TBC Aibu

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
TBC mnatutia aibu kuliwacha hilo screen bovu nyuma ya mtangazaji wa taarifa ya habari. Kumbukeni kuwa hii TV inatazamwa ndani na nje ya Tanzania, mnaitia doa jeusi Tanzania kote inakotazamwa.

Natazama taarifa ya habari sasa hivi hiyo screen nyuma inaonesha kabisa kuwa imechuja liquid upande wa chini kushoto, inaonesha baka jeusi, hivi hamuioni au ndio hamjali au ndio uzembe wa hali ya juu?

Mnatutia aibu, hivyo vi screen vimejaa kila kona si mbadili tu muweke nyingine? au mkaitowe ile iliyopo ofisini kwa Mkurungenzi wenu muiweke hapo panapoonekana uzembe wenu dunia nzima na hiyo ya hapo mkamuwekee Mkurugenzi wenu ofisini kwake.

Haya mambo yanakera na ni ya kijinga sana. Huyo mkurugenzi afukuzwe mara moja kwa huu ujinga. Hili ni kosa kubwa sana na si la mzaha. Mnaonesha uzembe wenu duniani!
 
Wamechoka kama serikali ya chama chao, dalili za kuchoka hizo!
 
Hii ndio bongo, chako ni kile kilichoko mfukoni, vingine sijali, uzalendo wa nini wakati familia inaishi vizuri na hivi vijisent ninavyopata. Mkuu Zomba nchi imeuzwa, huenda mkurugenzi wa shirika hajawahi kufika hapo studio yapata mwezi. Hii ni hatari sana na ni fedheha kwa Taifa.
 
TBC mnatutia aibu kuliwacha hilo screen bovu nyuma ya mtangazaji wa taarifa ya habari. Kumbukeni kuwa hii TV inatazamwa ndani na nje ya Tanzania, mnaitia doa jeusi Tanzania kote inakotazamwa.

Natazama taarifa ya habari sasa hivi hiyo screen nyuma inaonesha kabisa kuwa imechuja liquid upande wa chini kushoto, inaonesha baka jeusi, hivi hamuioni au ndio hamjali au ndio uzembe wa hali ya juu?

Mnatutia aibu, hivyo vi screen vimejaa kila kona si mbadili tu muweke nyingine? au mkaitowe ile iliyopo ofisini kwa Mkurungenzi wenu muiweke hapo panapoonekana uzembe wenu dunia nzima na hiyo ya hapo mkamuwekee Mkurugenzi wenu ofisini kwake.

Haya mambo yanakera na ni ya kijinga sana. Huyo mkurugenzi afukuzwe mara moja kwa huu ujinga. Hili ni kosa kubwa sana na si la mzaha. Mnaonesha uzembe wenu duniani!

Mkuu nilisha wasema sana kwa nia njema TU, lakini sijuhi ushauri wangu walikuwa wanauchukuliaje?
 
Hiyo ndiyo taswira ya taifa letu. Tunautangazia ulimwengu madhaifu yetu na jinsi viongozi wetu wasivyo makini katika utendaji wao.. Si ajabu ikaachwa hata miezi kadhaa mbele
 
ndugu yangu tbc hata mkienda na matarumbeta pale kwao kutaka wafanye mabadiliko japo tu ya kununua fagio jipya bado hawata tilia maanani.......iki chombo kinakufa kwa vile kiko chini ya serikali ya chama cha nanihii
 
TBC mnatutia aibu kuliwacha hilo screen bovu nyuma ya mtangazaji wa taarifa ya habari. Kumbukeni kuwa hii TV inatazamwa ndani na nje ya Tanzania, mnaitia doa jeusi Tanzania kote inakotazamwa.

Natazama taarifa ya habari sasa hivi hiyo screen nyuma inaonesha kabisa kuwa imechuja liquid upande wa chini kushoto, inaonesha baka jeusi, hivi hamuioni au ndio hamjali au ndio uzembe wa hali ya juu?

