Mbowe, Mwalimu watikisa Butiama

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
- Wabeba Mwenyekiti wa Kijiji na wajumbe wake

Na Mwandishi Wetu
FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu, leo wamepata mapokezi makubwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Buhemba, wilayani Butiama, mkoani Mara.

Katika mkutano huo, Magige Magera Musyoni, aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Magunga, Kata ya Mirwa, eneo la Buhemba, aliamua kujitoa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga CHADEMA.

Mwenyekiti huyo wa kijiji amejiunga na CHADEMA, ikiwa ni takribani miaka miwili tangu avuliwe uenyekiti wa kijiji na katibu wa CCM wilaya ya Butiama na Katibu huyo kumteua mwanachama mwingine wa chama hicho,Daud Saruya, kuwa mwenyekiti wa kijiji.

Kuondolewa kwa Magige kunahusishwa na misimamo yake ya kutetea wananchi na kupinga matumizi mabaya ya fedha na mali za umma yaliyotuhumiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa CCM na serikali yake kwenye ngazi ya kijiji na kata, akiwemo, Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo, anayetuhumiwa kutumia mabati ya kujengea shule ya umma, kwa maslahi yake binafsi.

"Moses Onyango, Mwenyekiti wa CCM wa kata alichukua mabati ya kuezekea shule. Kuna choo hapa Halmashauri cha mnadani hapa kilipaswa kikamilishwe ili kihudumie takribani wananchi 5,000. Halmashauri ilitoa milioni 8 na nikiwa kiongozi nilihamasisha milioni 4 zikatolewa na wanakijiji lakini mpaka leo choo hakijakamilika. Walinifanyia fitina nikaondolewa kwenye uenyekiti na katibu wa wilaya wa CCM. Halafu akamuweka mtu mwingine anaitwa Daud Saruya kuwa Mwenyekiti kinyume cha sheria na bila kupata ridhaa ya wananchi. Mapato na matumizi hasomi. Walinitoa kwasababu nilikuwa nawanyima uhuru wa kufanya upigaji wa fedha na mali za wananchi", alisema Magige na kushangiliwa na wananchi.

Magige aliongeza kuwa ameamua kujiunga Chadema ili aweze kushirikiana na wananchi katika kupigania maendeleo kwani imejiridhisha kuwa haiwezekani kusimamia maendeleo ya wananchi akiwa CCM kutokana na kuwepo kwa vigogo na viongozi wa kiserikali waliokuwa wanajaribu kumdhibiti na kumtaka aongoze kwa maslahi yao binafsi badala ya wananchi.

Akimpokea Kiongozi huyo, aliyeonekana kuungwa mkono na umati mkubwa wa watu waliohudhuria mkutano huo, Mbowe alisema:

"Kwanza ninampongeza sana kiongozi wangu huyu kwasababu ya kuwatetea wananchi na kukataa kutumika kuwadhulumu wananchi hawa. Ndugu yangu Magige hata kama ungebaki na uenyekiti huo wa CCM ambao nao uliupata kwa dhuluma, bado cheo hicho kisingekuwa na maana. Cha msingi ni kuwa bado unaweza kuwa Mwenyekiti halali na ukaendelea kuwatetea wananchi wako kupitia Chadema. Karibu sana Chadema

Pili, nawaagiza viongozi wangu wa Chadema Mkoa na majimbo, fuatilieni suala hili, iwe ni kwa Mkuu wa wilaya au Mkoa au mamlaka husika, hakikisheni mkutano mkuu wa kijiji unafanyika na wananchi hawa wanapata haki ya kumchagua Mwenyekiti wa kijiji kihalali", alisema Mbowe na kushangiliwa na wananchi.

Mbali na Magige, wengine waliojiunga Chadema ni wajumbe wa serikali hiyo ya kijiji, ambao ni: Juma Jumbe, Muriri Ghati na Joseph Wamburs Mang'ang'a

Awali katika mkutano huo, wananchi walieleza kuwa wanakabiliwa na kero kubwa ya kukosa maji safi na salama, wachimbaji wadogo kutopewa vibali vya uchimbaji dhahabu na kuwapo kwa mgogoro wa ardhi wa muda mrefu, ambapo wananchi 94 maeneo yao yalichukuliwa na Jeshi ili kupisha uwekezaji wa mgodi wa Buhemba mnamo.mwaka 1985.

Hoja ya wananchi ni kulipwa fidia, lakini mpaka leo wananchi 94 wanaoathiriwa na mgogoro huo, bado hawajalipwa.

Akizungumzia jambo hilo, Mwalimu, alisema Chadema inao uwezo mkubwa wa kutatua kero sugu zinazowakabili wa-Tanzania na kwamba inachohitaji ni kuaminiwa na kupewa mamlaka na wananchi.

Mwalimu amesema wamekuwa wakikutana na vilio vya wananchi kila mahali, wakiwaomba wawasaidie kuzitatua huku wakijua kuwa wao sio wenye Serikali.

" Ndugu zangu wa Buhemba, naona mabango yenu yanayoelezea kero zenu ikiwemo mgogoro wa kutwaliwa kwa ardhi yenu na Kampuni ya Meremeta mwaka 1985. Tunasikitika nanyi katika hili, lakini zaidi ya kupiga kelele hatuna cha zaidi. Kinachopaswa tupeni mamlaka tuwasaidie", alisema Mwalimu.

Alisema mgogoro huo wa ardhi umekuwepo tangu mwaka 1985 lakini umekuwa ukipigwa danadana na viongozi wa serikali kwa kusukumiana mpira, huku Seriakli ikiwa ni moja na ya chama kimoja kwa wakati wote wa mgogoro huo.

Mwalim ambae alikuwa mgombe Mwenza wa Urais wa Chadena kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ameelezea haja ya wanachi kuamua kuongozwa na Chadema kuanzia kijiji hadi taifa na kukiwezesha chama hicho kutekeleza sera zake.

Akizunguzmia uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu wa 2025, Mwalim amesema hapo ndipo pakuanzia na kutoa rai kwa wanachama wa chama hicho wenye nia ya kugombea kujitokeza na kusajili nia zao kwa mamlaka husika za chama.

"Tuna amini kuwa tunazo sera zinazoweza kuwasaidia lakini hatuna mamlaka...mwakani ni uchaguzi wa serikali za mitaa, anzieni hapo kwa kuchagua Chadema"
View attachment 2739416
 
Hongereni sana kitengo cha media, naona mpo active sana mitandaoni kuanzia YouTube, Twitter, JamiiForums n.k. naomba Kasi hii iendelee mpaka 2025 tuwe tunapata updates on time za kampeni na matukio muhimu ya chama.
 
Back
Top Bottom