Tatizo si uislam

Nishasema mara kibao hapa ukumbini kuwa tatizo linalotukabili hapa Bongo ni UFISADI na kukosa viongozi wenye maono, uzalendo na upendo kwa watu wao, lakini kwa makusudi kabisa kuna WAPUMBAVU ambao wanatumiwa na MAFISADI ili kutuondoa kwenye hoja za msingi na mshikakamano wa kuweza kuliondoa kabisa tatizo hili la UFISADI. Angalia inapokuja hoja ya ufisadi katika viongozi wetu basi haraka kuna watu wanaidaka juu juu na kuihusisha na udini.Watu hao wanafahamika hapa jamvini japo kwa ID zao,hawa hawataki kusikia ufisadi wa JK na genge lake na kumficha katika mwamvuli wa udini, huu ni ujuha wa hali ya juu kwani athari za ufisadi zinatukumba watu wa dini zote kwa mfano tatizo la mgao wa umeme na kupanda kwa asilimia karibu ya 20% ya bei ya umeme.Hao mafisadi wanatanua watakavyo na wenyewe wana mshikamano wao kwani wenyewe ni wa dini tofauti na wengine hata dini hawana sasa sisi walalalhoi tunaishia kuparurana kwa misingi ya dini.

Watu kama wewe pia ni tatizo sio tuu Tanzania ila hata humu JF. Watu tunapinga huo UFISADI tena kwa kiasi kikubwa. Watu wanachohoji kwa nini tuchague awamu au wakati wa kuupinga huo ufisadi na wakati mwingine tunashadidia? Ufisadi ulianza kushika kasi wakati wa Mkapa, kumbuka mawaziri ambao waliachishwa ama kujiuzulu kwa ufisadi kama Mbilinyi, Ngasongwa n.k. mbona viongozi wa kanisa walimkalia kimya Mkapa? Sasa hivi wako mstari wa mbele (si vibaya) kwa sababu ni rahis kumu-attack mtu asiye ndugu yako. (Give a dog a bad name then kill it)!. Kikwete kwa sababu ya uislamu wake amekuwa easy target kwa christian activists kwa kisingizio cha ufisadi! HILO NDIO TATIZO AMBALO SIAMINI KAMA UNAWEZA KUWA HONEST ENOUGH UKAKUBALI

Pia neno ufisadi limepunguzwa maana ili kulenga tatizo fulani tu! Kwa kiarabu au kiingereza neno hilo lina maana pana zaidi ya 'wizi wa mali ya uma" ambalo sasa ndio tafsiri inayopendwa. kama UFISADI ungekuwa unachukiwa kwa maana yake halisi tusingemshangilia na kumpa leeway mtu mzima anayechukua mke wa mtu (hawara) na kutangaza mchumba wake! Hii ni moral decay na ndio ufisadi namba moja! Mi naweza kumsamehe mtu anayeniibia pesa lakini SIO ANAYENICHUKULIA MKE WANGU! Sijui wewe!

Ngoja nikupe maana za Ufisadi (CORRUPT, CORRUPTION)
v. cor·rupt·ed, cor·rupt·ing, cor·rupts
v.tr. 1. To destroy or subvert the honesty or integrity of.
2. To ruin morally; pervert.
3. To taint; contaminate.
4. To cause to become rotten; spoil.
5. To change the original form of (a text, for example).
6. Computer Science To damage (data) in a file or on a disk.

corrupt [kəˈrʌpt]
adj 1. lacking in integrity; open to or involving bribery or other dishonest practices a corrupt official corrupt practices in an election
2. morally depraved
3. putrid or rotten
4. contaminated; unclean
5. (Literary & Literary Critical Terms) (of a text or manuscript) made meaningless or different in meaning from the original by scribal errors or alterations
6. (Electronics & Computer Science / Computer Science) (of computer programs or data) containing errors

vb 1. to become or cause to become dishonest or disloyal
2. to debase or become debased morally; deprave
3. (tr) to infect or contaminate; taint
4. (tr) to cause to become rotten
5. (tr) to alter (a text, manuscript, etc.) from the original
6. (Electronics & Computer Science / Computer Science) (tr) Computing to introduce errors into (data or a program)
 
lakini mbona ni kimbilio la waislamu?..................hivi huamini kuwa uislamu unaruhusu ushirikina....hebu tembelea misikiti yote utakuna nje ya misikiti hasa siku za kumuabudu allah wao kuna waganga wa kienyeji.....hii sio story ni ukweli.........hii ndiyo dini ya allah

Basi bwana Jile79,

Nimechoka kujadiliana na watu ambao wameshaconclude katika vichwa vyao kuwa Uislamu haufai. Mie nimeusoma uislamu ndani nje nje ndani. Tena si hivyo tu nimeusoma na ukristo pia, sasa nausoma uhinduism kama hobby. Uislamu unasema madhambi makuu ni haya:-
a. Ushirikina - ndio nambari 1 na dhambi ni mmungu mwenyewe ameapa mwenye kumchallenge kazi yake hana msamaha nae.
b. Uzinzi- Hili msamaha utaupata ukitubu ila mmungu anajua zaidi.
c. Fitna- hawa wanamoto unawasubiri.
d. Kiburi- Huyu akishirikiana na Fitna watasaidiana motoni.
e. Uongo- huyu msamaha ataupata akiacha na kutubu.
f. Kuvunja ahadi- huyu ni sawa na muongo.
etc...

Sasa nikuulize huoni kama ni contradiction uislamu umeuweka ushirikina dhambi ya kwanza kuu halafu wewe unasema unaruhusiwa Uislamu gani unaousema wewe?
 
lakini mbona ni kimbilio la waislamu?..................hivi huamini kuwa uislamu unaruhusu ushirikina....hebu tembelea misikiti yote utakuna nje ya misikiti hasa siku za kumuabudu allah wao kuna waganga wa kienyeji.....hii sio story ni ukweli.........hii ndiyo dini ya allah
Mtu mwenye dhana mbaya huwa ana maradhi ya wasiwasi na huwaogopa watu... uugua kwa dhana yake mbaya, mwili na roho yake huugua pia. Kisha usababisha aonekane mzee kabla ya wakati wake. Kwa sababu tabia hiyo isiyofaa huathiri vibaya mfumo mkuu wa fahamu na tezi za mwilini, na kusababisha ugonjwa wa utahahira wa kifikra kiasi cha kujenga chuki akilini mwake na kupelekea kujichukia yeye mwenyewe...!
 
tatizoni uislamu...dini ya chuki na visasi

Nikuulize kwanza umeanza kusema Uislamu unaruhusu ushirikina na misikiti yote unayoifahamu wewe washirikina, sasa unabadili mwelekeo kusema uislamu ni dini ya chuki na visasi, Haya tuambie wapi kumezungumziwa chuki na visasi.
 
Kwa nini basi viongozi wa dini ya Kiisilamu hawamsaidii. Wanamwogopa siyo? Ana nini cha kutisha? Msaidieni kwa kumdadavulia kilichopo kwenye kitabu. Ananikera sana mimi.

Katika uislam kila kitu kiko wazi, ni juu yako binadamu kukubali au kukataa.
Uislam unagawa binadamu katika mafungu makuu mawili, (1) wanaokubali kuwepo kwa mola na (2) wanaopinga kuwepo kwa mola.
Na hao wanaokubali kuwepo kwa mola nao wamegawanywa katika makundi mawili, (a) waumini; hawa ni wale wanaofuata hukumu za mola bila kubagua na (b) wanafiki; hawa ni wale wanachagua amri za kufuata.
Wanaofuata mafundisho sahihi ya uislam hao ndio waumini wa kweli. Muumini wa kweli kamwe hawezi kuwa fisadi wa aina yoyote ya ufisadi.
Kwa bahati mbaya binadamu wengi tumo katika makundi ya wanafiki (munafiqun) na wapingaji (qafir) ndio maana waliopewa mamlaka ya kuongoza katika dini huogopa kuwaambia ukweli wale walio na mamlaka katika uongozi wa siasa. (MUHIMU: uislam hautenganishi dini na siasa, sababu kwa mujibu wa uislam dini ni mfumo mzima wa maisha ambao binadamu anapaswa kuufuata ktk saa 24, siasa ni sehemu tu ya vitu vingi vinavyofanywa na binadamu ktk saa 24). Kwa kifupi watu wako kibiashara zaidi kuliko kidini.
ZINGATIA: UISLAM NA MUISLAM NI VITU VIWILI TOFAUTI. Utamtambuaje muislam wa kweli???!!!!!!, tenga muda na sikiliza maneno yaliyomo katika nyimbo hii

Last edited by a moderator:
lakini mbona ni kimbilio la waislamu?..................hivi huamini kuwa uislamu unaruhusu ushirikina....hebu tembelea misikiti yote utakuna nje ya misikiti hasa siku za kumuabudu allah wao kuna waganga wa kienyeji.....hii sio story ni ukweli.........hii ndiyo dini ya allah

Bwana mungu aliyenena na mussa katika mlima sinai akusamehe ewe jile79 kwa kuwa hujuwi ulitendalo!!!!!!
Ushirikina ni dhambi isiyosameheka mbele ya mola. Wale unaowaona misikitini wakiuza dawa za mitishamba sio waganga wa kienyeji kama unavyodai na unavyotaka watu wakuamini. Wale wataalamu wa tiba za asili, ambao hutibia watu kwa kutumia mitishamba. Wale hawana tofauti na wamasai waliozagaa mitaani wakiuza dawa za kimasai; pia hawana tofauti na wachina wanaouza dawa za kichina na pia hawana tofauti na akina fulani wenye famasi zao wakiuza dawa za kizungu huko mitaani.
Kama una tatizo la nguvu za kiume usisite kuwaona wale masheikhe, wataalamu wa tiba za asili, watakupa dawa utapona na ndoa yako itastawi, wale sio washirikina. Na kama una tatizo la chango kwa wanawake, pia tiba yake inapatikana, nenda ukatibiwe.
Na wale wanaokwenda kwa sheikh yahya kupiga ramli wale sio waislam wa kweli yaani waumini bali wale ni wanafiki. Uislam umekataza kupiga ramli (kutazamia nyota) na kamari. Ni sheitwan ndio anawashawishi waende kupiga ramli.
Ukitaka kuujua uislam tafuta vitabu uusome na wala usisikie maneno ya katika vijiwe vya kahawa na kuyaweka kichwani mwako!!!
 
Religious leaders should be capable of realizing the manipulation of politicians. Tumeona hata jana, kwenye kuwaombea marehemu waliopigwa risasi hapa Arusha na "polisi" kiongozi wa waislamu alijizuia kutoa maneno yoyote ya kukemea kilichotokea ili asiwaudhi viongozi wa nchi huu ni uoga na sidhani kama uislaumu unaruhusu uoga wa namna hii !!!!

Hakujizuia bali Hakuona haja ya kurudia kulaani kile kilicho laaniwa tayari
 
Tanzania haina dini bali wananchi ndio wenye dini,hivyo katiba inawaruhusu wote kuabudu pasipo kuvunja sheria.Uislam uko wazi pia hivyo msiojua tuulizeni tuwafundishe.Uongozi katika Uislam unamaadili yake mfano kiongozi lazima awe mtusafi na akubalike kwa tabia njema na awe mwadilifu katika uongozi wake.Kiongozi awapendelee na kuwahurumia raia wake kwa kuwapa huduma yao inayostahili.Sasa anapopewa Muislam kungoza anatakiwa aongoze kwa kivuli cha Uislam na kwakua kama Tanzania haina dini basi Muislam huyu itabidi kwanza awe mnyenyekevu mbele za Mungu na pia atekekeleze sheria za nchi.Kama mtu anajina na hafuati ule mwelekeo wa Uislam kwa kutenda haki basi yuko mbali na Uislam pamoja na Mungu,kwa maana anaifuata na kuiabudu nafsi yake na matamanio yake binafsi.Hivyo MAFISADI na WEZI wahukumiwe kwa dhambi zao na usiandamwe Uislam kama wengi wafanyavyo hapa JF.Anayefanya dhambi hizo uislam hauko naye na tayali wamejitenga wenyewe kwa kuukanusha Uislam.Uislam siotatizo bali tatizo ni wao viongozi.Ingelikua ni sheria ya Uislam kwa kubainika kashfa kiongozi anang'atuliwa.Hivyo kama JK ana matatizo msimuhukumu kwa DINI yake bali muhukumuni yeye kama yeye na si UISLAM na Waislam.