Mnatutia aibu, hivyo vi screen vimejaa kila kona si mbadili tu muweke nyingine? au mkaitowe ile iliyopo ofisini kwa Mkurungenzi wenu muiweke hapo panapoonekana uzembe wenu dunia nzima na hiyo ya hapo mkamuwekee Mkurugenzi wenu ofisini kwake.

Haya mambo yanakera na ni ya kijinga sana. Huyo mkurugenzi afukuzwe mara moja kwa huu ujinga. Hili ni kosa kubwa sana na si la mzaha. Mnaonesha uzembe wenu duniani!

hakuna chombo cha habari nisichokipenda km TBC,koz kinaendeshwa kwa kutumia ilani ya chama chao,dhaifuuuu
 
a Dar waongezeka

BOOKMARK THIS PAGE

?

?

Vigogo waliopata mgawo Viwanja Dar waongezeka

*Send to a friend

Thursday, 26 July 2012 20:36

??Patricia Kimelemeta
MLOLONGO mrefu zaidi wa majina ya vigogo umebainika kugawiwa viwanja katika eneo la Gezaulole, jijini Dar es Salaam, ambapo safari hii imo familia ya Rais* mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassani Mwinyi.

Jana, gazeti hili lilichapisha katika ukurasa wa mbele habari iliyoonyesha baadhi ya majina ya vigogo waliogawiwa viwanja na kufanya wananchi wa kawaida kulalamika.

Katika uchunguzi zaidi, imebainika kuna orodha ndefu ya majina ya vigogo waliopewa viwanja katika mradi huo wa Gezaulole ambayo inahusisha mawaziri, wabunge, wakuu wa taasisi za Serikali na familia za baadhi ya watu maarufu. *

Kwa upande wa familia maarufu, imo ya mzee Mwinyi ambaye pia amegawiwa eneo, wengine wana majina ya ukoo yanayofana na ya kwake ambao ni, Asina Mwinyi, Maimuna Mwinyi, Salama Mwinyi na Steven Ali Mwinyi, huku kutoka katika familia yenye jina la Kikwete yumo Ali J. Kikwete.

Viongozi wengine maarufu waliogawiwa viwanja hivyo ni Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emanuel Nchimbi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Manejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.

Kwa upande wa watendaji wa taasisi za dola, yumo Katibu* wa Bunge, Dk Thomas Kashilila, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, Balozi wa Tanzani nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, SACP Hamdan Makame, ACP John Gudaba, ACP Saada Juma Haji na* ACP Mohamed Usi.

Mlolongo huo pia unaonyesha majina ya baadhi ya wabunge ambao ni Murtaza Mangungu wa Kilwa Kaskazini (CCM), Mohamed Misanga, (Singida Kusini CCM), Jenister Mhagama (Peramiho CCM), Kheri Ameir (Matemwe, CCM), Kaika Telele (Ngorongoro, CCM), Amina Clement (Koani, CCM) na Ali Hamis Seif (Mkoani, CUF)** *

Pia kuna orodha ya wabunge wa Viti Maalum CCM ambao ni Subira Mgalu, Alshaiymaa Kweygir, Elizabeth Batenga, Josephine Genzabuke, Betty Machangu, Lediana Mng’ong’o na Mwanakhamis Kassim Said.

Wabunge wengine wa Viti Maalum CCM ni* Mariam Mfaki, Mariam Kasembe, Agnes Hokororo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa pamoja na* Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa Viti Maalum, Chadema na Ania Said Chaurembo ambaye ni mbunge mstaafu.* *

Majina mengine ambayo koo zake ni za watu maarufu ni pamoja na* Ahmed Dau, David Kandoro, Asila Ditopile, Alice Koka, Gemini Suchak, Fidelis Owenya, Filoteus Msigwa, Evelyne Manumba, Fatma Ismail* Rage, Jamhuri Kihwelo, Issack Mwang’onda, Hijjal Makamba, Joseph Nyambibo, Mbwana Samata, Mohamed Mzimba na Mohamed Mtonga.

Wengine ni pamoja na Masanja Manumba, Mariam Mkama, Mansour Al-Maamry, Onesmo Mtasiwa, Musa Chagonja, Omary Shein, Shimbo Shimbo, Sikitu Kijazi, Solomon Kivuyo, Thomas Nyalile na Aisha Sululu (diwani Jangwani, CCM).

