TBL building a $55 million brewery in Mbeya

US$55million only for Beer plant??
Tanzania hatuna miradi mingine jamani?? Je wakulima wa ngano wanafaidika vipi na hili?
Je mashamba hayo ni yaleyale tunayohitaji kwa ajili ya vyakula???
I'm really disappointed by this..... Tanzania is the only country in East Africa with 5+ Beer plants.
Which booming economy is there in TZ to justify sucha capex? Ulevi ulevi ulevi........
 
US$55million only for Beer plant??
Tanzania hatuna miradi mingine jamani?? Je wakulima wa ngano wanafaidika vipi na hili?
Je mashamba hayo ni yaleyale tunayohitaji kwa ajili ya vyakula???
I'm really disappointed by this..... Tanzania is the only country in East Africa with 5+ Beer plants.
Which booming economy is there in TZ to justify sucha capex? Ulevi ulevi ulevi........

Hizo ni pesa za mwekezaji na siyo za serikali, mwenyewe ameamua kuongeza uzalishaji kutokana na ongezeko ya wateja! Unapouliza hakuna miradi mingine, ulitaka serikali ipewe hizo pesa ijengee barabara?

Common guys, this is not rocket science jamani!!!!
 
Tatizo la nchi yetu hawaweki misingi imara ya kubenefit kutoka kwenye makampuni mbalimbali,.Watu watapata ajira lakini kununua bidhaa zetu na kuzitumia kwenye uzalishaji hili ndo la muhimu saana kwa sasa.

Nashangaa wanachukua ngano south africa ,na sukari,sasa faida za kuwa na wawekezaji zipo wapi?

Kwa hesabu za haraka haraka tu chukulia wewe ndiye ungekuwa unafanya hiyo investment. Lengo ni kupata faida kubwa kwa kupanga bei nzuri na kuhakikisha unapunguza kabisa gharama za uzalishaji na uendeshaji wa kiwanda!

Sasa swali linakuja, je ni wapi ambako utachukua ngano na sukari yenye ubora unaohitajika kwa gharama nafuu zaidi ili upate faida zaidi? Ni Tanzania au South Africa? Jibu liko wazi kwamba kuchukua ngano na sukari toka South Africa kunaongeza gharama za uzalishaji. Sasa kwanini bado waendelee kuleta ngano toka South Africa? Unadhani ni suala la uzalendo kwa nchi yao hilo?

Hapana, ni kwamba Tanzaia hakuna REALIBLE source za ngano iliyo bora, iliyo ya kutosha kuendesha uzalishaji wa kiwanda. Na kuhusu sukari, unazo taarifa kwamba hata viwanda vyetu havitoshelezi mahitaji ya sukari kwa nchi nzima? Na je wajua kwamba kuna sukari inayoagizwa nje ya nchi hata kwa matumizi ya wananchi wa kawaida tu achilia mbali matumizi ya viwandani?

Kabla ya kulalamika, tufikirie zaidi kuhusu hii nchi yetu iliyojaa ubabaishaji, miundombinu isiyo ya ukakika. Umeme wa Dar sasa hivi baadhi ya maeneo hata microwave tu wakati mwingine unashindwa kuiendesha. Inasemekana Mafuta House wanatumia jenereta kwa kuwa umeme wa TANESCO hautoshi kuendesha lile jengo! Bado unategemea mwekezajia ategemee wakulina na viwanda vya Tanzania katika mahesabu yake ya uzalishaji wenye tija ili kuurudisha pesa zake (ROI) katika muda unaotakiwa?
 
Changamkeni sasa, anzisheni kampuni za ulinzi kwa kuwa TBL hawawezi kuajiri mlinzi mmoja mmoja. Wanaingia mkataba na kampuni ya ulinzi ambayo inakuwa responsible na ulinzi wa eneo zima la kiwanda. Ndivyo mambo yanavyokwenda, mkilemaa mtashangaa wanaletwa KK Security toka Dar!

Halafu Watanzania bado tuko kwenye usingizi mzito sana kwenye suala zima la uwekezaji. Yaani nilishangaa kugundua kwamba asilimia 95% ya makampuni yote makubwa ya Ulinzi ni ya wazungu!! Ukienda viwandani ndio usisema, vyote ni vya wahindi.

Watanzania wengi wanaoitwa wafanyabiashara wana maduka ya jumla, salon za kunyolea nywele, salon za kike, mwingine ana madaladala 10, mwingine ana taxi 5....Hao ndio wajasiriamali tulionao. Waliobaki wote wameajiriwa maofisini. PERIOD!!!