Thanks a lot nimeipenda sana.
 
Hivi tunapambana na Chama au tunapambana na mtu maana kila kukicha wanabadilisha ,ikiwa tunania basi cha kuandamwa ni Chama Chao Cha CCM humo wamo wote wakiristu na Waislamu ,ila tukibaki na Kikwete 2015 wanamweka mwingine,mikilalamika na Makamba kesho kutwa wanamuweka mwingi ,tulalamike na Chama na sio watu.Natumai nchi haina mrengo wa dini na halikadhalika Vyama navyo havina udini ,tuikoromee CCM.
 
CITYBOY said:
Tanzania haina dini bali wananchi ndio wenye dini,hivyo katiba inawaruhusu wote kuabudu pasipo kuvunja sheria.Uislam uko wazi pia hivyo msiojua tuulizeni tuwafundishe.Uongozi katika Uislam unamaadili yake mfano kiongozi lazima awe mtusafi na akubalike kwa tabia njema na awe mwadilifu katika uongozi wake.Kiongozi awapendelee na kuwahurumia raia wake kwa kuwapa huduma yao inayostahili.Sasa anapopewa Muislam kungoza anatakiwa aongoze kwa kivuli cha Uislam na kwakua kama Tanzania haina dini basi Muislam huyu itabidi kwanza awe mnyenyekevu mbele za Mungu na pia atekekeleze sheria za nchi.Kama mtu anajina na hafuati ule mwelekeo wa Uislam kwa kutenda haki basi yuko mbali na Uislam pamoja na Mungu,kwa maana anaifuata na kuiabudu nafsi yake na matamanio yake binafsi.Hivyo MAFISADI na WEZI wahukumiwe kwa dhambi zao na usiandamwe Uislam kama wengi wafanyavyo hapa JF.Anayefanya dhambi hizo uislam hauko naye na tayali wamejitenga wenyewe kwa kuukanusha Uislam.Uislam siotatizo bali tatizo ni wao viongozi.Ingelikua ni sheria ya Uislam kwa kubainika kashfa kiongozi anang'atuliwa.Hivyo kama JK ana matatizo msimuhukumu kwa DINI yake bali muhukumuni yeye kama yeye na si UISLAM na Waislam.

CITYBOY,

..haya matatizo ya udini na kashfa za kidini yaliingia Tanzania mwaka 1986.

..kuna kikundi cha wahubiri wa imani moja kilianza mahubiri ya kuhoji na "kukashifu" maandiko matakatifu ya imani nyingine.

..inasemekana viongozi wa dini mbili kubwa waliitwa ikulu kwa Raisi ili waweze kusuluhishwa.

..baada ya kusikiliza pande zote, inasemekana Raisi, aliridhika na hoja za wale wenye imani ile iliyokuwa "ikikashifu" na "kudhihaki" imani nyingine.

..Raisi akawaelekeza viongozi wa imani iliyokuwa "ikikashifiwa" na "kudhihakiwa" kwamba they just have to deal with the new REALITY.

..tangu wakati huo Raisi huyo akaonekana ni mtu asiyetenda haki mbele ya imani ya wale waliokuwa "wakikashifiwa." waumini wa imani hiyo wakaanza kufukua kila baya alilofanya Raisi huyo.

..waumini wa ile dini iliyokuwa "ikikashifu" nao wakaona sasa wamepata Raisi ambaye ni "mwenzao", na wakamtetea kwa kila jambo hata alipoharibu kazi.

..hali imekuwa mbaya zaidi sasa hivi kwasababu kumeanza kuzuka ama vikundi, au madhehebu madogo madogo, katika imani kuu mbili nchini. kwa msingi huo ni vigumu sana kuudhibiti udini kwasababu hakuna center ya uongozi, au central figure, ambaye ana kauli ya mwisho kuhusu mwelekeo wa waumini wake.
 
