Tatizo la simu kujizima unapoiweka sikioni shida ni nini?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
View attachment 2832180

Umeshawahi kuona simu yako unapoweka sikioni wakati umepigiwa au unasikiliza voice note inajizima ? Je shida inakuwaga Nini unakuta mtu kakupigia simu unaweka sikioni kioo kinazima.

Lazima ujue kwenye simu yako Kuna kitu kinaitwa 𝗣𝗿𝗼𝘅𝗶𝗺𝗶𝘁𝘆 𝗦𝗲𝗻𝘀𝗼𝗿,ni ki hardware kidogo ambacho kinapatikana kwenye simu. Kimeundwa kwa kutumia electromagnetic utumika kupima umbali uliopo kati yako na kifaa unachomiliki.

View attachment 2832181

Sababu kubwa ya kuwepo hii Proximity Sensor
Kulinda maisha ya betri pale unapotumia simu.
Kulinda simu yako isijibonyeze bonyeze kwa bahati mbaya pale unapoweka karibu na sikio lako.

Mfano unapopiga simu au kupigiwa simu na mtu akapokea na kuweka sikioni basi Sensor ya proximity ufanya kazi ya kutambua simu yako umepigiwa hivyo inatoa ulinzi kwa kuweza kuzima simu yako na kioo kuwa (off) unapoweka kwenye sikio.

View attachment 2832182

Hii inakusaidia kuhusu sikio au Uso wako (shavu) kujibonyeza bonyeza Sehemu ya kukata Simu au kujiandika andika pale unapoongea na simu au ukiwa umelala.

Pia utumika kufanya auto brightness kwenye simu yako kwa kuweza kukupunguzia mwanga au kuongeza unapoweka simu yako karibu na sikio au usoni.

Simu%20kuzima%20%E2%80%93%203.jpg


Inafanya kazi kuanzia android version 8 na kuendelea FANYA HIVI ingia setting kwenye simu yako >> Display>> Tafuta Ambient display au lock screen display >> prevent accidental touch utaamua kuweka On au Off.

View attachment 2832183

Ulikua unajua hii au ndo tunakujuza tuachie maoni yako? Usisahau ku tags washikaji tujifunze sote .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom