Tazama upendeleo wa wazi anaofanyiwa Messi kwenye Kombe la Dunia

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,837
Kwenye mechi dhidi ya Croatia Messi mliona alivyopiga chenga na na kutoa pasi nzuri iliyozaa goli la 3. Ilikuwa pasi nzuri na ni kweli ilionyesha Messi ni mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani

Basi mitandao ilichafuka kwa sifa kuhusu alivyocheza Messi dhidi ya Croatia

Lakini jana kwenye mchezo dhidi ya Morocco tuliona Mbape alivyocheza na yeye kuchomoka kwenye kichaka cha mabeki na kutoa pasi iliyozaa goli la 2 la Ufaransa.

Ukiacha hata pasi hiyo Mbape alikuwa kacheza vizuri na kuleta hatari zaidi ya mara 3 kwenye lango la Morocco, Lakini Mbape hazungumziwi kabisa,

Ingekuwa ni Messi au hata Ronaldo angecheza kama Mbape jana, mitandao ingelipuka.

FB_IMG_1671081577695.jpg
 
Mbona huongelei Julian Alvarez na goli lake la pili mechi dhidi ya Croatia, ni solo goal na zuri zaidi ya mengi tu yaliyofungwa kwenye hii World cup. Umemuona Mbape tu.
 
Subiri Mbappe afikishe umri wa miaka 35 kwanza kisha afanye kama anachofanya Messi.
 
Kijana kaamka asubuhi hata hajanywa chai, donge limembana na choyo juu ya mchezaji mwenye kipaji zaidi duniani, anatoa povu lake.

Huyo unayemlalamikia kwamba anazungumzwa sana hilo ni dogo sana, kubwa timu zote zinazocheza dhidi ya timu yake zinalazimika kubadili mfumo na kutengeneza mfumo wa kumkaba yeye kwanza na mengine kufuatia
 
Hata Messi aliposhiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza 2006 midomo ya watu ilikuwa kwa akina Ronaldinho na Ronaldo De Lima.

Messi ameshajaribiwa na kujidhihirisha kuwa ni bora ndiyo maana anakuwa appreciated. Hao wengine hatujui kama kweli wako njema kivile au wamebahatisha!
 
Messi na Ronaldo ni biashara za watu zile ndo maana kwenye balon do'r hata wachezaji wengine wacheze vipi lakini hawapewi zile ni brand za watu na zinalindwa kwa gharama yoyote ile.
 
Messi na Ronaldo ni biashara za watu zile ndo maana kwenye balon do'r hata wachezaji wengine wacheze vipi lakini hawapewi zile ni brand za watu na zinalindwa kwa gharama yoyote ile.
Walishabetiwa mafanikio.
 
Back
Top Bottom