nimie
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 525
- 104
Yamesemwa mengi kuhusu migomo na makusudio yake ikihusisha madaktari, walimu na wafanyakazi kwa ujumla wao. Si kwamba hatuoni hali halisi, tuna macho na kwa kweli tunaona. Ukweli ni kwamba, pamoja na kuambiwa kuwa uwezo wa serikali ni mdogo, lakini tunaona jinsi wenzenu waliona nafasi wanavyofaidika na nchi hii. Tunaona na kusikia maliasiri mbalimbali na mahela ya ajabu yanayokwapuliwa humu humu na kwenda kuwekwa huko Uswisi, South Afrika nk. Kweli serikali kama iko puu, lakini mbona fedha nyingi zinaingia mikononi wa wateule wachache? Hiki ndicho kinachotia uchungu na kuwafanya watu wafikie maamuzi yenye muonekano hasi. Mgomo wa madaktari wengi watakufa, wa walimu wanafunzi wengi wanakosa elimu bora, wafanyakazi nao ufanisi unapungua. Watu wamechoka! Ndivyo ninavyoiona hali ya nchi yetu pendwa Tanzania!