Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Dawa ya Mtoto kuacha kukojoa kitandani Upate Kwato la N'gombe . Mtoto Apande juu ya Mti kisha umpe hilo kwato la N'gombe alinuse kisha hukohuko juu ya Mti akojoe kisha ashuke afanye hiyo dawa kwa muda wa siku 7 asubuhi na jioni kila siku atapona inshallah

Hii dawa kama ya kiganga.
 
mmmmh mzizimkavu kaniacha hoi,nashindwa nimuamini au nichukulie kama joke?
Bibie Jestina sio joke nichukulie Serious hiyo ni Dawa ya Ukweli au mnataka na sisi tujiite Wajukuu wa Babu Wa Loliondo? ili mpate kutuamini? Mimi basi ni mjukuu wa Babu wa Loliondo niamini hiyo ni Dawa hakuna Dawa Hospitalini ya kuacha mtoto kukojoa kitandani. kama kuna mtu ana Dawa ya hospitali ya kuacha kukojoa Mtoto Kitandani Tafadhali aweke hapa ili ipate kumsaidia huyo mwenzetu Asanteni.
 
mkuu mzizi mkavu, usiwashangae hao wanaokushangaa manake na mie nilikuwa najiuliza kama ww ni mtaalamu wa alternative medicine... not that it is bad. thank for sharing. hujamalizia afu kongoro linalobakia lichemshwe na mama wa mtoto apige supu yake ikiwa na pilipili na ndimu za kutosha. hapo jestina na husninyo watakuamini
 
Kuna sababu nyingi kwa tatizo hilo kwa watoto au umri mdogo miaka 4-10. Inwezekana ni tatizo la kurithi (atrophy) umbile pungufu, kunywa maji mengi karibu na wakati wa kulala,hofu za kushtushawa mchana na kuota usiku, magonjwa kama uti, kisukari, kushindwa kufanya kazi kwa kibofu cha mkojo, ajali, tatizo la figo. Kwa watu wazima, pombe nyingi kupita kiasi, ajali, magonjwa, prostate cancer, madawa ya high blood pressure, kisukari, kujifungua, msongo wa mawazo, ajali, magonjwa nk.

Punguza pombe au acha, fuata mpango wa uzazi salama/hudhuria kliniki, kupunguzwa kunywa vimiminika wakati wa jioni kwa watoto, kupima afya yako.watoto walale mahali salama na wapatiwe uangalizi mzuri. Kula vyakula vinavyorutubisha mwili, matunda , mboga nk. Ttiba ni muhimu mwone daktari kwa ushauri.
 
Habari wana JF,

Kuna mtoto wa kike wa rafiki yangu sasa ana miaka 6 tatizo anakojoa kitandani almost kila siku. jee kuna dawa yoyote ya kienyeji ama hospitali inayoweza kumaliza tatizo hilo?

Msaada plizz...

Kuna kampuni inaitwa TIENS wasiliana nao au ni pm nitakuelekeza utapata ufumbuzi na we utapenda
 
Dawa ya Mtoto kuacha kukojoa kitandani Upate Kwato la N'gombe . Mtoto Apande juu ya Mti kisha umpe hilo kwato la N'gombe alinuse kisha hukohuko juu ya Mti akojoe kisha ashuke afanye hiyo dawa kwa muda wa siku 7 asubuhi na jioni kila siku atapona inshallah

Mbona dawa ngumu na ina masharti hivyo.
 
Je, kuna uhusiano wowote kati ya kukojoa kitandani kwa mwanaume anapokuwa mtoto mdogo na kuwahi kufika kileleni(kupizi) wakati wa tendo la ndoa anapokuwa mtu mzima?

Je, nini suluhisho la matatizo haya?
 
je kuna uhusiano wowote kati ya kukojoa kitandani kwa mwanaume anapokuwa mtoto mdogo na kuwahi kufika kileleni(kupizi) wakati wa tendo la ndoa anapokuwa mtu mzima?
Je nn suluhisho la matatizo haya?

