Tawi la CHADEMA - Kongwa kwa waishio Dar na Pwani, kwa mapambano

Jul 31, 2012
22
3
Habari wanajf, habari wanakongwa,rejea na kichwa cha habari,

Ndugu wanajamii, wanakongwa tuishio Dar na Pwani, tumekusudia kufungua tawi la CHADEMA hapa mjini kwa ajili ya kuratibu shughuli za kichama kwa wanakongwa waishio Dar na Pwani.

Tawi limepewa baraka zote kutoka kwa mwenyekiti wetu wa wilaya ndugu Juma Chibiriti na sasa tunaomba nguvu zetu tuziunganishe ili kupambana na mkoloni mweusi ambaye anazoletesha maendeleo yetu:

Naomba kuwakilisha kwenu kwa maoni na ushauri.

Pamoja tutaijenga Kongwa yetu.
 
Safi sana inatakiwa tujenge kabisa ofisi ya kisasa .najua hapo kongwa viwanja bei rahisi pia tofali za kuchoma,itisheni mchango muweke na namba ya Mpesa tuwatumia mchango.
 
jamani hongereni sana sasa na sisi wa CHILONWA ebu tuamkeni basi mambo ya maccm sitaki kuyasikia magamba kabisa


Nafikiri ni hili ni wazo zuri sana na kama kuna kitu kinaweza kufanyakazi vizuri kuwaondoa ccm huko vijijini ni mfumo wa namna hii.
Karibia asilimia kubwa ya watu wenye uelewa wa mambo yanavyokwenda wako mijini lakini wametoka vijijini. Ni kitu kizuri kama wanaweza kujimobilize wakapeleka msaada wa elimu ya uraia katika maeneo ya majimbo waliyotoka ili kuwahamasisha wananchi wajue kinachoendelea na mwelekeo wa vijana wao walioko mijini.

Mimi napendekeza kama wapo wakazi wa jimbo husika kwenye mji fulani basi wafungue tawi dada la jimbo lao kwa ajili ya kulisaidia jimbo lao. Tawi hili litakuwa ni onestop kwa ajili ya ku coordinate mambo yote ya chadema kwenye jimbo lao! Mjini kuna watu wa aina nyingi kwa mfano wanafunzi wa vyuo wanaweza kutumika wakati wa likizo kwenda kuhamasisha jimboni kwao hivyo wanakuwa coordinated na hili tawi dada. Kwa sasa hivi ni ngumu mtu kujitolea pesa au muda wake kwenda jimboni kufanya kazi za uhamasishaji labda kama anataka kugombea. Ninaamini watu wengi sana wanapenda kujitolea ila wanashindwa kwa sababu wanakosa mtu wa ku coordinate na wanapojitolea wanataka wayaone matunda ya kazi yao pia!

Otherwise huu uzi ni muhimu sana. Ungefaa uwekwe kwa namna ambayo kila jimbo watafungua jimbo dada kwenye miji mikubwa walipo wakazi wa jimbo hilo.
 
hii habali ni njema kwangu nakumbuka CHADEMA kongwa mikutano inafanyika pale kwa mwenyekiti( mzee juma )
sijui kilicho mtoa WHITE hadi akajiunga na magamba ni nn ingawa ni mwenyeji wa mpwapwa ktk hilinawaunga mkono ni lini tunakutana na wapi
 
Back
Top Bottom