Pia wamo maofisa watatu wa Bunge ambao ni Herman Berege, Anslem Mrema na Theonest Ruhilabake pamoja na mmoja wa maofisa waandamizi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Boniface Njombe.

Wananchi waja juu
Baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke walisema fomu zilizochukuliwa ni zaidi ya 20,000 na kwamba kila fomu ilikuwa ikiuzwa Sh30,000, hivyo kufanya fedha zilizokusanywa kuwa zaidi ya Sh600 milioni.

Tayari mlolongo huo wa majina ya vigogo umesababisha baadhi ya wananchi waliokuwa wakisoma majina hayo kulalamikia mchakato wa utoaji viwanja hivyo, huku wengine wakidai kuwa, warejeshewe fedha zao.

“Tumelipa Sh20,000 kila fomu ya kuombea kiwanja na wananchi tuliojitokeza ni karibu 30,000, lakini majina yanaonyesha kuwa asilimia kubwa ya waliopata ni vigogo ambao tunaamini wana viwanja mahali pengine,” alisema mwananchi mmoja(jina limehifadhiwa).

Mwananchi huyo alisema kuwa, hakukuwa na umuhimu wa kutangaza zabuni hiyo kwa sababu tayari walikuwa na majina yao, hivyo* walitakiwa kuwakabidhi viwanja vyao badala ya kuwasumbua na kuwatoza fedha.

“Hali hii inaonyesha kuwa Serikali ipo kwa ajili ya watu wachache, wenye fedha na si wananchi wa kawaida,” aliongeza.

Mwananchi mwingine (jina tunalo), alisema idadi kubwa ya watu waliokabidhiwa viwanja hivyo ni watoto wa vigogo na wabunge.

Aliongeza kuwa hali hiyo inaonyesha wazi kuwa, hakuna kiongozi atakayewatetea wananchi, kwa vile kila mmoja wao yupo kwa ajili ya kupigania maslahi yake.

“Wabunge ambao tuliwategemea kutetea maslahi ya wananchi ndio wanaoongoza kwenye orodha ya kujichukulia viwanja, hii inaonyesha wazi kuwa hakuna kiongozi atakayeacha shughuli zake ili kutetea maslahi ya wananchi,” alisema.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Manispaa hiyo vinaonyesha kuwa, halmashauri hiyo imeingiza zaidi ya Sh600 milioni kutokana na uuzaji wa viwanja hivyo.



?

digg

Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
? ? ? ? ? ? ? ? ? ?

*

Comments?*

?1??2?

*

?#16 Alphonce ?2012-07-27 14:55

???

+10

Watanzania wanaishi maisha magumu kwa ajili ya CCM,lakin iko siku watajutia hayo wanayofanya

Quote

*

*

?#15 Alpha ?2012-07-27 14:29

???

+1

Inashangaza sana kuona watu tunashindwa kujua vile viwanja haikuwa sadaka ili ni biashara ambayo ilikuwa huru kwa mtu yoyote kununua.Ifahamike kwamba hao baadhi ya wananchi walipewa vocha na kushndwa kuzilipia na kuamua kuziuza sasa leo wanaongea mambo ya majungu na unafiki mtupu

Quote

*

*

?#14 mlupilo ?2012-07-27 13:46

???

+1

Hiyo ndio Tanzania.....KUNA WANANCHI NA WENYE NCHI. Mtanzania angalia tofauti ya hayo mawili.

Quote

*

*

?#13 MARMA KUBINI ?2012-07-27 13:42

???

+3

KWELI INANISHANGAZA SANA NDUGU ZANGU KWANI IDADI KUBWA YA WA2 HAWA NI VIONGOZI JE WAMETUMIA VIGEZO GANI KUWAPA WABUNGE NA WATU WENYE PESA HUKU LINDI LA WATU WALIO MASIKINI WANAANGAIKA KUTAFUTA MAHALI,TUSIDANG ANYANE PESA HIZO WALIZOVUNA MANISPAA HAZITAPITA BURE KWANI KUNA WATU HAWAKULA ILI WALIPIE VIWANJA THEN WANAPEWA WATU MATAJIRI KWELI?TIBAIJUKA MAMA UPO NA HILI UNALIONA KWELI AU?

