NZURI PESA
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 5,959
- 2,938
Nina rafiki yangu ambaye ana mwaka wa nne katika ndoa yao ana tatizo la kutoshika mimba. Wameshaenda hospitali nne tofauti na mumewe kuchekiwa na wameambiwa wote wawili hawana tatizo lolote. Nilipomuuliza je huwa wanafanya kwenye zile siku hatari alijibu ndio huwa wanafanya kwani kila mmojawao ana hamu na mtoto kwa muda huu na hajawahi kutoa mimba maishani mwake.
Tatizo kubwa linamsumbua huyu dada ni kuwa wanataka mtoto, pia mumewe na ameshamuambia mwaka huu ukiisha kama hajapata mimba ni lazima atatafuta mtoto nje ya ndoa ili aitwe baba.
Jamani naomba mumsaidie huyu rafiki yangu kwani hajui tatizo ni nini hadi hashiki mimba, yupo radhi hata kutumia tiba mbadala/ dawa ya asili itakayomsaidia kuweza kushika mimba haraka. Nakaribisha mawazo, ushauri,..... n.k
Ajaribu dawa hii OVA-MIT iliwahi kumfaa Pacha wangu.Inapatikana ktk maduka ya dawa za binadamu