Tatu ntimizi huchoki uongozi mama?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,149
Ntimizi awania uenyekiti UWT Tabora
Lucas Raphael, Tabora
Daily News; Friday,November 28, 2008 @20:01

Mbunge wa Igalula, Tatu Ntimizi amejitokeza kuwania uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora. Licha ya Mbunge huyo, pia yumo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Mwasiti Ngesi, Mwalimu Lucy Kayanda na mfanyabiashara Maimuna Mohamed.

Akizungumza na gazeti hili, Katibu wa UWT wa Mkoa, Martha Kanakamfumu alisema watu hao wanne ndio pekee waliojitokeza kuwania nafasi hiyo. Alisema kazi ya kuwachuja wagombea hao inaendelea na itafanyika chini ya Kamati ya Siasa ya Mkoa.

Alisema vikao vyote vya jumuiya hiyo vitafanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za UWT kwani kwa sasa ni vikao vya ndani ndio vinaendelea. Alisema uchaguzi wa jumuiya hiyo mkoa unatarajia kufanyika Desemba 6, mwaka huu katika ukumbi wa mkutano wa Kituo cha Wanafunzi mkoani hapa.

Uteuzi wa wagombea kwa jumuiya hiyo wamelazimika kurudia kutokana na mgombea mmoja kati ya wawili waliokuwa wameomba kukosa sifa. Hivyo kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kilichoketi mwanzoni mwa mwezi huu mjini Dodoma, kiliamuru nafasi hiyo itangazwe upya. Wagombea hao ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Urambo, Martha Susu na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Mwasiti Ngesi.
 
Mama Mia what is ur basis...? Umri? au perfomance au Elimu au nini?

au Hidden chuki ktk Nafsi zako?
 
Lakini unajua kuwa hayuko peke yake? Mbona hujamzungumzia Msekwa? na wengine wengi wanaong'ang'ania madarakani?
 
Wote ni walel wale jamani!!!!hawana maana kabisa
 
Huyu mama nimeanza kumsikia since nikiwa najikojolea mpaka leo

mi toka tumboni mwa mamayangu mkuu!!!
 
ndio aliefanya kipindi fulani mzee kifimbo akamuwekea bifu baba MALECELA!!!
aliposikia mzE MZIMA ANAKOKOTA MACHINE!!!WE......PALIKUWA HAPATOSHI
HE NAMWONA MPAKA LEO..LOH!!!!!!!!
 
Mama apumzike kwani anataka nini?analea wajukuu kwa post za kutudumaza demokrasia nchini?kwani lazima yeye?si awaachie wenzake amesahau nini kwenye uongozi?hata wa chama....apumzike....hii karne sio yao tena,maana hana jipya ....................
 
Katika nchi kama Tanzania ambako UONGOZI si UTUMISHI bali ni UTAFUTAJI na hivi kugombewa kwa gharama yoyote, kung'ang'ania UONGOZI ni jambo lisilokwepeka. Si rahisi kuachia uongozi katika hali hiyo. Ntimizi, kama walivyo akina Msekwa, Malecela, Makamba, Kingunge n.k.; baadhi ya Wabunge - Lubeleje, Shelukindo, Mzindakaya, Makweta na wengine wengi (orodha ni ndefu), hawawezi kung'atuka na kuwaachia vijana walete mawazo mapya kwani kwao suala si UTUMISHI bali UTAFUTAJI. Ubinafsi umewazidi kiasi cha kutojali maslahi ya Taifa. Yanayotokea sasa, ufisadi, rushwa n.k. ni matokeo ya kuendelea kuwa na viongozi watafutaji wenye mawazo mgando. Kiongozi mtumishi hujali maslahi ya taifa lake na kamwe hawezi kujihusisha na ufisadi kama ilivyo kwa viongozi, karibu wote, hapa Tanzania.
 
Duu?? kumbe ndo tatu huyu wa mwaka 47? Jamani huyu bibi antafuta pessure za bure, asubilie ale pension yake na amalizie ngwe yake kwa raha.
 
Duu?? kumbe ndo tatu huyu wa mwaka 47? Jamani huyu bibi antafuta pessure za bure, asubilie ale pension yake na amalizie ngwe yake kwa

ngumu rwabigiri watakuuliza wakale wapi ??????????

au watoto wao wasome wapi!!!we mpka leo ajasomesha mmhhh m sisemi!!!
 
Viongozi wetu hawako madarakani kwa maslahi ya wananchi zaidi ya kujineemesha kwa gharama za wananchi wasiojua haki zao,nasisitiza wananchi wasiojua haki zao kwasababu nafasi kama ya mbunge wananchi wanahusika kwa kuwachagua.Tuna sheria nzuri sana inayomzuia rais kuwa madarakani zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano,kunatatizo gani kama sheria hii makini itawahusu pia mawaziri,wakuu wa mikoa na wabunge ?.Bila kuwa na uko kwa nafasi kama za wabunge tutaendelea kuwa na wabunge wa aina ya Makweta,Mzindakaya,Shelukindo na kingunge.
 
Lakini nafikiri kumsema huyu mama ni kumuonea kabisa kwa kuwa jamaa wa rika lake bado wako wanapigania madaraka. Akina Malecela ambaye alikuwa unaburuza ule mzigo pamoja na akina Kingunge, Msekwa na wengine wengi tu wamemzidi huyu mama umri. Labda kama utasema kuhusu tatizo lake la elimu. Sijui hata huko jimboni kwao anawapa nini maana mama ni kilaza kwelikweli. Nakumbuka one time FMES alidai kuwa wakati akiwa waziri wafanyakazi walikuwa wanamkacha kuongozana naye safari za nje. Fikiria waTZ wanvyohusudu safari na marupurupu!!!!!
 
Lakini nafikiri kumsema huyu mama ni kumuonea kabisa kwa kuwa jamaa wa rika lake bado wako wanapigania madaraka. Akina Malecela ambaye alikuwa unaburuza ule mzigo pamoja na akina Kingunge, Msekwa na wengine wengi tu wamemzidi huyu mama umri. Labda kama utasema kuhusu tatizo lake la elimu. Sijui hata huko jimboni kwao anawapa nini maana mama ni kilaza kwelikweli. Nakumbuka one time FMES alidai kuwa wakati akiwa waziri wafanyakazi walikuwa wanamkacha kuongozana naye safari za nje. Fikiria waTZ wanvyohusudu safari na marupurupu!!!!!

Basi hiki kimeo
 
Back
Top Bottom