Nishasema mara kibao hapa ukumbini kuwa tatizo linalotukabili hapa Bongo ni UFISADI na kukosa viongozi wenye maono, uzalendo na upendo kwa watu wao, lakini kwa makusudi kabisa kuna WAPUMBAVU ambao wanatumiwa na MAFISADI ili kutuondoa kwenye hoja za msingi na mshikakamano wa kuweza kuliondoa kabisa tatizo hili la UFISADI. Angalia inapokuja hoja ya ufisadi katika viongozi wetu basi haraka kuna watu wanaidaka juu juu na kuihusisha na udini.Watu hao wanafahamika hapa jamvini japo kwa ID zao,hawa hawataki kusikia ufisadi wa JK na genge lake na kumficha katika mwamvuli wa udini, huu ni ujuha wa hali ya juu kwani athari za ufisadi zinatukumba watu wa dini zote kwa mfano tatizo la mgao wa umeme na kupanda kwa asilimia karibu ya 20% ya bei ya umeme.Hao mafisadi wanatanua watakavyo na wenyewe wana mshikamano wao kwani wenyewe ni wa dini tofauti na wengine hata dini hawana sasa sisi walalalhoi tunaishia kuparurana kwa misingi ya dini.

Mungu akubariki umeongea point ya msingi kuliko mtu yeyote humu JF katika siku za usoni.
 
Religious leaders should be capable of realizing the manipulation of politicians. Tumeona hata jana, kwenye kuwaombea marehemu waliopigwa risasi hapa Arusha na "polisi" kiongozi wa waislamu alijizuia kutoa maneno yoyote ya kukemea kilichotokea ili asiwaudhi viongozi wa nchi huu ni uoga na sidhani kama uislaumu unaruhusu uoga wa namna hii !!!!

Hapana! Si sawa kuwapangia viongozi wetu wa dini nini waseme na wapi waseme!
 
Religious leaders should be capable of realizing the manipulation of politicians. Tumeona hata jana, kwenye kuwaombea marehemu waliopigwa risasi hapa Arusha na "polisi" kiongozi wa waislamu alijizuia kutoa maneno yoyote ya kukemea kilichotokea ili asiwaudhi viongozi wa nchi huu ni uoga na sidhani kama uislaumu unaruhusu uoga wa namna hii !!!!
Ulitaka wakemee ili huo msikiti ugeuke mwembechai ya Arusha? Siku zote kama mnakumbuka waislamu wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki katika nchi hii, lakini mara zote ndio wamegeuzwa kuwa wahanga wa maguvu ya serikali. Ama hamjui ni mara ngapi watu wamepigwa na hata kufikia mbwa kuingizwa misikitini? au hamkumbuki pia ni misikiti mingapi hii leo inaendeshwa kwa misingi ya serikali (mmojawapo ni ule anaouongoza Khalifa Khamis ambaye hata uraia wake una utata mpaka leo!) Neno 'UOGA' katika uislamu halipo bali kuna "TAFAKURI na HEKIMA" lazima kwa sasa hali ilivyo viongozi wa kiislamu watazame upande wa pili pia. hatuhitajii kuona misiba ikiongezeka bali tunahitaji kuizuia. Napenda kuwaambia ndugu zangu waTanzania

"ENYI WANASIASA, MICHEZO YENU NDIO MAUTI YETU"
 
Tanzania haina dini bali wananchi ndio wenye dini,hivyo katiba inawaruhusu wote kuabudu pasipo kuvunja sheria.Uislam uko wazi pia hivyo msiojua tuulizeni tuwafundishe.Uongozi katika Uislam unamaadili yake mfano kiongozi lazima awe mtusafi na akubalike kwa tabia njema na awe mwadilifu katika uongozi wake.Kiongozi awapendelee na kuwahurumia raia wake kwa kuwapa huduma yao inayostahili.Sasa anapopewa Muislam kungoza anatakiwa aongoze kwa kivuli cha Uislam na kwakua kama Tanzania haina dini basi Muislam huyu itabidi kwanza awe mnyenyekevu mbele za Mungu na pia atekekeleze sheria za nchi.Kama mtu anajina na hafuati ule mwelekeo wa Uislam kwa kutenda haki basi yuko mbali na Uislam pamoja na Mungu,kwa maana anaifuata na kuiabudu nafsi yake na matamanio yake binafsi.Hivyo MAFISADI na WEZI wahukumiwe kwa dhambi zao na usiandamwe Uislam kama wengi wafanyavyo hapa JF.Anayefanya dhambi hizo uislam hauko naye na tayali wamejitenga wenyewe kwa kuukanusha Uislam.Uislam siotatizo bali tatizo ni wao viongozi.Ingelikua ni sheria ya Uislam kwa kubainika kashfa kiongozi anang'atuliwa.Hivyo kama JK ana matatizo msimuhukumu kwa DINI yake bali muhukumuni yeye kama yeye na si UISLAM na Waislam.

City Boy Bakwata nao ni waislam? nikiwaangalia huwa naona kama huwa wanasupport uovu wa serikali (I stand to be corrected), jumuia za kikristo zikikemea maovu wao wanaongea the opposite. Ni kupingana na wakristo au intentionally huwa wanatetea uovu?
 
Thread ilikuwa inaendelea vizuri, tena ninampongeza aliyeanzisha. Ila naona bado mambo yanataka kurudi kwenye udini tena.

Ni muhimu watu wakamsifu au kumlaumu kiongozi yeyote bila kujali na kuhusisha dini yake. Kwa kweli inakera inapokuwa labda ninamsifia Mwinyi, mtu mwingine anaona ninamsfia kwa sababu ni Mimi ni Muislam. Hali kadhalika, ninapo mtetea Mkapa kwa mfano, hamna haja ya kunishambulia kuwa mimi ni Mkatoliki. Cha muhimu ni points zangu ziwe wazi, kuwa Kiongozi fulani ni mzuri kwa vile alifanya A, B, C, na Kiongozi fulani ni mbaya kwa sababu X,Y,Z.

Suala la vyama pia ni hivyo hivyo. Ni makosa kwa great thinkers kuvihusisha vyama na dini fulani, kwa sababu tunaona wazi, vyama vyote vina watu wa dini zote.

Hongera tena kwa aliyeanzisha hii thread, na wale wanaotaka kuleta uislam na ukristo na uninini wachangie kwenye zile thread zingine.
 
CITYBOY,

..haya matatizo ya udini na kashfa za kidini yaliingia Tanzania mwaka 1986.

..kuna kikundi cha wahubiri wa imani moja kilianza mahubiri ya kuhoji na "kukashifu" maandiko matakatifu ya imani nyingine.

..inasemekana viongozi wa dini mbili kubwa waliitwa ikulu kwa Raisi ili waweze kusuluhishwa.

..baada ya kusikiliza pande zote, inasemekana Raisi, aliridhika na hoja za wale wenye imani ile iliyokuwa "ikikashifu" na "kudhihaki" imani nyingine.

..Raisi akawaelekeza viongozi wa imani iliyokuwa "ikikashifiwa" na "kudhihakiwa" kwamba they just have to deal with the new REALITY.

..tangu wakati huo Raisi huyo akaonekana ni mtu asiyetenda haki mbele ya imani ya wale waliokuwa "wakikashifiwa." waumini wa imani hiyo wakaanza kufukua kila baya alilofanya Raisi huyo.

..waumini wa ile dini iliyokuwa "ikikashifu" nao wakaona sasa wamepata Raisi ambaye ni "mwenzao", na wakamtetea kwa kila jambo hata alipoharibu kazi.

