongeza kitu gani katika miili yetu na kwa utafiti upi walioufanya.
TBS watakuambia bila hata kufanya utafiti, hawana muda huo siku hizi. Siku hizi bidhaa nyingi zina nembo ya ubora TBS lakini kilichomo hakina ibora huo, nilinunua unga wa sembe wa kiwanda kimoja kikubwa nchini, nilichokikuta ni nusu unga nusu chenga! Sasa hizo chenga unazifanyaje?
 
Unga mwingi tunakula uchafu maana mashine nyingi hazitoi vyuma.
 
Miaka ya hivi karibuni kumezuka viwanda vingi sana mitaani vinavyosaga unga wa mahindi na muhogo, ubora wa unga huo u atia mashaka kwani viwanda husika haviko kwenye usafi unaoridhisha.

Kiwanda ambacho hakiko kwenye usafi hata ubora wa unga wake utatia shaka, ni wazi viwanda hivyo vina mashine ya kukoboa na kusaga, havina mashine ya kusafisha nafaka husika hivyo kunauwezekano mkubwa kusagwa na takataka nyingine.

Nafaka zinazopatikana miaka hii huwa na uwezekano wa kuathirika na sumu kuvu na sumu zitokanazo na madawa ya kuhifadhia nafaka pamoja na ya kuua wadudu mashambani, haya yote ni hatari kwa afya zetu.

Ni jambo lililo wazi nchini kwetu hakuna utamaduni wa kichukua sampuli madukani na kwenda kuzipima maabara, TBS na TFDA nendeni madukani mchukue sampuli mkazipime naamini matokeo yatalishitua taifa kutokana na utitiri wa viwanda vya vichochoroni.
Hili jambo mi muhimu sana. Maindi pia huwekwa sumu ya kuzuia yasiliwe na wadudu, bilaa kuyasafisha vizuri kabla ya kuyasaga yanaweza kuleta madhara kwa binadamu.
 
Yes,kwa sasa maisha ni kujilinda mwenyewe kwanza maana sumu ni nyingi sana kwa vitu tunavyotumia.
Hapa kumezungumzwa sana unga zaidi lakini kuna mboga za majani,huko ndo balaa zaidi lilipo.Watu wanapiga dawa na kuuza mboga kabla siku 7 hazijaisha.
Ukija matumizi ya nyanya ni dawa dawa dawa sana.....Lakini pia nyama na maziwa tunazokula na kunywa ambazo nyingine zimetokana na wanyama kutibiwa mda mfupi kabla ya kuchinjwa.
Wengi wetu tunakula mayai iwe kwenye chips au vinginevyo...hao kuku wanapata dawa na vitamins nyingi sana za dukani na zote zina masharti yake unapotaka kutumia product ya kuku aliyepewa hizo dawa au vitamins,watu hatuzingatii na wenye mamlaka hawasisitizi maana wengine hawafanyi kwa makusudi bali kwa kutokujua coz mtu hana habari ya kusoma maelezo ya kwenye packict.

Kwenye matumizi ya mbolea huko nako sijui madhara yake sana ila nina wasiwasi napo.
Shamba la ekari moja la mpunga watu wanaweka hadi mifuko 6 ya mbolea sasa hapo sijui nini kinatokea kwenye miili yetu.
 
Je, kunahaja ya uongozi ulipo sasa wa TBS kuwepo madarakani au tupaze sauti uondolewe ili tupate viongozi wengine watakaojali afya zetu kwa kusimamia vizuri ubora wa vyakula?
 
Miaka ya hivi karibuni kumezuka viwanda vingi sana mitaani vinavyosaga unga wa mahindi na muhogo, ubora wa unga huo u atia mashaka kwani viwanda husika haviko kwenye usafi unaoridhisha.

Kiwanda ambacho hakiko kwenye usafi hata ubora wa unga wake utatia shaka, ni wazi viwanda hivyo vina mashine ya kukoboa na kusaga, havina mashine ya kusafisha nafaka husika hivyo kunauwezekano mkubwa kusagwa na takataka nyingine.

Nafaka zinazopatikana miaka hii huwa na uwezekano wa kuathirika na sumu kuvu na sumu zitokanazo na madawa ya kuhifadhia nafaka pamoja na ya kuua wadudu mashambani, haya yote ni hatari kwa afya zetu.

Ni jambo lililo wazi nchini kwetu hakuna utamaduni wa kichukua sampuli madukani na kwenda kuzipima maabara, TBS na TFDA nendeni madukani mchukue sampuli mkazipime naamini matokeo yatalishitua taifa kutokana na utitiri wa viwanda vya vichochoroni.
TBS miyeyusho. Niliwahi kuwashtua siku moja kuhusu mikate isiyo na nembo ya TBS iliyozagaa huku mitaani, nikakusanya sample tatu za mikate kutoka watengenezaji tofauti, lakini sikuona hatua zozote zikichuliwa.

Na hao watengenezaji sio wengi kivile na wanajulikana wako wapi. Ukifanya sampling operesheni ya mwezi mmoja tu utawapata wote na kuwachukulia hatua stahiki.

Ukiwa unafanya operesheni za kushtukiza kila mwaka watajifunza na kufuata taratibu.
 
Umbea huo unaingilia kazi za watu, unadhani kamati ya ulinzi na usalama eneo vilipo hivyo viwanda hawavioni?
 
Je, kunahaja ya uongozi ulipo sasa wa TBS kuwepo madarakani au tupaze sauti uondolewe ili tupate viongozi wengine watakaojali afya zetu kwa kusimamia vizuri ubora wa vyakula?
TBS wameshindwa kazi..TFDA irudi..hapa jpm alipotoshwa sana.

Samia sikiliza kilio cha wananchi taifa linakula sumu wananchi wanaumia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom