TBC aibu tupu kwa taifa

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
253
Kikao Muhimu cha bunge kinaendelea Dodoma na TV ya taifa ni lazima si ombi kuwaonyesha wananchi wake kitu ambacho wawakilisho wao wanakijadili Bungeni.

Cha ajabu hii tv inakatika katika na tangazo kubwa wanalotuwekea ni VAZI LA TAIFA. no excuse nothing, So shame for the great Nation which we are all proud of it.

DR's still on strike to wake up the Government
 
Vazi la Taifa ndo interest ya ccm kwa sasa so usipoteze muda wako kuwafuatilia, hawajali lolote about vikao vya bunge
 
ccm wanataka kuvaa sasa wapendeze, ni mapema sana ukilnganisha na matatizo tuliyonayo
 
Yana hayo mambo ya vazi la taifa yananiudhi sana,wakikupigia hesabu ya hizo gharama unaweza kuzimia
 
Hivi nchi zenye vazi la taifa zilipataje vali hilo? Walifuata utaratibu kama huu tunaopewa sisi? Vazi linapigiwa kura kama mbunge!!
Lakini nani atavaa hilo vazi na kwa uda upi? Kazini au katika sherehe?
Kwa nini vazi la taifa sasa na si kabla?
 
We uliona wapi TV wakati wa kutoa ripoti toka mkoani kwa mfano sikia hii- Mwanaripoti wetu Hosea Cheyo wa Mbeya anatuhabarisha zaidi kutoka Mbozi......... Hapo itapigwa pozi ya dakika 10 na mtangazaji anang'aa macho tu hana la kufanya. sasa huwa sielewi kuwa CD imekwama au mtayarishaji anaitafuta. TBC the most boring TV. Ukisikia sa sa ni habari za kimatifa basi wataleta item moja tu na kusikia huu ndio mwisho wa habari za kimataifa. sasa kwenye prime news unaweka item moja. Mimi huwa sielewi huwa hakuna habari za kutosha au ni wavivu kutafuta news.
 
Wewe hujawajulia? Kwenye kujadili mambo yanayowafagillia CCM na serikali ndiyo wanaonyesha kwa mbwembwe. Ikitokea mjadala unaiwajibisha serikali hasa kutoka kwa upinzani wanafunika kwa kuweka hayo matangazo na kama hilo la vazi la taifa ambalo kwetu sisi Watanzania siyo wakati wake kuna mambo muhimu zaidi ya kujadili kujinasua kutoka katika hii hali mbaya ya maisha tuliyonayo!
 
Bado wanaendeleza siasa zao za kifisadi na kuficha mambo muhimu kwa wananchi. Ukiona hivyo ujue kuna move inafanyika pale Bungeni ya ambayo hawataki watu waione live kwa sababu ni aibu kwa serikali. Lakini wamefanya hivyo purpose kabisa. Mtasikia baadae moto uliowaka huko.

Nimepata tetesi kuwa kuna karatasi imepitishwa mle Bungeni na imesainiwa na wabunge zaidi ya 2/3 kuwa hawana imani na PM. Sasa hivyo move ni kali kwelikweli haiwezi ikawekwa LIVE. Tusubiri.
 
Hili la vazi la taifa wadau linakera,hiz ghalama za kulitafta ukijumlisha na zile za miaka 50 ya uhuru zingetosha kuongeza mshahara wa madaktari.
 
Mkuu fafanua kdg hapo kwenye red, mbona unaturusha roho wenzio!
 
Aibu tupu kuita tbc tv ya taifa, tv za taifa za mataifa yote africa zinaonesha mashinda ya mpira ya africa lakini tbc hawaoneshe, Toka Tido mhando alipo ondolewa tbc hakuna jipya tena
 
Hili la vazi la taifa wadau linakera,hiz ghalama za kulitafta ukijumlisha na zile za miaka 50 ya uhuru zingetosha kuongeza mshahara wa madaktari.

Naomba uelewe kuwa nchi hii inakimbizana na mambo ya kijinga siku zote ndugu yangu,usione ajabu kwa hilo.
 
Ni aibu kubwa sana kwa Taifa au jamii kukosa vazi la taifa ambao ndio unakuwa utambulisho wenu mnapokuwa ndani au nje ya mipaka ya nchi yenu.

Hebu nitazameni mimi hapo kwenye avatar yangu nikiwa na vazi letu la taifa. Je kwa vazi hilo si unaweza kujua natoka nchi gani.

Fungukeni na mtafute utambulisho wenu kitaifa na kimataifa.
 
we ni raia wa nchi gani?
 
Hivi na ninyi mlipigia kura hilo vazi ulilovaa?
Suala ni kuwa utaratibu wa kupigia eti vazi la taifa.......only Tz..
 
Ni aibu kubwa sana kwa Taifa au jamii kukosa vazi la taifa ambao ndio unakuwa utambulisho wenu mnapokuwa ndani au nje ya mipaka ya nchi yenu.

Hebu nitazameni mimi hapo kwenye avatar yangu nikiwa na vazi letu la taifa. Je kwa vazi hilo si unaweza kujua natoka nchi gani.

Fungukeni na mtafute utambulisho wenu kitaifa na kimataifa.

Dkt. nakubaliana nawe kabisa lakini mimi nadhani vazi la taifa hutokana na majority ya wananchi wake kulivaa. Wewe hapo omani ni nani alimichagulia kanzu na kilemba? Sasa tuangalie na sisi tulikuwa tunavaa nini kwa ujumla wetu hakuna haja ya kuweka promo!
 
Back
Top Bottom