Tawi la CHADEMA kufunguliwa USA

Exactly Bro. The best they can do to support CHADEMA ni kama ifuatavyo badala ya kufungua tu matawi:-

(i) Kwa dini yako, kwanza iombee Tanzania na watu wake; halafu ombea CHADEMA na viongozi wake Mungu awalinde hasa katika kipindi hiki kizito ambacho maadui ni wengi.

(ii) Isaidie CHADEMA kwa michango ya hali na mali; mambo yanayotakiwa kufanywa ni mengi mno but resources are so limited.

(iii) Wakati wa kujiandikisha na kupiga kura kwa uchanguzi wowote tokeni huko Marekani na kwingine mliko; rudini nyumbani muipigie kura CHADEMA.

(iv) Fundisha watoto na watoto wa watoto wako, ndugu, jamaa, na marafiki zako kuyashika yote yaliyoelekezwa katika (i), (ii), (iii) hapo juu.

This is the best you can do for CHADEMA and Tanzania in general.

They need to a little bit organised to do what you are advising. Good comment anyway.:tonguez:
 
Kwenye buluu hapo; Why the first and not the later mkuu? Who should "convince the govt" to allow voting overseas? Nadhani ungepaswa ujue kazi ya tawi la chama cha siasa mahali popote kabla ya kusema this and that is the "best".
Hapo kwa red: Nina mashaka makubwa na hii comparison broo! Hivi unaweza kufananisha siasa za marekani na Tanzania? Unaelewa kwanini hawa wanaitwa democrats na wale republicans? Sasa je unaelewa kwanini hawa wanaitwa CHAMA CHA MAPINDUZI na wale CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO na wale NCCR na wale CUF na wale PPT MAENDELEO?

The Best thing is to try to convice the GVT to allow people to Vote Overseas and not kufungua Tawi;

Kwasababu ina Maana watu wa huku watakuwa wanatafuta Ruzuku toka Makao Makuu ya Chadema kama CCM? itakuwa ni Wizi Mtupu angalia USA hawana Tawi la Republicans or Democrats nje ya nchi yao, kwanini sisi Masikini?
 
hongera titan kazeni but pia nakupa 100% dudus mchango wako ni muhimu kwa cdm yetu:A S-rose:
 
imekaa njema nyie fungueni tu wala hakuna shida...hawakawiii kusema mmpepewa pesa na marekani....ahahahhahaha
 
When this copy and paste trend is going to stop? Just like them same route same crap, you can't defferenciate between the two, they dance the same tune, I wonder what will be the next move!

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Correct. Kama CDM itaanza kuiga CCM, basi by extrapolation kuna hatari nayo ikaja fikia kuwa gamba. Waacheni CCM na matawi yao. Nyinyi wafuasi wa CDM mnaoishi nje ya nchi mna nafasi n yingine nyingi za kuisaidia CDM bila kufungua matawi huko. Kwanza sidhani kama katiba inayatambua matawi ya aina hiyo

1. Imitate what is good, shun what is evil.

2. Be of more objective and of less subjective.
 
acha unafiki wewe,ni lini ulikuwa cdm ww? Ebu rudia michango yako ya nyuma hapa jf kama ujielewi.

michango yake ya nyuma haimfanyi kutokua mwana chadema,
labda alikua haikubali na sasa ameona kuna matumaini ndani ya chadema
 
CDM inahitaji watanzania wote kuisaidia nchi yao kufikia utawala bora na maendeleo ya kweli ya Mtanzania. Inahitaji wapiga kura na elimu ya kutosha ya uraia kwa watu wake. Inahitaji wanachama wengi kadri inavyowezekana. Inahitaji michango mingi ya mali, elimu, sayansi na technologia kwa ajili ya kusaidia kuifanya nchi iendelee.

wajibu mkubwa wa walio nje ni kuwa chachu ya maendeleo ya kijamii, kielimu, sayansi, demokrasia nk kwa nchi yetu. Ni vizuri kuwa na matawi, ila kabla kuanzishwa kwake ni lazima kufanyike utafiti wa nini itakuwa faida, na mwelekeo wa matawi haya. Ikizingatiwa sheria haziruhusu kupiga kura nje ya nchi.

Je kukiwa na matawi kutawafanya wote wenye nia njema kuwa huru kusaidia chama kimawazo, na kimaendeleo?

USA walipokuwa wanahangaika na health care bill, walifanyautafiti mkubwa na waliangalia kwa kina nchi zenye mfumo kama ule waliokuwa wanautaka ili kuona kama ni vipi walifanikisha kuwa na health care kama waliokuwa wakiitaka, waliangalia nchi kama Canada, na nchi za scandinavia.

Sio jambo geni kuwa na vyama vya siasa nje ya nchi, bangladesh walikuwa na mkusanyiko wa wabangadesh ukiongozwa na Dr Yunus wakaweza kuitengeneza Bangladesh kuwa nchi. Ghana walifanikiwa kuitoa serikali iliyokuwa madarakani kwa msukumo wa watu walioishi nje. Italy ilisaidiwa na walio ishi nje ya italy. Singapore vile vile ilisaidiwa sana na wananchi wake walioishi nje ya nchi.

Matawi ya nje ni lazima yawe yana mission sio utitiri tu wa matawi usio na kichwa wala miguu. huwezi kuwa na Tawi nje ya nchi la kudumu. Kazi za siasa haswa zinahitajika kwenye uwanja husika. Wengi walioanzisha matawi ya nje ni kwasababu ya hali ya kisiasa haikuwaruhusu kufanya kwa ufanisi kazi za siasa kwenye nchi zao.

Ili kuisaidia Tanzania ni vyema kuanzisha taasisi za kusaidia maendeleo, kutetea haki za binadamau, mazingira, uwekezaji na haki elimu kwa jamii. kupitia haya tutasidia sana CDM ambayo tayari imeonyesha nia ya wazi kuwakomboa watanzania. Vikundi kama hivi huwa vinasikilizwa sana kwani huwa havionekani vimeegemea upande mmoja wa shillingi.

Naipenda sana CDM na ningefurahi sana ingekuwa na matawi nje ya nchi ila nafikiri kunahaja ya kuangalia mtandao mzuri utakoisadia zaidi kuliko matawi ambayo hayatakuwa na kazi kubwa. Wapo watanzania wengi nje wanaoitakia mema Tanzania hasa kutoka mikononi mwa CCM. Na wanapenda sana kuisaidia CDM kwa hali na mali bila kuwa wanachama.

Wakati tunafikiri kuwa na matawi hasa sisi wanachama hai, tujadili ufanisi wa hayo matawi, yasije yakawa matawi jina.

Nafurahi kuona njozi zikiwa kweli
Mbona kama kuna watu wanawasiwasi na jambo hili. Kama tawi linafunguliwa liwe moja kwa US nzima.. ndio ushauri wangu..

Mwankijiji wazo lako ni zuri sana, ila kwa ukubwa wa USA sidhani kama malengo yatafikiwa. Kama nia ni kuunganisha watanzania na kuwezesha harakati za nyumbani sio rahisi watanzania wa USA kuwa na Tawi moja kutokana na uhalisia wa maisha na umbali kutoka state moja hadi nyingine, wapo Watanzania wengi wanaishi state moja for the rest of their stay in USA kutokana na kazi na umbali wa interstate.

Ushiriki na utambuzi wa vipaji ni muhimu sana, ikizingatiwa state za US zinajitegemea kiuchumi na kiutawala. Tunahitaji kuwa na mtandao US nzima kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi, human resourses na technological know how. Ni mawazo tu.
 
Back
Top Bottom