Good research question. Andikia proposal hiyo ufanye, hutakosa donor wa kukupa grant..unaweza ambulia hata PhD! goodluck.
 
Jamani mimi kuna jamaa yangu ana kabinti kana miaka 10. haka kabinti kana tabia ya kukojoa usiku. Na hali hii ni ya mara kwa mara, naomba msaada wenu ili nimuelekeze huyu jamaa yangu namn y kulikabili hili tatizo.
Natanguliza shukurani.
 
Ahakikishe hanywi maji muda mfupi kabla ya kulala na amzoeshe kumwamsha usiku kukojoa.
Asante, ngoja nianze kuweka strategy ya kumuamsha usiku maana sasa maodoro ndiyo hayo hayaangaliki sasa. ukizingatia mazingira yenyewe ya uswazi, hakuna hata sehemu ya kuanika godoro akishalimwaga.
 
Asante, ngoja nianze kuweka strategy ya kumuamsha usiku maana sasa maodoro ndiyo hayo hayaangaliki sasa. ukizingatia mazingira yenyewe ya uswazi, hakuna hata sehemu ya kuanika godoro akishalimwaga.

Kumbe kabinti kako! Haya fanya hivyo, kama kuna dawa wadau watakwambia.
 
asante, ngoja nianze kuweka strategy ya kumuamsha usiku maana sasa maodoro ndiyo hayo hayaangaliki sasa. ukizingatia mazingira yenyewe ya uswazi, hakuna hata sehemu ya kuanika godoro akishalimwaga.

Jipange vizuri, kwenye post # 1 umedai ni kabinti ka jamaa yako na unatafuta ushauri ili nawe umshauri huyo jamaa yako. Hapa (post # 3) unadai upange strategy ya kuwa unamwamsha huyo binti. Lipi ni sahihi? Ni binti yako au ni binti ya jamaa yako? Hata hivyo ushauri uliopewa utabaki kuwa sahihi.
 
Unaonesha ushaanza unyanyapaa! Post ya kwanza umedai ni binti wa rafikiyo lakini post ya tatu inaonesha ni binti yako. Hata hivyo halijaharibika jambo, kama alivyojangia mdau hapo juu....jitahidi kuweka ratiba ya kumuamsha usiku aende kukojoa.
Jamani mimi kuna jamaa yangu ana kabinti kana miaka 10. haka kabinti kana tabia ya kukojoa usiku. Na hali hii ni ya mara kwa mara, naomba msaada wenu ili nimuelekeze huyu jamaa yangu namn y kulikabili hili tatizo.
Natanguliza shukurani.
 
Jamani mimi kuna jamaa yangu ana kabinti kana miaka 10. haka kabinti kana tabia ya kukojoa usiku. Na hali hii ni ya mara kwa mara, naomba msaada wenu ili nimuelekeze huyu jamaa yangu namn y kulikabili hili tatizo.
Natanguliza shukurani.
Kwani wewe ukisema Mwanao wangu ana umjri wa miaka10 anakojoa kitandani kwani utakuwa na aibu gani? kwani humu ndani unamuogopa nani kwenye hii forums? tujaalie ni mimi mwenye huyo Mtoto wangu anae kujoa kitandani Dawa yake ni hii hapa nakupa
Dawa ya Mtoto kuacha kukojoa kitandani Upate Kwato la N'gombe . Mtoto Apande juu ya Mti kisha umpe hilo kwato la N'gombe alinuse kisha hukohuko juu ya Mti akojoe kisha ashuke afanye hiyo dawa kwa muda wa siku 7 asubuhi na jioni kila siku atapona inshallah

Tumia kisha unipe Feedback
 
Mi nilikua na tatizo kama hilo nilipokua premari nikapewa dawa ya kienyiji. Bahati mbaya yule mganga amekufa. Tafuta dawa za jadi zinaweza kusaidia
 
Back
Top Bottom