Inasemekana hata dili kama za EPA zimeanza miaka mingi iliyopita na zilikuwa zinawashirikisha wahindi peke yao. Walipokosea mwaka 2005 kuwaingiza Waswahili ndipo mambo yalipoharibika! Aibu!

du

ndo maana naona umuhimu wa watu wazima sie kufundishwa hata namna ya kufungua na kuendesha biashara

serikali yetu kwa makusud ingekuwa inatoa maarifa haya. ila naona haioni haja kwa sababu kuna watu - wahindi - sorry - ambao wana maarifa haya na wana endesha businesses

serikali yetu ingefungua vituo sehemu mbalimbali kote tz (ikiangalia ni maarifa/mbinu zipi) zifundishwe wapi. ingekuwa kama elimu ya watu wazima. tofauti hapa ni kuwa ingekuwa inalenga kuanzisha na kuendeleza businesses

tutajuaje kama hatujafundishwa?

naweza kuwa mhasibu au mhandis. nafanikiwa kukusanya mil 5, 10, 15, au hata 20. zaid zaid ntakachokimbilia kufanya ni kununua hiace, kufungua saloon, tax and stuff like that
 
kwa nchi, naona kuna faida nyingi za kuwa na kiwanda kingine cha bia kuliko hasara

huenda tunaweza kuona viwanda vya bia vinaongezeka zaid kwa sababu viwanda vingine hatuna

kama alivyosema mtanzania, cha zaid jamaa wabanwe au waombwe watumie raw materials from tz zaid kama vile kutoka arusha
 
Ukimlazimisha anaweza kwenda nchi nyingine. serikali kupitia wizara ya kilimo ingejaribu kuwaelimisha wakulima njia bora ya kuzlisha hizo mali ghafi (sukari, ngano etc) kwa wingi na ubora mzuri. Tungekuwa na wakulima wachache wakubwa ingesaidia sana.
Kwa sasa nchi ina faidika kwa kupata kodi na ajira .
Tukumbuke tulipotoka , ulikuwa huwezi kupata bia mpaka kwa vibali (kama una harusi una bidi ku attach card ). Na bia ilikuwa moja tu - Safari
 
Wakati ule ukitoka ukifika Bar unaagiza kama 10 unaweka chini ya meza ..manake wanaochelewa unakuta zimeisha! Sema safari za wakati ule zilikuwa tam sana tofauti na sasa!

Sasa kama serikali inapata kodi mnalalamika nini? mnataka watu wanywe gongo anu Mnazi?
 
Hawa jamaa waongo kweli, according to me the world financial meltdown itawafanya watu tunywe saaana kwani ndo tutasahau shida zetu. Sasa hawa wanahofia. We angalia nyumbani mtu anaweza asiwe na mboga lakini ya ulabu iko pale pale!

Wabongo hatuna periorities, kuanzia wananchi wenyewe, viongozi, serikali na nchi kwa ujumla. Bora tujirushe tu na mabia moto na baridi. Kili baridi yuko wapi???????
 
Watanzania ni wakali wa kinywaji na totoz! mambo mengine mkiani! Kwi kwi kwi!!!

Muhimu tu ni kuna ndugu zetu watapata ajira na taifa litapa mapato. Ni kuwabana tu hawa makaburu watumie ngano yetu na sio kubeba kila kitu toka kwao.

...tuko pamoja hapo,acha watu wajipatie kazi ndio muhimu,na kwa revenue ya almost 300bn naona serikali at 35% corporate tax rate inakomba zaidi ya 100bn,wish tungekuwa na makampuni 50 tuu kama haya bugdet yetu ingejitosheleza vizuri sana
 
Wakati ule ukitoka ukifika Bar unaagiza kama 10 unaweka chini ya meza ..manake wanaochelewa unakuta zimeisha! Sema safari za wakati ule zilikuwa tam sana tofauti na sasa!

Sasa kama serikali inapata kodi mnalalamika nini? mnataka watu wanywe gongo anu Mnazi?

ehe,

zimekuwa kali? mi nijuavyo zikiwa kali zinamfanya mnywaji anywe chache na hivyo chache zitauzwa.

sasa hii si kujipunguzia soko kwa tbl?

wangezifanya tamtam
 
Wabongo hatuna periorities, kuanzia wananchi wenyewe, viongozi, serikali na nchi kwa ujumla. Bora tujirushe tu na mabia moto na baridi. Kili baridi yuko wapi???????

priorities? zipi hizo? au kivip?

mwenye mtaji na muamuzi ni tbl. suppose priority yetu ingekuwa kutumia hiyo hela kujenga chuo cha teknolojia dodoma au kuanzisha kiwanda cha chuma tungefanyaje na hali tbl ndo mwenye hela?
 
Hao TBL wakae wakijua pamoja na jitihada zao za makusudi na nia njema ya kujenga kiwanda hicho, jamaa wateendelea na Kimpumu chao kama kawa
 
Watu bwana!

Eti bia ni ulevi..sasa wanataka wote tunywe tu soda?

Mie soda haipandi kabisa! Sasa ninywe nini?
 
"Ongeza sita baridi na nne moto hapa......na wape wale kinadada tatu tatu za baridi", aliagiza Liyumba.
 
TBL ndiyo kampuni inayoongoza kulipa kodi Tanzania tukumbuke

Bwana tafadhali, TBL ni mawakala tu wa kukusanya hiyo kodi, sisi wananchi tunaopata 'kilaji' ndio tunaolipa kodi. Serikali imeamua kuwa sehemu kubwa ya budget yake itutegemee sisi wanywaji.

Sijui wanampango gani kwani tutakapo amua kuwa sote walokole na waswahilina safi basi mapato hakuna tena! Inaudhi sana, kila ikifika July bungeni kodi kwenye kinywaji imeongezeka kiasi fulani, sipendi kabisa, matokeo yake kila mwaka ni kupoteza wanachama ambao huamua kujiunga kwenye "supu ya mawe" kwa kushindwa kufikia bei ya bia.
 
Back
Top Bottom