Quote

*

*

?#12 E ?2012-07-27 13:13

???

-1

Jamani nisaidieni nimeuliwa watu wa dar watau hawajui grzaulole iko wapi.
Nisaidieni kuniambia mahali ilipo.

Quote

*

*

?#11 ll ?2012-07-27 12:44

???

+1

Quoting Omary maruzuku:

Hiyo ndio tz bwana. Tuwe makini kwenye katiba mpya hiyo ndio ambayo itatusaidia ss na vzaz vyetu. Wananchi tumechoka hali hii mpaka lini bwana. aliokuwa nacho anaongezewa asiokuwa nacho anazidi kupokonywa hata hicho alichokuwa nacho. mpaka lini? je tutafika? Tuamke kudai uhuru wetu. Ramadhani kareem.



katiba mpya nini bwana, hiyo wanaandika hao hao wakubwa.

Quote

*

*

?#10 michael william ?2012-07-27 12:16

???

+1

Nafikiri viongozi na watu wengine wenye uwezo walipaswa kwa utashi wao kujiondoa kwenye huu mchakato ili watu wa chini na wa kati ndio wapatiwe viwanja maana hata kiwango cha pesa kilivyowekwa kinaonyesha dhahiri kiliwalenga watu wa uwezo wa chini. Tatizo viongozi hawawapendi wananchi wao, asiyeshiba kwenye sahani hata kwenye sinia hawezi kushiba na hicho ndicho walichonacho viongozi wa nchi hii.

Quote

*

*

?#9 mwajuma r ?2012-07-27 11:56

???

+4

inauma sana.ilia Mungu yupo'na hakika iko siku mtalipia gharama za matendo yenu duniani.

Quote

*

*

?#8 Omary maruzuku ?2012-07-27 10:04

???

+3

Hiyo ndio tz bwana. Tuwe makini kwenye katiba mpya hiyo ndio ambayo itatusaidia ss na vzaz vyetu. Wananchi tumechoka hali hii mpaka lini bwana. aliokuwa nacho anaongezewa asiokuwa nacho anazidi kupokonywa hata hicho alichokuwa nacho. mpaka lini? je tutafika? Tuamke kudai uhuru wetu. Ramadhani kareem.

Quote

*

*

?#7 reginald thy barhe ?2012-07-27 09:55

???

+6

... hao ndo viongozi wetu wanaosimama jukwaani kutuhadaa kuondoa umasikini, kumbe umasikini ni wao wenyewe kujinufaisha, haswa hao wanaojulikana kuwa wakombozi wa kijani, jama kinyani sasa maana yake haina tofauti sana na ilhali halisi tunayoona kule ughaibuni kwa kina Ghaddafi, Ben Ali na Hosni Mubbarak na sasa Bashar... waliyafanya hayo hayo, subirini kama mnafikiri Tanzania huo usingizi wa u[NENO BAYA] kama utaendelea milele.... Na ninyi ciku yenu haiko Mbali, mnawaweka watoto wenu madarakani, ardhi na mali asili zetu badala ya kuwanufaisha masikini wa nchi hii uwanufaishe ninyi.....inatosha inatosha endeleeni, mahakama yenu ambao ni raia karibu wanachemka....na ndo kwa makusudi hayo hayo kina Lowasa wanasafisha majina kwa gharama yeyote lakini Muamuzi ni boksi la kura ikishindikana subirini mapanga na marungu na wakati huo mtajitahidi kutumia jeshi kama Libya, Tunisia, Misri na sasa Syria.. na wote mtashindwa maana na jeshi itabidi iamue kuwa la raia ama la mafisadi wachache, poleni lakini ni ulevi wa madaraka, mgekuwa na masikio yanayosikia na macho yanayoona, na utashi ulio hai.... Baba Wa Taifa alikuwa mwalimu tosha Kwa UADILIFU WAKE... ONENI MPAKA LEO WATZ WANAMPENDA NA KUMSIKIA... wengine wenu Wtz wanatamani kuwazika bado mpo hai... Nasema Ole wenu... na Tena Ole wenu...

