Tatizo la ulevi Rombo: Wanawake wakodi wanaume kutoka Kenya kufanya nao ngono

Jamaa wameamua kuwa wanywaji kukimbia maambukizi. Huko Rombo maambukizi yanatisha. Hao wakenya wanapeleka kilio kwao
 
Muda c mrefu na kwetu machame itakuwa hivi hivi vijana wanapiga viroba na bangi kama hawana akili nzuri,kijana amekauka kwa viroba sura imekunjamana kama mzee. Aisee
 
Kwa sisi tunaotoka Kilimanjaro ukienda nyumbani unaona tatizo kabisa, asubuhi tu wanasema Wanatoa LOCK wanawake wanalalamika wamekuwa wajane tatizo ni Kiroba

mbege.jpg

.............hawa watu hata Yesu amewashindwa ! :becky:
 
Msosi kule upo wa kutosha mihogo ya nini sasa .

Kumbe wewe apana jua ..... Hujaona wanawake Dar wanauza mihogo mibichi kwenye foleni ? wateja wake umechunguza ni kina nani ? wengi wanaotumia ni madereva wa kiume hasa wa malori ya safari ndefu. hawa hua na wanawake kila kituo
 
huu sasa ni udhalilishaji kwa sisi warombo itabidi tuandae maandamano kupinga huu uhuni wa baadhi ya waandishi wa habari. Watu wachache wanahojiwa wanachafua hali ya hewa ni upuuzi kabisa mi sikubaliani nao.[/QUOTE

wanawake uvumilivu umewshinda, midume yao muda wote inasinzia tu. Na midume mingine iko songea mtwara, dar mbeya halafu imeacha wake zao Kilimanjaro, kurudi mara moja kwa mwaka krismass. Lazima mke atafute mkenya loo
 
Tungejua ujira ni ngapi,fasta ningechukua likizo bila malipo,

Hodi Hodi Miss Chaga and the like!!!!
 
Hiyo habari imetiwa chumvi. Niliwahi kufanya kazi Rombo na japo swala la ulevi ni la kweli kwa wanaume lakini wanawake wa Rombo wanafanya sana kazi ngumu na swala la mapenzi halina kipaumbele kwao kiasi cha kuagiza wanaume kutoka Kenya. Mji wa Tarakea ulio mpakani una mchanganyiko wa watu mbalimbali wakiwemo wakenya wanaokuja kwa ajili ya biashara. Kwa hali hiyo machangudoo wapo vilevile. Sikatai pengine kwa hao wanaume wachache walioathirika na pombe baadhi ya wake zao watageukia marafiki za waume zao na si kutafuta Kenya.

Hakuna chumvi angalia leo kipindi cha report maalum ITV saa 3 unusu.
 
Kenya Bar haifunguliwi kabla ya saa kumi na weekend ni saa nane sisi ni saa 24 tunakula viroba na banana wine

Inaonekana eneo la Kenya mpakani na Rombo wanaume wake hawajaathirika na pombe. Kenya hili tatizo ni kubwa kuliko hata Tanzania. Kumbuka wanawake wa central kenya walipoamua kuwachapa hawa wanaume.Pombe haramu haziuzwi baa. viroba vinauzwa hata kwenye maduka ya kawaida. Hata wilaya ya hai ninakotoka hali ni mbaya. wanaume hasa vijana wa 20-30s wamepotelea kwenye pombe. wanalala nazo na kuamka nazo. kazi hawafanyi wanachukua vijimali vya nyumbani hata chakula cha watoto wanaenda kuuza wapate hela ya pombe. wanawake wakikosea wakaweka hela hovyo zinaibwa ili pombe ikanunuliwe. Viroba vimesambaa na kupata umaarufu kupita kawaida. mzigo wa maisha umewaelemea wanawake. huko hai wanadai sababu ni kuanguka kwa zao la kahawa ambapo kumewafanya wanaume wakose shughuli za kiuchumi za kufanya!?! arusha nako hivyo hivyo....maisha magumu yanafanya wanaume wapunguzie mawazo kwenye viroba, matokeo yake nguvu ya kuzaa na kufanya kazi inapotea.
 
Maana hapo wamekutana.
Maana haya wanawake wa huko kwenye mapenzi sio kabisaaa tasteless .
Ndio maana wameenda Kenya kuchukua vimeo wenzao.
 
huu sasa ni udhalilishaji kwa sisi warombo itabidi tuandae maandamano kupinga huu uhuni wa baadhi ya waandishi wa habari. Watu wachache wanahojiwa wanachafua hali ya hewa ni upuuzi kabisa mi sikubaliani nao.

waromboo hoi hoi hoiiii
 
Angalie sasa hivi ITV wanaonesha kabisa huko rombo hali ilivyo..
 
Nimejionea hali ilivyo Rombo kupitia report maalum Itv, Hali ni mbaya akina mama wanalalamika hawapati huduma, uzalishaji mali kwa wanaume ni mdogo sana kwa sababu ya ulevi wa pombe za kienyeji!rai yangu vyombo husika vichukue hatua kali za kisheria dhidi ya hawa watengenezaji. Lasivyo hili ni janga.

ILA NIWAPONGEZE HAWA WACHAGGA!mwonekano wa hayo mazingira haufananii na hao walevi! Najiuliza ni nan wanaojenga huko vizuri namna hyo ilihali wenyeji ni pombe tuu
 
HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO

TANGAZO LA KAZI

Halmashauri ya wilaya ya Rombo kwa kushirikiana na chama cha wanaume rijali Tanzania (CHAWARITA) inatangaza nafasi elfu saba na miatano (7500) za Maafisa Rijali (AR) watakaofanya kazi katika zoezi la uboreshaji wa ndoa rombo na kuiepusha wilaya kutokana na kizazi cha wakenya.

Muda wa Mkataba wa kazi ni mpaka ambapo kina swai Massawe Mushi na kina Mlacha watakapoacha kupiga kilaji na kuurudia urijali wao.

Sifa za Mwombaji
1. Awe ni Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45 mwenye uzoefu katika masuala ya ndoa michepuko au fani inayofanana na hiyo.

2. Mwombaji aambatanishe CV akielezea uzoefu wake katika mapenzi na picha mbili (Passport size)

3. Waombaji ambao si wachagga watapewa kipaumbele.

4. Mwombaji asiwe mlevi maana rombo idadi ya bar na nyumba ni sawa.

5. Mwombaji aambatinishe nakala za vyeti vya magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI kutoka katika hospitali inayotambiliwa na serikali.


Mwisho wa kupokea Maombi ni tarehe 22/05/2015 saa SITA na NUSU usiku. Maombi yatumwe au kuletwa kwa:-

MKURUGENZI WA WILAYA,
HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO,
S. L. P 3040,
KILIMANJARO.
 
Back
Top Bottom