sasa wamegoma kutuletea bunge live??manake sasa naona wale wachina wao wanaoongea kiswahili!
Kuna siku imepita bila ya kutaja dini yako? Wewe nadhani hata mada kama inazungumzia mpira lazima utataja diniTanzania watu wanafanya kila njia kuuondoa utamaduni wa kanzu na kofia na khanga kuwa ndio vazi la asili na linalotumiwa na watu wengi kwa ufinyu tu wa mawazo kuwa ni la Kiislaam. Ndio maana unaona kuhangaika kote huku.
Yana hayo mambo ya vazi la taifa yananiudhi sana,wakikupigia hesabu ya hizo gharama unaweza kuzimia
Ni aibu kubwa sana kwa Taifa au jamii kukosa vazi la taifa ambao ndio unakuwa utambulisho wenu mnapokuwa ndani au nje ya mipaka ya nchi yenu.
Hebu nitazameni mimi hapo kwenye avatar yangu nikiwa na vazi letu la taifa. Je kwa vazi hilo si unaweza kujua natoka nchi gani.
Fungukeni na mtafute utambulisho wenu kitaifa na kimataifa.
Kitengo cha propaganda na uenezi cha ccm, sio tv ya taifa hiyo
i see. .
Vazi la taifa?
Sijui 'ishu' ya nani hii!
ni kweli kabisa tangu tido aondolewe TBC imeshuka sana tarifa za habari ni aibu tupu, watangazaji wanapata aibu pale mchanganya picha za matukio anaposhindwa kuunganisha picha za matukio yanayofuata.
Bado wanaendeleza siasa zao za kifisadi na kuficha mambo muhimu kwa wananchi. Ukiona hivyo ujue kuna move inafanyika pale Bungeni ya ambayo hawataki watu waione live kwa sababu ni aibu kwa serikali. Lakini wamefanya hivyo purpose kabisa. Mtasikia baadae moto uliowaka huko.
Nimepata tetesi kuwa kuna karatasi imepitishwa mle Bungeni na imesainiwa na wabunge zaidi ya 2/3 kuwa hawana imani na PM. Sasa hivyo move ni kali kwelikweli haiwezi ikawekwa LIVE. Tusubiri.