Tbc1 na intaneti

chibhitoke

Member
Jun 1, 2010
60
12
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikisikia wasomaji taarifa za habari za TBC1 wakisema ''habari hii imetumwa kwa njia ya internet''. Mimi naona kama kuna tatizo- intaneti ni njia ya kawaida ya mawasiliano mbona hawasemi zinazotumwa kwa njia ya posta, EMS au simu.

Nimewahi kuona vituo vya nje wanapoona ubora wa picha zao sio mzuri ndipo husema samahani picha hiyo imetumwa kwa internet. Sasa hawa wenzetu inaonesha huo ndio mchezo wa kila siku
 
Wanaona ni sifa sana kusema hivyo... Una jua vituo vingi vya tv hapa tz taarifa zao za mikoani huwa wanazipata kwanjia ya mabasi au ndege, hivyo wao kupokea habari kwa njia hiyo wanaona wamepiga hatua.
 
mimi jana niliwatumia sms wakati wanasoma habari saa mbili usiku kwamba waache ushamba wa "habari hizi zimeletwa kwetu kwa njia ya intaneti". nilitegemea watasoma ushauri wangu kama wanavyofanya kwa wanaposifiwa na watazamaji. wakamezea ushauri wangu. kazi ipo.
macinkus
 
Hawa jamaa ukiwaponda kwa sms kupitia Taarifa, Jambo au Usiku wa Habari sms yako inawekwa kapuni!
 
Jamaa washamba kwelikweli! Huwa nawashangaa sana wanaposema hivyo. Sijawahi kusikia kituo chochote duniani kinasema habari hii imekutufikia kwa njia ya internet. Kwani internet si ni njia ya kawaida tu! Waache ushamba bwana!
 
Back
Top Bottom