Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,247
- 26,149
Kwa miezi sasa nchi imekuwa ikisumbuliwa na mgao wa umeme
Leo nimeamka na taarifa za DG wa Tanesco kuondolewa Tanesco
Wiki iliyopita ilitrend taarifa ya kampuni kubwa ya Starlink kuanza kazi Kenya huku hapa Tanzania ikiwa ilipigwa danadana za kutosha
Sasa wameenda na Zimbabwe.
Kwa uzoefu wangu wa Tanzania, nchi hii ina tatizo moja serious sana nalo ni kutokuwa na userious kwenye kupanga na kutekeleza mipango madhubuti badala yake tumekuwa watu wa siasa na funika kombe mwanaharamu apite.
Ndo mana kila siku nchi hii tumekuwa tukiishia kuwa wapiga maneno tu huku wenzetu wakiwa wanatuzidi kila siku.
Nimewahi sema humu na leo nasema tena, matatizo ya Umeme na Maji nchi hii ni kwa sababu hatuko serious kwenye mipango madhubuti inayoangalia kesho ila badala yake tumekuwa tukiwaza vyeo, ulaji na siasa tu.
Kwa namna mabadiliko ya tabia nchi yalivyo ni ujuha uliotukuka kutegemea maji kama chanzo cha Umeme na ndo mana ukitokea ukame tu tunarudi kwenye mgao.
Sio hivyo tu. Hata kwenye maji ni ujuha uliotukuka kwa sasa tunategemea mito ambayo kiuhalisia nayo itapungua maji kipindi cha ukame.
Nimalize kwa kusema. Kama hatujabadilika na kuamua kubadilika na kuwekeza nguvu na akili nyingi katika kupanga na kutekeleza mipango madhubuti ili tutoke hapa, kila siku tutaishia kuwa wapiga kelele na siasa na tutazidi kuwa nyuma hadi kihama.