Tawi letu la Buzuruga Mwanza limezinduliwa

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,216
7,908
Naibu katibu mkuu wa chadema kamanda salum mwalim muda mfupi uliopita ametuzindulia tawi letu hapa buzuruga jijini mwanza, kata ya buzuruga ni kitovu cha mabadiliko ambapo kata ya buzuruga ina mitaa mitano katika uchaguzi wa serikali za mitaa chadema tulichukua minne na ccm mmoja
attachment.php

attachment.php
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1420285887.036985.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1420285887.036985.jpg
    86.2 KB · Views: 1,631
  • ImageUploadedByJamiiForums1420286013.837471.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1420286013.837471.jpg
    94.7 KB · Views: 403
  • ImageUploadedByJamiiForums1420286177.721191.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1420286177.721191.jpg
    95.2 KB · Views: 1,527
  • ImageUploadedByJamiiForums1420286217.968475.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1420286217.968475.jpg
    104.3 KB · Views: 406
Mbona kimyakimya?

Chadema ni msingi ni silent killer mkuu, naibu katibu mkuu alikuwa ameambatana na mwenyekiti wa bavicha taifa, baada ya uzinduzi wa tawi letu kamanda kaenda magu na baadae lamadi ambapo atakuwa na mkutano wa hadhala, yaani kimya kimya
 
hilo ni tawi la chadema au ukawa maana nimeona na bendera ya nccr ktk moja ya picha

Hilo ni tawi la chadema, hapo unapoona pamefunikwa turubai ni kijiwe chetu kinaitwa kijiwe cha ukawa na juu kumefungwa bendera za cdm, cuf na nccr, hapo ndo kazi inapofanyika ndo maana unaona matokeo ni 4-1 serikali za mitaa.
 
Naibu Waziri wa Afya Mhe.Steven Kebwe akabidhi Zahanati msaada wa Kitanda chenye thamani ya Shilingi Millioni tatu na nusu na mchango wa zaidi ya Shilingi Millioni mbili na Laki tano kwa Mwenyekiti wa CHADEMA huko Serengeti Mara.

Naibu Waziri wa Afya Mhe.Steven Kebwe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mkoani Mara kupitia CCM, alimkabidhi Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyansurura kupitia CHADEMA Mhe.Francis Garatwa Muhingira Kitanda cha akina Mama Wajawazito chenye thamani ya Tsh.3,500,000 (Million tatu na Laki tano katika Zahanati ya Kijiji cha Nyansurura.

Tukio hilo lilifanyika mbele ya Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyansurura Bw.Maxmillian Peter Nyamhanga, Katibu wa Mbunge Bw.Masosota na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyansurura Bw.Nyantito.

Pia Mhe.Kebwe alisema kwamba ameweka Tsh.1,000,000 (Million Moja) kwenye Akaunti ya Zahanati ya Kijiji cha Nyansurura na Shule ya Msingi Matanka kama mchango wake wa kununulia Mifuko ya Saruji ili kufanikisha Ujenzi wa Zahanati hiyo na Nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Msingi Matanka.

Pia Naibu Waziri Mhe.Kebwe amesema kuwa ametoa Tsh.561,000 (Laki tano Sitini na moja Elfu) katika Akaunti ya Shule ya Sekondari Nyansurura kama mchango wake kwenye zoezi la Ujenzi wa Jengo la Maabara.

Kwa niaba ya Wananchi wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho cha Nyansurura kupitia CHADEMA Mhe.Garatwa bila kuangalia tofauti za Kiitikadi na Kisiasa, ametoa shukrani zake kwa Mhe.Naibu Waziri kwa mchango wake huo wa zaidi ya Shilingi Millioni mbili na nusu na Kitanda chenye thamani ya Shilingi Millioni tatu na nusu kwa ajili ya akina Mama Wajawazito na Wagonjwa wengine.

Source:Jamii forums
 
Back
Top Bottom