..hali imekuwa mbaya zaidi sasa hivi kwasababu kumeanza kuzuka ama vikundi, au madhehebu madogo madogo, katika imani kuu mbili nchini. kwa msingi huo ni vigumu sana kuudhibiti udini kwasababu hakuna center ya uongozi, au central figure, ambaye ana kauli ya mwisho kuhusu mwelekeo wa waumini wake.
inasemekana..... Tusimame katika ukweli mara zote. Udini Tanzania umeingia toka mwaka 1965 na ukathibitishwa rasmi miaka michache iliyofuatia. Wote wanaofahamu na wanaofuatilia siasa za tanzania wanaujua ukweli. Wala haukutokana na Mihadhara wala hizo kashfa unazozisema. Kwani maana ya kashfa ni nini? Ikiwa kupingana ndio kashfa basi jua ya kwamba walipowakisimama wahadhiri wa kikristo kwenye majukwaa (Padre Nkwera na wengineo - hiyo ni kabla ya 1986 unayoisema) na kuutaja UTATU, hiyo ni kashfa kubwa kwa UISLAMU, Je huo tuuite ulikuwa uchochezi wa kashfa za kidini. Mambo ya Mihadhara yanafanyika kote duniani na mwisho wa siku watu wanarudi kwenye masuala ya msingi. Nimepata kutoa mifano hapa na kufasiri maana ya NENO KAFIIR neno hili asili yake ni Kiarabu kwa kiswahili likiwa na MAANA "MPINGAJI" hivyo basi mathalan hata kisiasa, KAFIRI WA CHADEMA NI CCM na kinyume chake. Ukinijia ukaniambia Masiha ni Mungu au Mwana wa Mungu je ikiwa Imani yangu i kinyume na hivyo uone HUJANIKASHIFU!? ikiwa ndio maana ya Kashfa!!! Hivyo basi nami nikikwambia Imani yangu iko kinyume nawe IWEJE hapo iwe NIMEKUKASHIFU? Mihadhara ni hiyari ya mtu kwenda ama kusikiliza. Je tuseme TV ya AGAPE inawakashifu Waislamu? au Redio za Kiislamu zinawatusi WAKRISTO? Na laiti ikiwa hivyo ndivyo basi GAZETI LA AMKENI linaongoza kwa KUUKASHIFU Ukristo ikiwa kinyume na imani ya mmojawapo ni kashfa kwa mwingine!! haya hayakuanza leo ya kashfa za kidini kama ikiwa ndio maana halisi ya kashfa. Walikua wageni wakaziita DINI ZA KISHENZI, IMANI ZA KISHENZI kwa babu zetu, Nadhani huenda hizi zilikuwa sifa njema kwa baadhi ya watu!! HAZIKUWA KASHFA!!! Tunapojadili tusitazame tumeangukia wapi twende mbali zaidi ya hapo.

TUSIPENDE MAJIBU RAHISI KWENYE MASWALI MAGUMU.

UDINI NCHI HII UNASABABISHWA NA UBINAFSI, CHOYO, WANASIASA KUWATUMIA VIONGOZI WA DINI ZAO, WAUMINI WENZAO KWA MASLAHI YAO, SIASA MBOVU NA VIONGOZI KUTOWAJIBIKA IPASAVYO.
 
kwani kina mtu hapa anamlaumu kikwete kwa uislam wake? kama yupo niambieni ni nani ili nimrushie jiwe. mie bado kuelewa sawasawa
 
Thread ilikuwa inaendelea vizuri, tena ninampongeza aliyeanzisha. Ila naona bado mambo yanataka kurudi kwenye udini tena.

Ni muhimu watu wakamsifu au kumlaumu kiongozi yeyote bila kujali na kuhusisha dini yake. Kwa kweli inakera inapokuwa labda ninamsifia Mwinyi, mtu mwingine anaona ninamsfia kwa sababu ni Mimi ni Muislam. Hali kadhalika, ninapo mtetea Mkapa kwa mfano, hamna haja ya kunishambulia kuwa mimi ni Mkatoliki. Cha muhimu ni points zangu ziwe wazi, kuwa Kiongozi fulani ni mzuri kwa vile alifanya A, B, C, na Kiongozi fulani ni mbaya kwa sababu X,Y,Z.

Suala la vyama pia ni hivyo hivyo. Ni makosa kwa great thinkers kuvihusisha vyama na dini fulani, kwa sababu tunaona wazi, vyama vyote vina watu wa dini zote.

Hongera tena kwa aliyeanzisha hii thread, na wale wanaotaka kuleta uislam na ukristo na uninini wachangie kwenye zile thread zingine.
mada ni njema kabisa ulivosema, lakini kuna watu wao wana CHUKI za kidini mioyoni mwao. Na ndio sababu mada yoyote iliyo kinyume na fikra zao hutafuta jinsi ya kuitibua. HAWATAKI WATU WAHUKUMIWE KWA MAKOSA YAO BALI DINI ZAO kana KWAMBA NDIZO ZIMEWATUMA!!! Mimi utanisamehe kwa hili mkuu... namjibu mtu alipoulizia asije akapotea njia tukapata kazi mpya ya kumtafuta na polisi wenyewe ndo hawa!!!

Hivyo basi huwa kuna njia mbili za kwenda nao:

1. Mjinga huelimishwa akaelimika na akawa ni mwenye manufaa na elimu aliyopata bali -
2. Mpumbavu huambiwa ili autambue tu upumbavu wake (napo ni kama akitaka)
 
Back
Top Bottom