Quote

*

*

?#6 Paul David ?2012-07-27 09:49

???

+13

Familia ya mwinyi wanaviwanja na wamekalia mikocheni na mpaka hapa mbezi njia ya kawe wamekaa, kaaka na dada yaani mheshimiwa Husein Mwinyi na dada yake, Baba yake amejenga nyumba mbili tena gorofa zinazofanana kwa wake zake tena amepewa uwanja mkubwa tu, kwani na sisi walalahoi hatuitaji hivyo viowanja? Jamani tuachieni na sisi pia, maana mara ya kwanza Gezaulole, tuliambiwa vimepimwa kwa ajili ya wabunge na hii nayo tena , hadithi ni zile zile tu, hakuna jipya, serikali ya CCM ndivyo ilivyo.
fisadi kila kona.

Quote

*

*

?#5 tinsoldier ?2012-07-27 09:36

???

+8

Ukiangalia wengi ni CCM kama yupo wa chama kingine ni nadra kwa hiyo CCM kweli ni Chukua Chako Mapema

Quote

*

*

?#4 Alitan ?2012-07-27 09:20

???

-17

Kwani kuwa kiongozi kunaniondolea sifa ya kupata kiwanja cha nyumba?
Hayo ni majungu

Quote

*

*

?#3 Kamura ?2012-07-27 08:51

???

0

No comment.

Quote

*

*

?#2 Nikolas ?2012-07-27 08:37

???

-2

Ni haki ya kila mtu kupewa kiwanja, tusiwataje na kuwakashifu viongozi waliopata kwani ni haki yao pia, shida na tatizo ni kwenye ugawaji, ikiwa viwanja ni vichache,KWELI UMPE MBUNGE KIWANJA KWA SHS ELFU 30, wasitoe zabuni za bei chini km hiyo, kwani hapo wametumia ujanja wa kudanganya wengi walipe ili wapate pesa nyingi, kwa hali ya gharama za sasa, upimaji, uwekaji wa miundo mbinu, wangetaja gharama halisi, ambayo ingepunguza hata wenye uwezo wa kulipia, pia masharti baada ya kupewa kiwanja unatakiwa ukamilishe ujenzi ndani ya muda maalumu, hii itazuia ujengaji holela na magofu, na vichaka ktk makazi yetu.TAJENI GHARAMA HALISI,BAADA YA KUWEKA MIUNDO MBINU YOTE, KM BARABARA ZA LAMI KUU NA ZA MITAA, MFUME WA MAJI SAFI NATAKA, UMEME, MASHARTI YA MUDA WA KUKAMILISHA UJENZI NA AINA YA NYUMBA ZINAZOTAKIWA. HII ITAPUNGUZA MALALAMIKO.

Quote

*

?1??2?

?Refresh comments list

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!

?Name (required)

?E-mail
 
tbc mnatutia aibu kuliwacha hilo screen bovu nyuma ya mtangazaji wa taarifa ya habari. Kumbukeni kuwa hii tv inatazamwa ndani na nje ya tanzania, mnaitia doa jeusi tanzania kote inakotazamwa.

Natazama taarifa ya habari sasa hivi hiyo screen nyuma inaonesha kabisa kuwa imechuja liquid upande wa chini kushoto, inaonesha baka jeusi, hivi hamuioni au ndio hamjali au ndio uzembe wa hali ya juu?

Mnatutia aibu, hivyo vi screen vimejaa kila kona si mbadili tu muweke nyingine? Au mkaitowe ile iliyopo ofisini kwa mkurungenzi wenu muiweke hapo panapoonekana uzembe wenu dunia nzima na hiyo ya hapo mkamuwekee mkurugenzi wenu ofisini kwake.

Haya mambo yanakera na ni ya kijinga sana. Huyo mkurugenzi afukuzwe mara moja kwa huu ujinga. Hili ni kosa kubwa sana na si la mzaha. Mnaonesha uzembe wenu duniani!

hongera yaani unasikiliza habari zilizo haririwa na mhariri mkuu wa serikali!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom