Malisa Godlisten
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 201
- 1,534
SAKATA LA MURO: KESI YA PANYA KAPEWA PAKA.
SAKATA la madai ya kuomba Rushwa ya shilingi Mil.10 linalomkabili mwandishi wa shirika la Habari la TBC, Jerry Muro linahitaji uchanganuzi wa Kina, na fikra yakinifu zitakazokidhi haja za watanzania wanaofuatilia swala hili, na kuondoa utata unaoonekana wazi.
Suala la Muro limejaa utata na halieleweki wazi si tu kwa wananchi wanafuatilia, bali hata yeye nadhani hajui kunachoendelea.
Utata huu unatokana na mambo makuu mawili. Kwanza ni mazingira ya kukamatwa kwa hicho kinachodaiwa Rushwa na pili ni wahusikakatika Kesi yake.
Mazingira ya Kesi tangu kukamatwa kwake hadi kufikishwa kituoni yanaibua maswali mengi kwa kila mwenye fikra hai. Murro alikamatwa Jumapili ya tarehe 31/01/2009 akiwa katika gari lake aina ya Cresta GX100 lenye namba za usajili T 545 BEH na kufikishwa katika kituo kikuu cha Polisi Mkoa wa Dar; kwa madai ya kuomba rushwa ya Sh. Million 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Bw. Michael Wage.
Bw. Wage anadai kwamba aliombwa rushwa hiyo na Muro siku mbili kabla ya kukamatwa, walipokutana na Muro katika Hotel moja jijini Dar. Hivyo Muro alipofikishwa kituoni hapo alitakiwa kutoa maelezo kuhusu tukio la siku mbili zilizopita.
Haingii akilini mtu kuomba rushwa leo halafu eti akamatwe siku mbili baadae; Lazima Umma uelezwe kwanini hakukamatwa siku hiyo hiyo alipoomba rushwa? Au labda makachero wote wa Polisi walikuwa wameenda likizo hivyo ilibidi kusubiri hadi siku mbili baadaye watakaporudi kutoka huko walikokuwa wameenda kula good time.
Lakini pia ni kwanini Bw. Wage hakuripoti Sakata hilo TAKUKURU ambao kisheria ndio wanaoshughulikia rushwa? Angeenda TAKUKURU angepewa noti zilizojizolea umaarufu kama Pesa za moto ambazo zingetumika kama ushahidi mzuri wa kumtia Murro hatiani. Je, Wage hafamu kuwa TAKUKURU ndio wenye dhamana ya madai yote yanayohusu rushwa? Kama anafahamu hilo, alienda Polisi kufanya nini?
Kwanini alikimbilia Polisi badala ya TAKUKURU? Huko polisi alikuwa anamfuata nani? Lazima swali hili lijibiwe kwa ufasaha na uyakinifu.
Lakini cha kuchekesha ni kwamba alikamatwa bila ushahidi wowote uliohusu Rushwa. Si noti za moto za TAKUKURU wala sarafu za Polisi alizokutwa nazo Murro.
Badala yake Polisi waliibua madai ya kukutwa na pingu ambayo hayana uhusiano wowote na kesi ya msingi ya Rushwa.
Lakini hili la pingu nalo linahitaji mjadala mpana. Mjadala huu ni kutokana na mazingira ya kukutwa kwa Pingu hizo. Gazeti la Nipashe la Jumatatu February 1/2010 liliripoti kuwa Murro alipofikishwa Kituoni hapo alipelekwa sehemu ya juu (Ghorofani) ya kituo kwa ajili ya mahojiano. Wakati Murro akiwa kwenye mahojiano gari lake lilikuwa likilindwa na askari kanzu.
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi, siku hiyo alipoombwa rushwa Wage alidai kuona Pingu ndani ya gari la Muro. Hivyo Muro alipokamatwa gari yake ikalazimika kupekuliwa. Lakini funguo zikapotea katika mazingira yaliyojaa utata hapohapo kituoni. Hivyo Muro kulazimika kupiga simu nyumbani kuomba funguo za akiba.
Lakini kabla funguo za akiba hazijafika, zile zilizopotea zilipatikana na pingu hizo kukutwa ndani ya gari la Jerry; Je, nani alikuwa na funguo hizo?? Je, nikisema kwamba kuna askari alipoka fungua hizo na kwenda kuweka Pingu kwenye gari la Muro nitakuwa nimekosea?? Au nikisema wale makachero walioachwa kulinda gari wakati Muro akiwa kwenye mahojiano walitumia mbinu zao za Kimafya kutumbukiza Pingu katika gari la Muro nitakuwa navunja kifungu gani cha Sheria??
Lakini Wage, (mhasibu aliyesimamishwa kazi na waziri Mkuu kutokana na shutuma za ubadhirifu) akaibua hoja nyingine mufilisi. Eti alipokuwa kwenye gari ya Muro (wakati Muro akimuomba rushwa) alisahau miwani yake ambayo baada ya upekuzi ilikutwa kiti cha mbele wakati wa upekuzi.
Binafsi sidhani kama kukutwa kwa miwani kinahusika na sakata la msingi la Rushwa. Bali kwa kutumia ushahidi wa miwani kwa mbaaali kunaweza kutusadikisha (japo si sana) kuwa Wage alipanda gari ya Muro. Lakini je, kila anayepanda gari ya Muro anaombwa rushwa? Kama kila anayepanda gari ya Muro huombwa rushwa basi madai ya Wage yatakuwa na msingi; vinginevyo hizo ni fikra kurupushi tu.
Katika gari ya Muro kulikutwa vitu kadhaa, vikiwemo vifaa vyake vya kazi. Lakini pia ilikutwa miwani, boksi mbili za tissue na pingu za mkononi.
Viwili kati ya hivyo yaani miwani pamoja na tissue, Wge alidai ni mali zake na alizisahau aliposhuka. Kama amekiri kumiliki miwani na tissue na kwamba alivisahau aliposhuka, basi yawezekana hata hizo pingu yeye ndiye mmiliki wake na alizisahau tu, kama alivyosahau hivyo vingine. Kama aliweza kusahau miwani (anayoitumia kila siku), kwanini tushindwe kuamini kuwa hata hizo pigu alizisahau??.
Baada ya kuona namna MAZINGIRA ya Kesi yalivyojaa utata hebu tuangalie WAHUSIKA katika Kesi hii.
Michael Wage ambaye ndiye mlalamikaji mkuu katika Kesi hii ni mhanga katika bomoabomoa iliyofanywa na waziri mkuu mhe.Mizengo Pinda ambapo watendaji wa juu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo walisimamishwa kazi.
Lakini ikumbukwe kuwa hadi waziri mkuu kufikia hatua ya kuwasimamisha watendaji hao kazi inadaiwa Murro ndiye aliyefichua ufisadi uliokuwa umeighubika Halmashauri hiyo. Kwa tafsiri hiyo Muro ndiye aliyewachomea utambi watendaji hao, na kwa maana hiyo wana hasira nae. Hivyo nikisema Kesi hii ni ya kupikwa sidhani kama kimantiki itapingika.
Lakini hata jeshi la Polisi nao si marafiki sana wa Muro maana nao walishajeruhiwa na makucha yake.
Akiwa ITV Muro aliwahi kufichua rushwa iliyotolewa kwa trafiki katika maeneo ya barabara ya Dar Moro. Habari hiyo ilirushwa na kituo cha televition cha ITV kupitia kipindi cha Ripoti maalum haikufurahiwa sana na Polisi maana Askari polisi 13 walisimamishwa kazi kwa tuhuma hizo za rushwa. Lakini pia hivi majuzi Murro alishiriki kuandaa kipindi cha Usiku wa Habari kilichorushwa na TBC -1 ambapo askari wa Usalama barabarani Mkoa wa Iringa walionekana wakipokea Rushwa.
Hili nalo liliongeza idadi ya maadui wa Muro na labda pia liliibua mbinu za namna ya kumzima. Ndio! Hatakiwi kuendelea kuumbua wakubwa kwa kile anachokiita Habari za Uchunguzi. Nani ana uhakika wa kupona kama akiachiwa aendelee kufichua? Yeah! Lazima azimwe maana fichua fichua yawezekana akafichua pasipofichulika.
Lakini jumatatu tarehe 1/February/2010 Kamanda wa Polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam; Selemani Kova aliongea na waandishi wa habari kuelezea tukio la kukamatwa kwa Muro. Pamoja na kuongea sana (kama kawaida yake) alinukuliwa na vyombo vya habari akisema ..hapa namsaidia Wage kusema; maana haya alipaswa kuyasema yeye.
Kauli hii inaibua utata kwa kila mwenye akili timamu. Wage ni nani hadi aajiri Jeshi la Polisi kumsemea? Kwa lipi hasa? Na kwa ujira wa shilingi ngapi?
Baadhi ya watu wenye fikra finyu walimsifu RPC Kova kutoa tamko bila kujua kuwa Kova alikuwa anajishtaki mwenyewe. Kwa kukiri kwamba anasema kwa niaba ya Wage; ina maana kuwa Wage ndiye aliyemtuma aseme. Swali. Tangu lini Kamanda Kova amefanyika kuwa Afisa habari/msemaji wa Wage??
Napotafakari kauli ya Kova (Kwamba alimsaidia Wage Kusema) naanza kupata majibu kwanini Wage hakwenda TAKUKURU na badala yake akakimbilia Polisi.
Kutokana na kauli hii uhusiano baina ya Kova na Michael Wage unapaswa uchunguzwe ili tujue msimamo wa RPC wetu. Ikiwezekana achague moja kama ataendelea kuwa RPC au ataacha kazi yake ya upolisi abakie na hiyo mpya ya kuwa Afisa habari wa Wage.
Kwa ujumla mlalamikaji katika Kesi hii Michael Wage pamoja na wanaoendesha kesi hii Jeshi la Polisi wamewahi kuwa majeruhi wa Muro kwa nyakati tofauti. Halafu eti leo ndio wanaongoza upande wa mashtaka katika Kesi ya yuleyule mbaya wao. Halafu tunategemea haki itendeke. Thubutu!! Hicho ni kichekesho. Tusishangae kuona Muro akipokwa HAKI yake waziwazi maana Kesi ya Panya kapelekewa Paka. Ni uzandiki.

Niachie ujumbe:
0715-187677;
0712-025958